Thecoder
JF-Expert Member
- Aug 10, 2015
- 1,706
- 4,500
Mimi huwa niko na kawaida ya kutengeneza playlist tofauti tofauti na kuzisikiliza wakati naendelea na kazi zangu (huwa napata utulivu wa kubaki kwenye jambo moja kwa wakati huo, kwasababu kichwa changu huwa kina shida ya kufungua mafile mengi kwa wakati mmoja hasa kikiwa kwenye utulivu wa kutokupokea mambo mapya kutoka nje, hali hii huwa inanifanya niweze kufanya vitu nusu nusu).
Sasa leo kwenye playlist yangu nimejikuta niko na ngoma kadhaa za hao jamaa wakuitwa navy kenzo, na kilichotokea ni kwamba wakati ngoma inahama kutoka kwa hawa jamaa kwenda kwenye ngoma ya msanii mwingine kuna test tofauti kabisa ambayo inatosha kusema ile ngoma iliyopita haiwezi kuwekwa kwenye mzani sawa na hii iliyoingia kutokana na ubora wa sound yake.
Yaani kuanzia kwenye midundo hadi mixing, na uimbaji wao na midundo ni kama imefungana kiasi cha kuleta test fulani ya tofauti yaani ile test ya ki-Grammy Grammy kabisa.
Kila siku tumekua tukistruggle juu ya wasanii wetu kupenya kwenye soko la kimataifa ili hali tobo la kutupeleka huko ni kama lipo wazi kabisa ila ni vile tu hatujaamua, kwa mfano "Nahreel on the beat" ingekua inaskika kwenye ngoma nyingi za wasanii wetu wanaopambana kwenda kimataifa nadhani wangefika wanapotaka kutokana na sound ya jamaa jinsi ilivyo(au nimefika mbali sana😅).
Anyway, unahisi ni nini shida inayopelekea hawa jamaa wakose support kwa mtaa, ukiachana na sababu ya kuyajenga maisha yao kwenye engo ngumu ya kutokufungamana na mambo mengi ya kijamii ikiwemo ya kisiasa (sijui kama wameshawahi kwenda Dodoma kiuoto wa asili hawa), au sound yao iko mbele ya muda sana?.