Hivi kwanini wanaume wana tabia hii?

ntuchake

JF-Expert Member
Apr 17, 2024
373
1,341
Katika maisha ya kawaida binadam kusaidiana ni kitu cha kawaida. Haijalishi unamfahamu au humfahamu kama mtu anahitaji msaada msaidie tena bila kutegemea kitu chochote in return.

Kuna hii tabia wanaume ukiwasaidia lazima baadae warudi wakutongoze. Sijui huwa wanawaza nini! Umesaidiwa toa shukrani zako kisha nenda haina haja ya kutaka kuleta mazoea mengine.

Nakutana na hili mara nyingi sana nashindwa kuelewa inaonekana msaada ni kitu cha ajabu sana kwa wanaume hawaamini kama mwanamke anaweza kutoa msaada bila kuhitaji chochote kutoka kwao. Maana wao wamezoea hawatoi msaada hasa kwa jinsia tofauti mpaka wahakikishe kuna kitu atapata kutoka kwa mtu anayemsaidia.

Ukisaidiwa shukuru kisha ondoka usitake kuleta mazoea, wengine hatupendi mazoea na shobo zisizokua na maana.
 
Pole
 
Huo pia ni msaada anaohitaji. Kama wewe ni mtu mwema, mpe pia huo msaada kwa mara nyingine halafu mwambie aache mazoea!
Yaani awe anakutafuta tu pale akihitaji msaada.
 
Back
Top Bottom