Hivi bodi ya ligi na TFF wanajielewa kweli? Mbona kama wanavyotoa ufafanuzi ndio wanakosea zaidi,au hawajisikilizi wanachosema!

Mister mimi

JF-Expert Member
Apr 29, 2018
201
312
Wanasema Simba hakugomea mechi,ila wao ndio walighairisha.
Swali ni je,kati ya wao bodi na Simba nani alikuwa wa kwanza kutoa taarifa rasmi kuwa hakutakua na mechi?

Simba walitangaza usiku wa kuamkia siku ya mechi kuwa wao rasmi hawatocheza mechi.na kulivyokucha asubuhi ya siku ya mechi bodi ilisema imepokea taarifa ya simba LAKINI MECHI IKO PALE PALE (yaani itachezwa).
Kwa maana ya kwamba kama kuna maandalizi yalikua yanaendea kwa alji ya mechi yaendelee.
Kama mashabiki walikuwa wanajiandaa kusafiri basi wasafiri.
Kama mtu alikua hajalipia kingamuzi na anataka kuona mechi basi alipie.
Kama shabiki alikua stendi anataka kukata tiketi aende kwa mkapa asighairishe.

Kama mjasiriamali alikua anaandaa bidhaa yake kwa ajili ya kuuza uwanjani basi asiache.

Halafu inafika saa 8 mchana siku hiyo hiyo ya mechi bodi inatangaza HAKUNA MECHI SIKU HIYO,hii ni akili au ni nini? Unavofanya maamuzi ya ghafla namna hiyo unakua umefikiria nini!

Gharama za fedha,akili na muda alizotumia mwenyeji kuandaa mazingira ya mchezo nani anarudisha?
Gharama za fedha,muda na matarajio ya mashabiki nani anafidia?
Hasara walizopata wajasiliamali kuandaa bidhaa nyingi afu ziishie kuharibika nani anawafidia?
dabi yetu ni kivutio,kuna watu wanatoka nchi zingine,nani anaibeba aibu yetu kwao na gharama walizotumia?

Muungwana akivuliwa nguo huchutama!
TFF na bodi ya ligi mmeyabeba makosa ya Simba mgongoni mwenu,maana nyie ndio mliosisitiza mechi ipo hata baada ya kupokea taarifa ya Simba,baadae mnasema mechi haipo,Kwahiyo nyie ni vigeugeu?
Hivi mnaweza mkatuambia sababu yenye mashiko iliyofanya muaghirishe mechi masaa matano kabla ya mchezo?

Tutakua tunakosea tukisema mmeungana na simba kugomea mechi ndio maana hamkupeleka wasimamizi wa mchezo ambayo asubuhi mlisisitiza kuwa mechi ipo?
Hivi hamjajifunza kwa Al ahly na zamaleki?

Siwatetei Yanga, ila mnavyotoka kuongea naona ndio mnazidi kujichafua zaidi!

Lililo bora ilikua ni kuomba radhi tu na sio kuonesha ubabe,na hiyo ndio busara ambayo mnaizungumzia!
 
Uoga wa wanasiasa unafanya wazidi kuzidumaza Simba na Yanga, na soka la Tanzania kwa ujumla
 
Hao wahuni walizoea kuifanyia Yanga mambo ya kihuni kwa muda mrefu. This time wataita maji mma! Na ikiwezekana Yanga ikaze mpaka mwisho ili wajifunze kuachana na mambo ya ushabiki maandazi.
 
Wanasema Simba hakugomea mechi,ila wao ndio walighairisha.
Swali ni je,kati ya wao bodi na Simba nani alikuwa wa kwanza kutoa taarifa rasmi kuwa hakutakua na mechi?

Simba walitangaza usiku wa kuamkia siku ya mechi kuwa wao rasmi hawatocheza mechi.na kulivyokucha asubuhi ya siku ya mechi bodi ilisema imepokea taarifa ya simba LAKINI MECHI IKO PALE PALE (yaani itachezwa).

Kama shabiki alikua stendi anataka kukata tiketi aende kwa mkapa asighairishe.

Kama mjasiriamali alikua anaandaa bidhaa yake kwa ajili ya kuuza uwanjani basi asiache.

Halafu inafika saa 8 mchana siku hiyo hiyo ya mechi bodi inatangaza HAKUNA MECHI SIKU HIYO,hii ni akili au ni nini? Unavofanya maamuzi ya ghafla namna hiyo unakua umefikiria nini!

Muungwana akivuliwa nguo huchutama!
TFF na bodi ya ligi mmeyabeba makosa ya Simba mgongoni mwenu,maana nyie ndio mliosisitiza mechi ipo hata baada ya kupokea taarifa ya Simba,baadae mnasema mechi haipo,Kwahiyo nyie ni vigeugeu?
Hivi mnaweza mkatuambia sababu yenye mashiko iliyofanya muaghirishe mechi masaa matano kabla ya mchezo?

Tutakua tunakosea tukisema mmeungana na simba kugomea mechi ndio maana hamkupeleka wasimamizi wa mchezo ambayo asubuhi mlisisitiza kuwa mechi ipo?
Hivi hamjajifunza kwa Al ahly na zamaleki?

Siwatetei Yanga, ila mnavyotoka kuongea naona ndio mnazidi kujichafua zaidi!

Lililo bora ilikua ni kuomba radhi tu na sio kuonesha ubabe,na hiyo ndio busara ambayo mnaizungumzia!
Cha ajabu kingine, kama kweli wao ndo walikuwa wa kwanza kutoa taarifa kuhusu mechi,
1. KITU GANI KILIWAFANYA WAITISHE KIKAO?
2. KWENYE BARUA YAO WAMESEMA SIMBA HAKUTOA TAARIFA KWA YEYOTE, TAARIFA YA NINI?
3. KWENYE BARUA YAO WANUKUU KIPENGERE CHA MGENI KUFANYA MAZOEZI KABLA YA MECHI, WAMEJUAJE KAMA SIMBA HAWAKUFANYA MAZOEZI NA ILIHALI WAO WALIKUWA WA KWANZA KUTOA TAARIFA?
 
Wanatumia nguvu nyingi wanajikuta wanajichanganya tu kwenye maelezo,ni bora wangekaa kimya kuficha madhaifu yao ya makusudi.
 
Muungwana akivuliwa nguo huchutama!
TFF na bodi ya ligi mmeyabeba makosa ya Simba mgongoni mwenu,maana nyie ndio mliosisitiza mechi ipo hata baada ya kupokea taarifa ya Simba,baadae mnasema mechi haipo,Kwahiyo nyie ni vigeugeu?
Fuata taarifa ya mwisho. Wajinga ndio mliendelea kukata tiketi

1742446063202.png
 
Back
Top Bottom