Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Tumeshuhudia katika ziara anayoendelea kuifanya Rais Magufuli, akiwazodoa na kuwakejeli kupita kiasi wabunge wa upinzani wa Chadema!
Nimekuwa nikijiuliza hivi ina maana gani kwa Katiba yetu ya Jamhuri yauungano wa Tanzania ya mwaka 1977, iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2005, ibara ya 3(1) ambayo inaeleza wazi kuwa nchi yetu ni ya kidemokrasia na ni ya mfumo wa vyama vingi??
Hivi wananchi wa Serengeti wamefanya makosa kumchagia Mbunge Marwa Ryoba kuwa mbunge wao??
Kwa maana kwa namna alivyoongea Mheshimiwa Rais na wananchi wa Serengeti ni dhahiri kuwa ana chuki kubwa sana na chama kikuu cha upinzani nchini cha Chadema
Haiwezekani wewe Rais umetoa fursa ya wananchi wa jimbo hilo watoe kero zao na Mbunge wao Marwa Ryoba anasimama kueleza kero zao kwa niaba ya wananchi waliomchagua halafu wewe Rais unaziclash hoja hizo na kuingiza matusi na kejeli dhidi ya mbunge huyo!
Hivi huoni Mheshimiwa Rais kuwa kwa kitendo kile umewatukana wananchi wa Serengeti waliomchagua mbunge huyo??
Tumekusikia pia Mheshimiwa Rais ukitishia kutotoa bajeti ya maendeleo kwenye maeneo yanayoongozwa na wabunge wa upinzani, eti kwa madai wameikataa bajeti!
Kwani kuikataa bajeti Bungeni ni makosa kwa mujibu wa sheria zetu??
Hivi ni kwanini Rais unaleta mgawanyiko wa Taifa hili kwa kiwango cha kutisha wakati Taifa hili linajulikana na Dunia nzima kwa umoja na mshikamano wetu bila kujali itikadi za vyama vyetu??
Hivi ukilinyima jimbo la upinzani Fedha za maendeleo wakati wananchi wake wanaendelea kulipa kodi hivi kwa hilo huoni Mheshimiwa Rais kuwa unakosea sana??
Nitie rai tu kwa wabunge wa upinzani, ingawa siyo jambo jema lakini inabidi lifanyike ni kwa wabunge wote wa upinzani, hususani kutoka chama kikuu cha upinzani cha Chadema kususia kuwepo kwenye ziara hizi za Rais hadi pale atakapojirekebisha na kuwa FAIR kwa wabunge wote wale wa CCM na wa upinzani, hususani wa Chadema
Mungu ibariki Tanzania