Hivi kweli kupenga makamasi kwa kutumia kitambaa na hajaa kubwa kwa kutumia tissue na kupiga chafya kwa kutumia kiganja,ni usafi na ndio kustaarabika?

Salary Slip

Platinum Member
Apr 3, 2012
49,126
151,484
Kwa wengi tuliokulia mijini, bila shaka tumeshiriki katika kuyafanya haya na huenda bado tunaendelea kutekeleza huu utamaduni wa kimagharabiki ambao tunauona ni sahihi na ndio kustaarabika.

Tusione aibu na tujadiliane hapa kama kweli hii tabia ya kupenga makamasi na kisha kuweka kitambaa cha mafua mfukoni na hii ya kutumia tissue badala ya maji tukiwa toilet kama ni usafi na ndio kustaarabika?

Tunaweza kuwaponda wazungu, lakini hata huko vijijini kuna wanaotumia majani hata kama wangeweza kusubiri wafike nyumbani ambako maji yanapatikana.

Practice nyingine ambayo huwa inanipa shida na iliyozoeleka, ni hii ya kupiga chafya kwa kutumia kiganja cha mkono baada ya kutumia kiwiko au sehemu nyingine ya mawili mfano kwenye mapaja,n.k.

Mkono huo huo ndio unautumia kusalimiana na watu,kufungulia vinywaji wateja bar na wageni nyumbani n.k, na ukiingia kazini, unautumia kushika mouse ya computer, computer ambayo mnaitumia kwa ku-share na staff wenzako, n.k.

Karibuni kwa mjadala na pole kwa wataoguswa.
 
Kwa wengi tuliokulia mijini, bila shaka tumeshiriki katika kuyafanya haya na huenda bado tunaendelea kutekeleza huu utamaduni wa kimagharabiki ambao tunauona ni sahihi na ndio kustaarabika.

Tusione aibu na tujadiliane hapa kama kweli hii tabia ya kupenga makamasi na kisha kuweka kitambaa cha mafua mfukoni na hii ya kutumia tissue badala ya maji tukiwa toilet kama ni usafi na ndio kustaarabika?

Tunaweza kuwaponda wazungu, lakini hata huko vijijini kuna wanaotumia majani hata kama wangeweza kusubiri wafike nyumbani ambako maji yanapatikana.

Practice nyingine ambayo huwa inanipa shida na iliyozoeleka, ni hii ya kupiga chafya kwa kutumia kiganja cha mkono baada ya kutumia kiwiko au sehemu nyingine ya mawili mfano kwenye mapaja,n.k.

Mkono huo huo ndio unautumia kusalimiana na watu, ukiingia kazini unautumia kushika mouse ya computer, computer ambayo mnaitumia kwa ku-share na staff wenzako, n.k.

Karibuni kwa mjadala na pole kwa wataoguswa.
Kumbe umekulia mjini ndiyo maana unashabikia mambo ya kijinga ya chadema
 
Dalili za kutokuwa na fedha msimu huu wa sikukuu.

Yaani hata treni ya Polepole Return ticket ya Dar - Moshi - Dar tsh 14000/= imekushinda bwashee?!!!
 
Tusione aibu na tujadiliane hapa kama kweli hii tabia ya kupenga makamasi na kisha kuweka kitambaa cha mafua mfukoni na hii ya kutumia tissue badala ya maji tukiwa toilet kama ni usafi na ndio kustaarabika?
Lakini hoja zingine aiseee! Leo umekuwa low sana mwamba! Kwa hiyo kipi bora, kupenga kwa kitambaa au kupenga kwa mkono mtupu? Hiyo ya mkono mtupu ndiyo tabia yetu Waafrika! Pia hatukuwa na utamaduni wa kutumia maji, tulikuwa tunajiburuza chini na kutumia magunzi! Sasa walipotuona tukifanya hayo wakatuletea maji na tissue! Sasa wewe unataka turudi kwenye kujiburuza chini?
 
Back
Top Bottom