Hivi kampuni kongwe inayomilikiwa na Mtanzania (mweusi) ni ipi? Ina miaka mingapi?

KABAKA28

JF-Expert Member
Jun 18, 2014
207
220
Naomba kujuzwa, kampuni gani kongwe inamilikiwa na mtanzania na ina miaka mingapi?
Nini sababu za kampuni kudumu muda mrefu?
Nini unapaswa kufanya kurefusha uhai wa kampuni yako?

Nimeona Japan kuna makampuni yana miaka zaidi ya 500. Sisi kampuni kongwe lina miaka mingapi?

Asanteni.
 
Sababu za zingine
1. Mtanzania mweusi, hatuna roho ya uvumilivu,tunahitaji faida kubwa kwa uwekezaji mdogo.
2.Siri za biashara kutojulikana kifamilia yaani mzee atakuwa na biashara ambayo mke,watoto,ndugu hawaijui na hawajui kiasi Cha frdha mtaji na masoko vikoje,ndo maana akifa na biashara haidumu.
3.Roho mbaya zetu,ikiwa ni watz wakiajiliwa wanakuwa wa kwanza kuharibu hiyo biashara,kuisema vibaya na kutaka mapinduzi ili yeye haimiliki na ikiwezekana kumuua mwanzilishi. Ivyo kampuni nyingi hufa mapema.
4.Tuna biashara janja janja ivyo zinakuwa kwa miaka5/10/20 then zinapotea kwani mwanzilishi atoi Siri,njia au kuandaaa mtu atayemiliki baada ya yeye.
5.Kuwa na uwekezaji usiousisha familia, unakuta mzee anamiliki kampuni flan lakini watoto wake wote wanasomea kitu tofauti, ivyo mzee anakuwa Hana msimamizi.
6. Kampuni ili ikae mda mrefu lazima iwe wazi,iwe na share za kifamilia nyingi , na iwe na wataalam hasa hasa wahindi, ambao wanajua biashara kwa miaka mingi.
7. Zaidi ya hayo ni ngumu mtanzania kuwa na kampuni itayozidi30yrs.
Kwa sasa naishia hapo. Japo sababu ni nyingi sana. Asante.
MJ de Watcher
 
Naomba kujuzwa, kampuni gani kongwe inamilikiwa na mtanzania na ina miaka mingapi?
Nini sababu za kampuni kudumu muda mrefu?
Nini unapaswa kufanya kurefusha uhai wa kampuni yako?

Nimeona Japan kuna makampuni yana miaka zaidi ya 500. Sisi kampuni kongwe lina miaka mingapi?

Asanteni.
Mimi hapa ni mtanzania mweusi tii kama tairi
Namiliki kampuni yangu kongwe ya kuuza majeneza na huduma zote za mazishi pamoja na ukarabati wa makaburi (kwa wakazi wa Dodoma wengi wananijua)
Kampuni yangu ni kongwe nimeanza tangu mwaka 2009
Mpaka leo nimefanikiwa kupanua biashara ambapo nina matawi Dar, Zanzibar, Moshi na Arusha.
Siri ya mafanikio ni ubunifu mfano sisi ndo waanzilishi wa kuuza majeneza used kwa wateja ambao hawana uwezo wa kununua jipya,
Pia tunakodisha majeneza kwa wale ambao hawaziki kwa jeneza wanakodi kwa ajili ya kusafirishia tu.
Nimeweza kuzalisha ajira kwa vijana wapatao 26 na matarajio ni kuongeza matawi mikoa zaidi.
 
Naomba kujuzwa, kampuni gani kongwe inamilikiwa na mtanzania na ina miaka mingapi?
Nini sababu za kampuni kudumu muda mrefu?
Nini unapaswa kufanya kurefusha uhai wa kampuni yako?

Nimeona Japan kuna makampuni yana miaka zaidi ya 500. Sisi kampuni kongwe lina miaka mingapi?

Asanteni.
Kampuni gani hiyo ina miaka 500?
 
Kuna kampuni moja ilikuwa ya serikali ikafa ikanunuliwa keko pharmaceutical industry KPI, inaendeshwa na mbongo Ina miaka 27 kwa sasa, nadhani zipo nyingi tatizo ni kutokuwa na successor wazurii kwenye biashara pale mwanzilishi anapokuwa amechoka ama kufariki waendelezaji mara nyingi ndo changamoto huanzia kwao,
 
IPP
Mohamed Interprise Ltd
Mansour Oil
Kamanga Ferries
Said Salim Bakresa (Azam)
Crdb bank
Sahara Media
Mwananchi Communication
Nyanza Road Works
Aboud Bus
Super Najmunisa
 
Back
Top Bottom