Hivi kuna ubaya gani kurudi katika misingi iliyo asisi taifa hili.

daza steven

JF-Expert Member
Aug 30, 2016
359
357
Ndugu zangu nawasalimu katika salamu ya kitanzania, bara mpaka visiwani 'mamboo'.

Mimi naomba niulize sisi kama watanzania tunaoipenda nchi yetu kweli, hivi tuna nini cha kujivunia hadi sasa? Je. tunajijuwa au hatujijui? Mbona kama bado tuna zozona kila kukicha wenyewe kwa wenyewe, mbona bado ni sisi ni masikini nchi ya ... kutoka chini hata mimi nashangaa, Tume rogwa? au tuna laana? Kama kuna mzalendo ebu tujadiliane kidogo.

Mimi nimeshangaa kuona kumbe taifa letu la watanzania lilikuwa na misingi yake ambayo Mungu alipotuweka katika ardhi hii ya Watanganyika na Wazanzibari kumbe ilianza na misingi yake.
Na hii misingi ilikuwa ni mizuri ila kwa sababu za kijinga tu, tena za kipumbavu kabisa tukaicha na kushika mambo mengine ambayo hayatuunganishi kabisa, yana turudisha nyuma kila kukicha tena yanazidi kututenga watanazania.
Leo hii watu wanapigania kwa nguvu zao zote Uchama, leo watu wanapigania Udini, leo watu wanapigania Ukabila, Ukanda, leo watu wanapambana kupiga dili chafu. Sisi maskini ambao ni wengi tuna shabikia wajanja wachache ambao wanatuumiza kila kukicha kwa sababu eti ni viongozi.

Tumejaribu mambo mengi sana ya kijinga na yote tumeshindwa vibaya, mengine yalionekana kama yanafaa kipindi tunaanza kuyajaribu, lakini tuligundua kuwa hayakuwa mazurisiyo lakini atukustuka. Tuliacha asili yetu, utamaduni wetu na kuiga watu wengine na kupokea kila jambo pasina kulilinganisha na misingi yetu. Kila tulilolisikia halikuishia masikioni tu sisi tukalijaribu hata kama ni baya kwa kuliangalia tulilijaribu tu. Hatukuwa na hofu tulijaribu kila kitu hata vitu vya hatari.

Badhi ya mambo tuliyo yajaribu:-
Tulijaribu kuuza viwanda/ mashirika ya umma.
Tulijaribu kuua Reli.
Tulijaribu kuua elimu na shule zetu.
Tume jaribu mfumo wa vyama vingi.
Tulijaribu kuua muungano.(serikali tatu)
Tulijaribu kuua bandari.
Tumejaribu kuua Azimio la Arusha, na kuanzisha azimio la Zanzibar.
Tukajaribu kuwaamini IMF na WORLD BANK kwa 900%
Haya ni baadhi tu.

Ebu tuangalie misingi iliyoasisi taifa hili ambayo ilijengwa na awamu ya kwanza chini ya uongozi wa baba wa taifa Mwl. J.K.Nyerere, na misingi hii ilianza tangia TANU na ASP.
Lakini nikianza tu kuandika misingi hii utakuta mtu anachukia, tena anakereka sana eti kwa sababu za itikadi yake ya chama, ukimuuliza misingi hii inaubaya gani anasema haina ubaya wowote ila ina u CCM ndani yeke. (mimi nafikiri umefika wakati sasa wa kusimamia katika ukweli hata kama moja ya karaktalistiki ya ukweli ni mchungu tumeze, tumeze tu na tutapona ) Kwa bahati mbaya au nzuri nchi hii haijawai kuongozwa na chama kingine zaidi ya Ccm, na Ccm ilipokea misingi hii hapo mwanzo na kutokana na ujinga tu Ccm waliiacha misingi hii na cha ajabu kabisa hakuna chama chochote cha upinzani ambacho kilianzishwa na kilidaka misingi hii au kuiendeleza ila navyo vyote viliingia katika kupiga dili kama CCm na vyama vingine kama CUF, CHADEMA, NCCR na vingine hatukuwai kuona vikidaka misingi iliyoasisi taifa hili vyama vyote viliamua kuiacha misingi yetu makusudi. Hivyo mimi naamini chama chochote hakiwezi kutukomboa mpaka apatikane mtu kwanza.

Hii misingi ilichukuliwa kutoka katika ahadi za chama, ikumbukwe kuwa kipindi hicho kilikuwa ni mfumo wa chama kimoja. Na baadaye tulipata kitu kinachoitwa Azimio la Arusha ambalo hadi sasa hakuna kitu chochote kibaya ndani yake labda marekebisho madogo madogo.
Ukiangalia utakuta misingi hii ililenga kujenga taifa lenye utu, usawa na ummoja na mshikamano tofauti na sasa, watu anaona ni sawa tukiwa tofauti katika taifa moja kumbe ni ujinga na ni hatari. Hata waliotuletea vyama vingi hawafanyi hivi wenyewe wana mshikamano wa utaifa wao.
Soma hii misingi alafu ikosoe kama wewe huna vinasaba vya ufisadi au ujinga.
  • Nitaitumikia nchi yangu na watu wangu wote.
  • Nitajitolea nafsi yangu kuondoa ujinga, umaskini, magonjwa na dhuruma.
  • Rushwa ni adui wa haki sintopokea wala kutoa rushwa.
  • Cheo ni dhamana, sintotumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu.
  • Nitajielimisha kwa kadri ya uwezo wangu na kutumia elimu yangu kwa faida ya wote.
  • Nitashirikiana na wenzangu wote kujenga nchi yetu.
  • Nitasema kweli daima fitna kwangu mwiko.
  • Nitakuwa mwaminifu kwa rais wa serikari iliyopo madarakani.
Sasa ukiangalia haya ukichanganya na azimio la Arusha kama tutarudi katika haya na kuyaboresha kuna ubaya gani? Tutakuwa tumekosa nini sisi watanzania maskini.
Angalia 80% ya watanzania bado ni maskini tunajisifu na nini?, na Rushwa, na Ukabira, Uchama, Ukanda, Ufisadi, haya yatatufikisha wapi? Si upuuzi huu, tumesha yajaribu yote na hakuna faida yoyote kama taifa tumeendelea kuumia.

Angalia historia kidogo.
Enzi za mwalimu huduma za kijamii zilitolewa bure na kwa usawa bila kuangalia mtu usoni, kwa mfanao sisi tulipokuwa shule tulisoma pamaoja na watoto wa mawaziri, watoto wa wakuu wa mkuo, watoto wa mkuu wa wilaya, watoto wa wakurugenzi, watoto wa wabunge na watoto wa matajiri wa kipindi hicho. tuliingia darasa moja, tulikuja na miguu wote na kuondoka shule kwa miguu. c tulikuwa maskini? kama kufagia tulifagi na mtoto wa waziri, nakama mtoto wa mkubwa alikosea alilambiswa bakaora tatu matakaoni kama mtoto mwingine yeyote yaani tulikuwa sawa.

Huduma za hospitali zilitolewa bure kwa wote bila kuangalia huyu ni nani wote tulipata huduma katika foleni moja. Hadi tuna fika mwishoni mwa miaka ya 1980's wananchi waliasafiri pamoja na wabunge wao katika mabasi walipokuwa wana elekea bungeni wakitokea katika majimbo yao. Ilikuwa kawaida njiani ukinunua chungwa unagawana na mbunge au korosho mnagawawa kwani mbunge naya alikuwa anaishi katika nchi maskini pia.
Tuliwaona viongozi wakiwa sawa na sisi wananchi hawakuwa juu sana hadi ushangae, wanaokunywa bia tulikutana baa mmoja, wanaokunywa ile ya kupuliza tulikunywa nao pammoja yaani tuliona viongozi wanaowaongoza watu maskini na viongozi wao maskini.

Nakumbuka kama mtu alienda katika ofisi flani ya serikali nakuombwa rushwa, mtaani ilikuwa gumzo watu walishangaa na kuuliza ikawaje, na kwasababu enzi zile watu walikuwa wanaogopa sana polisi walienda kwa mjumbe wa nyumba kumi kumi na kusema kuwa kuna mtu flani anaomba rushwa na haikuchukuwa muda alibainika na kukamatwa. Fisadi hakutamba kabisa.
Kipindi hicho ilikuwa ni ngumu kwa fisadi kutamaba, ilikuwa ngumu kabisa kuibia shirika au serikali, ilikuwa ngumu kutoa rushwa au kupokea rushwa. Sina maana kuwa hakukuwa na rushwa au mafisadi hawakuwepo lahasha walikuwepo lakini walikuwa na wakati mgumu sana.

Nakumbuka ilitokeaga siku familia inapata mtoko siku hizi mnaita OUT, familia moja ililipuka na viwalo kuelekea katika sherehe au sikukuu flulani tuliweza kuona baba, mama, na watoto kama 7au 8 wa familia moja walipendeza sana na nguo kutoka Urafiki au Mwatex au polista Morogoro, viatu kutoka Bora au Moro shuu, au viatu kutoka viwanda vidogovidogo kipindikile tulikuwa tunaviita viatu vya wachaga, kwani wenyewe walijikita katika utengenezajai wa viatu vile. Nini nachotaka kusema tulikuwa wa uzalendo wa dhati kutumia vitu vyetu zaidi kuanzia viongozi hadi wananchi.

Sasa angalia, tulipoingia tu katika mfumu wa vyama vingi ndipo mafisadi walipoanza kupata nguvu, tukaanza kuona viongozi mafisadi, rushwa ikakolea, tuaanza kuona mafisadi ndani ya chama tawala, tukaona baadhi ya mafisadi wakatoka Ccm na kwenda kuanzisha vyama vingine tuka shuhudia ufisadi ukiingia kwa kasi kubwa sana. Tukaona mafisadi ndani ya Ccm, Tukaona mfisadi ndani ya vyama vya upinzani kikiwemo cha kikuu cha upinzani Tanzania Chadema kikiwa na mafisadi. Na tumeshuudia jinsi mafisadi walivyo na nguvu ya kulindana na kujisafisha. tuliana kashfa nyingi za ufisadi kuliko wakati tukikaa ndani ya misingi iliyo asisi taifa hili.

Hivyo hoja yangu ya msingi ni kuwa turudi katika misingi hiliyo asisi taifa hili kwani ipo misingi na ni yetu, Ccm ilijaribu kuiacha na vyama vya upinzani nao hawakutaka hata kutamka misingi yetu nao wakaja na yao.

Na kwakuwa kwa sasa tumepata rais ambaye amenyesha nia ya kizalendo ya kutaka kurudisha hii nchi katika misingi yake, bado nahoji kuna ubaya gani kumpa sapoti sisi Watanzania maskini 80% ambao harizetu ni ngumu, hawa wajanja tuta wakumbatia hadi lini? Kwanini tusikubatie taifa? Na kwanini tusianze sasa hivi na huyu jamaa ambaye amesema hadharani kujitoa sadaka kwanini sasa tusimjaribishe kwa miaka hii michache iliyobaki? Kwani sisi shida yetu ni nini? chama? dini? ukabila au kutambika?
Mh. Jonh Pombe ameomyesha nia ya kumjali mtanzania maskini, hivi mbona tulijaribu vitu vingi kwanini tusimjaribu na huyu jamaa kwa umoja wetu bila kuangalia itikadi zetu.
Mimi nashauri tena tumjaribu na huyu jamaa kama tulivyo jaribisha vitu vingine, tena Mh, huyu anasikiliza ushauri, kwa sababu jamaa anania ya kuturudisha katika misingi iliyo asisi taifa hili ili tuanzie hapo tuende mbele kwa sababu tulipotea kabisa.

Nawasilisha.
0714733111
 
Msingi mkuu upo katika Azimio la Arusha " ITIKADI YA SIASA YA UJAMAA NA KUJITEGEMEA. Dalili ya kuwepo kwa msingi huu imepotea hivyo kila zama baada ya Mwl. Nyerere zinakuja na itikadi mpya tofauti na mwelekeo alioukusudia.
Ninaamini Rais wetu ana nia njema kuturudisha katika misingi ya miiko ya viongozi na utumishi wa umma, matumizi bora ya rasilimali na uadilifu kwa ujumla kwa kupiga vita rushwa, ufisadi na ubadhirifu kivitendo.
Mambo haya yote mazuri yanatakiwa yawe katika mfumo thabiti ili atakapotoka madarakani tusirudi tulikotoka, wasiwasi wangu upo katika ujenzi na uimarishaji wa huo mfumo thabiti ambao utaendeleza haya.
Katiba nzuri ya nchi iliyoboreshwa na kujipambanua katika maeneo ya uadilifu, Dira ya Taifa itakayoainisha vipaumbele vya nchi kwa wakati, Mfumo wa utoaji haki na haki za binadamu, Usaidizi wa taasisi za kidini katika kujenga maadili ni maeneo ambayo yakitazamwa vizuri tunaweza kurudi katika njia tuliyopotea.
 
Makala ndefu na iliyo nzuri sana kusema kweli. Nimependa sana ulivyojenga hoja na usijari kashfa na vijembe kutoka kwa wapinzani wa fikra zako kwani ni kawaida.

Ubaya uliousema ni sisi kupenda kujaribu kila kitu bila kushirikisha vichwa vyetu, tuliweza kuwapa nafasi wazungu watutawale na kufikiria kwa niaba yetu. Leo tumeletewa mdudu demokrasia basi sote ni kama tumepalalaizi. Kumbe jamaa walitaka kutuchanganya, walijua familia yenye misingi na isiyoyumba ni ile yenye kuwa na one center of power na authority na walijua pia, hata nchi ya hivi ni imara sana kimaamuzi kwahiyo haitakuwa rahisi kuwachanganya. Wakaona waharibu hii kitu, kila mmoja awe na uhuru wa kuamua, kuongea na kuamua mambo yake mwenyewe. Kumbe walikuwa wanatuwinda.
Tunajua kunatakiwa kuwa na hierarchy ya command na respect ya orders. Leo si ndani ya familia si ndani ya nchi, hierarchy haieshimiwi, ukiwaambia waheshimu mamlaka wanasema ni kunyimwa uhuru, Uhuru hupi wakati tokea 61 nyinyi mu huru? Mbona hata maandiko yanasema, zitiini mamlaka.

Wewe mtoto leo unataka kuamua uishije, kwani wazazi waliokuzaa hawakujua kwanini unazaliwa? mkitembea mnaonekana wamoja lakini ndani mwenu mmegawanyika kweli kweli, kuna majoka, makenge na mbwea ( ila nyinyi ndo mnaita demokrasia). Mkija kufikia muafaka mshagombana sana, mamlaka zinakwama na zinakosa nguvu kabisa kwasababu eti ya uhuru, ila watu hao hao yakiwakuta wanarudi kuilaumu mamlaka, si mlitaka uhuru bwana?

Huu unafiki unaoitwa "demokrasia" ni mdudu hatari sana kwa maendeleo na maendeleo siyo lazima demokrasia na tunazo nchi mifano zilizoendelea nje ya mifumo mdudu demokrasia na sasa ziko mbali sana
 
Back
Top Bottom