Hivi kuna manufaa gani Rais au kiongozi akitoka katika dini yako ?

Mbingo

JF-Expert Member
Mar 20, 2014
411
230
Tanzania ni nchi ambayo huwa hufanya uchaguzi kila baada ya miaka 5 lakini kwenye kipindi cha uchaguzi viongozi wetu wa dini wamekuwa wakitushawishi kuwa tumchague kiongozi wa dini yetu aka mkristo au Muislamu .
Je kwa waisilamu Kikwete aliongoza kwa miaka kumi je walipata manufaa gani kutokana na uongozi wake?
2.Je tunajua Huyu wa hapa Kazi tu ni mkristo Je wakristo wameshanufaika nini na kama hakuna kwa nini kipindi cha uchaguzi dini zao zinahusishwa naomba kuwasilisha .....!!!!
 
Haya maajabu ya watufulani kupenda raisi awe ni wa dhehebu la kwake yanapatikana Tanzania tu
Napendekeza tungeyapigia kura ili yaingie kwenye maajabu saba ya Dunia
 
Kuna manufaa ya kujengewa makanisa na misikiti, uteuzi kwa kupendelea dhehebu lake.
 
Madaraka ya Rais ni makubwa sana.
Viongozi wa dini wanajua hilo ndio maana kila mtu anajaribu kuvutia upande wake.
Kiongozi mkuu wa nchi yenye mfumo wa utawala unaompa rais madaraka makubwa sana ,anaweza akaamua kumwa mdini au mkabila au mstaarabu mwenye usawa kwa wote.Ni maamuzi yake tu mana hakuna sheria ya kuhoji!.
Kwa hali kama hiyo viongozi wa dini hawana namna ni lazima wajipambanue mapema kuwa wanamuunga mkono zaidi mtu wa dini yao.

Cha msingi kabisa ni kuweka mfumo na katiba inayoweka mamlaka ya viongozi au kiongozi wa nchi kuwa na madaraka ya wastani. Na kuhoji teuzi na utendaji wenye uelekeo wa kuvunja umoja wa nchi.
Bila kuwa na katiba na mfumo wenye uwezo wa kumhoji kiongozi mkuu wa nchi basi tutegemee iko siku ataingia madarakani rais mfia dini na ataiweka nchi chini ya taratibu za dini yake na yeyote atakayejaribu kuhoji atakua amechelewa kwani tayari sekta zote zitakua zimeshabana na kila anga itakua imetanda kanuni za dini yake na mashushu watajaa kila kona kuwachunguza na kuwachukulia hatua kali wale wote wanaohoji juu ya hali hiyo.

Bahati nzuri mwenye nchi yetu mpaka sasa bado hatujaweza kuwa na kiongozi mwenye udini wa kupindukia. Na hii ni kutokana mchuano mkali na makundi tuliyoyazoea ndani ya michakato ya kutafuta wagombea ndani ya vyama vyetu vikubwa.

Mara nyingi nchi inaweza kuelekea huko pale vyama vya kisiasa vinapoanza kutisha na kushughulikia makundi ya kimitandao yenye lengo la kupata wagombea. Mitandao ndani ya vyama inaua sana udini na ukabila.
Ukifanikiwa kuua kabisa mitandao ujue kuna siku utawala utabaki wa kurithishana.
Hapa kwetu kuna baadhi ya vyama vimekua vikiitwa vya kikabila na kikanda kutokana na ukweli kuwa vimakuwa vikishughulikia wale wote waliokuwa wanataka uongozi ndani ya vyama au hata kugombea. Matokeo yake wenyeviti ndio wanabaki kuwa na mamlaka ya mwisho ya kutaka nani agombee na nani ashughulikiwe. Kilichojitokeza ni vyama hivyo kujikuta vinaongozwa na watu wa kabila au ukanda mmoja na wenyeviti.

Kuepuka pia udini na ukabila ni lazima pia demokrasia ndani ya vyama ziwepo ili mtu mwenye hulka za udini na ukabila asemwe kwa uwazi huko huko kwenye vyama ma ashindwe kabisa kupenya huko kwa uwazi.

Demokrasia ya kweli ndani ya vyama ndio dawa halisi ya kuua udini, ukabila na ukanda.
 
Kwa kikwete alifanikishea kuwawekea mahakama ya Kadhi kwenye katiba ya CCM na hata kidogo aiweke kwenye katiba ya nchi although ilipingwa kila kona
 
Serikali ya Tanzania haina dini dhehebu kabila wala ukanda katika kumpata rais haijalishi we nani watoka wapi ilimradi mtz na watu wa chama chako wamekupitisha na wa Tanzania wakikuridhia chebwedaa
 
Kwa kikwete alifanikishea kuwawekea mahakama ya Kadhi kwenye katiba ya CCM na hata kidogo aiweke kwenye katiba ya nchi although ilipingwa kila kona
Siyo kweli kwani CCM ilikuwa na katiba yake na kama ni hivyo mbona haikuwa hivyo swali je kunamanufaa gani kwa waisilamu waliomchagua kwa sababu ya dini yake? Hivi wewe unajua mahakama ya kadhi? Sheria za Kadhi zipo mpaka sasa hivi kabla ya kikwete,
 
Kwa kikwete alifanikishea kuwawekea mahakama ya Kadhi kwenye katiba ya CCM na hata kidogo aiweke kwenye katiba ya nchi although ilipingwa kila kona


Aliyeiweka kwenye ilani ya CCM hakuwa Kikwetu.
Tusimchafue mzee wa watu.

Ilani ile alikabidhiwa na mtangulizi wake

Na ninakuambia kama Kikwete angekua ni mtu wa kuongoza kwa mkono wa chuma bila kusikiliza kelele za walioko nje ya utawala basi leo hii Mahakama ya kadhi ingepita mana ile ndio ilikua ilani ya chama chake.

Kama angewashughulikia wote waliokua wanaipinga nadhani hakuna ambaye angejitokeza kuvunjwa mguu wake. Lakini hata hivyo usikivu wake na kuheshimu demokrasia na maoni ya watu kuliweza kuondoa ile hoja bila vurugu wala vitosho.

Hebu fikiri kama Kikwete angeamua kukataza mtu yeyote au taasisi yoyote kutoa maoni tofauti na sera hiyo ya chama tawala ya kuanzisha mahakama ya kadhi ingekuwaje?
Yani kila mtu au chombo cha habari wakati huo kingepewa jukumu la kusifia tu uzuri wa mahakama ya kadhi bila kupinga kwa kuwa tu ni ilani ya chama tawala. Na kule bungeni iwe ni mwiko kupinga mahakama hiyo kwa mbunge wa chama tawala!!!
Na Gwajima alipoipinga mahakama hiyo angekamatwa na kuitwa mchochezi ingekuwaje?
 
hakuna umuhimu wa moja kwa moja coz serikali haijihusishi na dini ko labda kiongozi yeye binafsi ndo amue awe na kaupendeleo ka upande fulani wa dini ila kwa usawa wa 2017 unambiwa kila abiria achunge mzigo wake maana si kwa uongozi huu
 
Huenda sisi ambao si viongozi wa hizo dini hatujui manufaa yanayopatikana. maana siku za hivi karibuni kuna kiongozi mmoja amekuwa na kauli zenye kututia shaka juu ya mwenendo wa serikali yetu ya sasa. maana taasisi ya kiongozi huyo ilikua mstari wa mbele kwenye awamu iliyopita kutoa miongozo kuhusu katiba na utawala wa sheria. lakini hivi sasa ni mwendo wa kuimwagia sifa tu serikali yetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…