Nimekuwa nikifuatilia hoja za wanasiasa, wateule au wenye nia ya kuwa wateule wanatumia maneno ya kughiribu kama kiswahili changu kiko sahihi.
Yaani kila wanapoongea wanatumia msemo "mheshimiwa anataka hivi" au kama mheshimiwa anavyotaka au mheshimiwa ana nia nzuri.
Kwangu mimi naona kama wanatumia "physiological bribe" ambayo sina uhakika kama ipo kwenye kamusi za takukuru lakini kwa uhakika terminology hii inaguarantee their safety in their positions regardless their performance.
Ni vigumu jambo hili kusimamiwa na viongozi wa juu maana kila mmoja anatamani kuwa addressed hivyo na walioko chini yake lakini kama taifa kwa kutamani kuwa na watendaji bora na utendaji bora uwe ndio safety factor ya mtu kazini basi tungeweka limit kama wateule kutumia maneno ya kulaghai viongozi.
Nakuhakikishia kwa asilimia 80, ukijitahidi kutumia maneno mazuri kama hayo kwa viongozi wako, kazini utadumu, vyeo utapanda regardless how mbumbumbu you are. Hii haina tija kwa taifa bali kwa personal feelings tu hivyo tupige marufuku ulaghai huu.