Hivi huu kama siyo umbumbumbu ni nini?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
59,949
119,214
Kwanini Watu wote ( kasoro Mimi ) tukipanda Daladala tukikaribia kushuka Vituo tunavyoshuka hata kama tupo jirani ( pua na mdomo ) na Dereva lakini wote tutahangaika kupaza sauti zetu kwa Kondakta aliyepo nyuma au mbali yetu kidogo.

Je hii hali inaashiria nini? Ni sahihi abiria wanavyofanya au ndiyo pengine uthibitisho wa matatizo yetu ya kufikiri?

Hebu tulijadili hili kwa kina kwani binafsi ninapoona abiria wakifanya hivi huwa nahisi kuwa wana uwendawazimu fulani hivi kichwani kwani haiwezekani Dereva ambaye ndiyo anajua mbele kulivyo na anaendesha gari unaacha kumwambia akushushe na unahangaika kumwambia Kondakta tena kwa kupiga kelele kuwa akushushe.

Uwanja ni wenu katika " kutiririka " zaidi nikijua kuwa kati ya Members 330,000 tuliopo humu JF wanaotembelea magari yao binafsi wakizidi sana ni 23 tu lakini wote 329,977 ni full kupanda Daladala 24 / 7 ( ukibisha basi tu unataka bundesliga " ubishi " na mimi usiyo na maana ) ila ukweli ndiyo huo.
 
Jibu jepesi tu ni kwamba makonda wana asili ya ubabe na kupenda kuabudiwa na abiria ndio maana abiria huwaomba makonda.

NB: Hapo kwenye data zako za wamiliki binafsi wa magari! ngoja watafiti waje nao watolee maelezo.
 
Mkuu Genta oooooops! GENTAMYCINE mi kama wewe, hata nikiwa nimeketi nyuma taarifa zangu za kuchukua atazipata dereva. Makonda hawakawii kujisahaulisha kutoa taarifa kwa dereva akiona dalili ya abiria mbele. Halafu mara nyingi kichwa kiko nje ya gari wala hasikii.
 
mara nyingi tunawaamrisha na kuwakoromea makondakta kwasababu ndio tunawapa hela

Kwahiyo na Dereva nae akikupelekeni mtaroni na mkavunjika miguu yenu, mbavu, ugoko na utumbo kuchungulia nje huku ulimi nao ukipepesa kama nyoka bado tu utaendelea kumkoromea huyo Kondakta unayempa Hela yako?
 
Mwenye gari ni konda, hivyo yeye ndiyo mwenye maamuzi ya kusema shusha hapa, nk. Je kama haujalipa nauli dereva hatajuaje? konda ndiyo kila kitu kwenye hiace na mara nyingi ata hesabu ya tajiri konda ndiyo uwasilisha
 
Ha! ha! mkuu Genta hata suzuki carry inakushindwa sasa unafanya nini duniani, ivi pesa ya bandle unayotumia kupost ungeweka kwenye kibubu tangu 2013 sasa hivi siungekuwa na kiji toyo cha kuzugia.
 
Ni jukumu lao na kazi yao pia. Dereva hatakiwi kubugudhiwa.

Ukiwa bar hata Kama upo karibu vipi na Counter lazima umuite barmaid akuhudumie.
 
Interesting...kuna vitu ni mazoea tu
mfano jaribu kumwambia konda wewe ni 'mteja' wake
uone atakavyo kushangaa
shida ya usafiri inafanya watu wasahau abiria ni 'wateja'
lakini mteja huyu anafokewa,anasukumwa,anajibiwa kijeuri,anatukanwa....
 
Ha! ha! mkuu Genta hata suzuki carry inakushindwa sasa unafanya nini duniani, ivi pesa ya bandle unayotumia kupost ungeweka kwenye kibubu tangu 2013 sasa hivi siungekuwa na kiji toyo cha kuzugia.
Chunga sana kauli zako. Hizo Suzuki carry zinabei sawa na noah huko kwenye ma showroom
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…