Hivi ile tume ya kurekebisha mishahara ya watumishi iliishia wapi?

Mnyerede

JF-Expert Member
Dec 29, 2016
210
230
Serikali hii ina mbwembwe za ajabu na kupenda kiki kuliko awamu zote zilizopita, wadau mtakumbuka kuwa wakati magufuli akiwa nyumbani kwao chato alitangaza kuwa kuna watu wanaishi kama malaika kwa mishahara minono huku wengine wakiishi kama mashetani kwa mishahara kiduchu.

1. Sote tunakumbuka kuwa aliagiza tume inayohusika na mishahara kupanga mishahara kwa uwiano sahihi. Swali ni kwamba je time ile iliishia wapi?

2.Je mheshimiwa haoni kuwa gharama za maisha zimepanda kuliko wakati wowote au kwa sababu yeye anakula vinono vya ikulu?

3. Hivi wale vijana wanaobrash viatu hawakumueleza hali halisi ya maisha au waliishia tu kumchekea?

4.Hivi hawa watumishi wa serikali walioongezewa makato na bodi ya mikopo pasipo kujali mikataba yao na bodi ya mikopo inasemaje wala kujali gharama za maisha zinazopanda kila kukicha wamlilie nani?

5.Hivi haya matrilioni yanayokusanywa kila mwisho wa mwezi yanaenda wapi au ni kiini macho?

6.Hivi hizi ahadi tamu tamu tunazopewa halafu zinageuka kuwa hewa badala yake maisha yanageuka kuwa magumu na machungu kama sifongo yeye na jk nani mzee wa hewa?

7.Kwa mtu mwenye akili timamu atafikiria kuwa mpaka 2020 hakuna kitu itafanyika zaidi ya mbwembwe na kiki nyingi zaidi ya zile za babu wa loliondo.

KAZI KWENU MNAOENDELEA KUAMINI ALIYE JUU MNGOJE CHINI, MTAKUFA KAMA WALIVYOKUFA WAFUASI WA KIBWETERE!!!

Alamsiki!!
 
Makusanyo ya sasa hivi hayana tofauti na aliyokusanya mzee wa msoga...
 
Makusanyo ya sasa hivi hayana tofauti na aliyokusanya mzee wa msoga...
ila utofauti wao ni kwamba, mzee wa msonga alikua rais wa wanyonge, ila huyo ni rais wa wapigadili. mtaani maisha magumu ila jamaa hasikii vilio vya asiyewajua. kila mtu abebe msalaba wake
 
Nliwakusikia waziri husika akisema tathimini itakamilika february,2017.Wenye taarifa zaidi watatujuza
 
Mwezi huu kwa wadaiwa wa Mkopo Sheria ya Asilimia 15% ya Makato kwny Mishahara inaanza kutumika haijalishi ni Mdaiwa Mpya au wa zamani.

Hiki Chuma kikipelekewa Bajeti ya Mamilion ya Uchaguzi 2020 huenda akaahirisha Kama Congo kuepuka gharama au atapunguza Muda wa Kampeni toka Miezi mitatu hadi Mwezi mmoja!
 
Ulikuwa umeoza wapi? taratibu si ziko wazi, wanaoshindwa kumudu majukumu wafutwe kazi. Lakini wanapohukumu watumishi wote kwa makosa ya wachache sio sawa.
Tulikuwa Tumeoza Mkuu, Ugonjwa Wetu Ulikuwa Sugu Na Tiba Huchukua Muda Mrefu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…