Historia ya 2014 kujirudia: CCM tunapozidi kuimarika chini ya Dkt. Bashiru, kuelekea 2020 CHADEMA wanawaza kugawana mbao ili kibanda kianguke.

FPT

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
1,216
1,848
Mwaka 2014, mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mkuu wa 2015, mjumbe wa kamati kuu na mwanasheria mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu alitoa dukuduku la moyoni mwake kuwa ana nia ya kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa Tanzania wa 2015 kama chama chake kitampa ridhaa. Hayo yote yalipokuwa yanafanyika hivyo CHADEMA , hali ilikuwa tofauti kwa CCM kwa sababu katibu mkuu wa CCM wa kipindi hicho Ndg. Kinana alikuwa anafanya ziara mbalimbali za kukijenga na kukiimarisha chama.

Kauli ya Tundu Lissu ya mwaka 2014 ilichukuliwa kwa hisia tofauti sana na wenye chama na mmoja wapo wa aliyeonekana kukerwa na kauli hiyo ni mzee Mtei na Mwenyekiti Mbowe na maamuzi waliyochukuwa ni kumtosa kabisa 2015. kwa nini alitoswa ilhali alijiona ana vigezo vyote?

Sintofahamu kama ya 2014 inatolewa tena 2019 ,mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mkuu wa 2020. Kipindi hiki ambacho Dkt Bashiru akizunguka nchi nzima kukinadi chama na kukitangaza kwa wenye chama( CCM ni mali ya wanaCCM) ,mtu yuleyule kutoka CHADEMA anatangaza nia ileile ya kuutaka urais mwaka mmoja kabla ya uchaguzi. kwa nini?

Kwa sababu historia inajirudia upya, mtifuano lazima uwepo ndani ya CHADEMA na kila mtu kutoka CHADEMA anajipanga mapema ili kuwafurahisha wenye chama na wanaCHADEMA hasa watangaza nia wanafahamu kwamba mchakato wa kumpata mgombea urais ndani ya chama chao haueleweki hivyo kila mtu anajitangaza kwa uwezo wake na yule ambaye ataonekana tishio ndio atapewa nafasi ili uharibifu ukitokea usilete madhara makubwa .

Uharibifu lazima utokee upinzani hasa CHADEMA lazima upitie msoto kupitia kwa wanachama wake na sasa hivi wanaCHADEMA hawatataka mgeni apewe dhamana ya kugombea na hapo ndipo dhana ya wanachma kugawana mbao ili kibanda kianguke itatimia.

Dkt. Bashiru anafanya kazi iliyokuwa inafanywa na Ndg. Kinana kama Katibu mkuu wa CCM lakini huku kwa jirani unaonekana moshi mkubwa ambao utaonesha moto muda mrefu. watanzania watashuhudia anguko kubwa sana la CHADEMA litakaletwa na wanaChadema wenyewe huku CCM ya Magufuli na Bashiru ikitamba kifua mbele kwa wingi wa kura kuanzia za ubunge hadi Urais.

Historia hii ni karma kwa CHADEMA ambayo hawawezi kuikwepa kwa namna yeyote na hii ni kwa sababu watanzania wanaiombea CCM ili mtifuano usiwepo na hivyo tupate nafasi tena ya kuwaletea kiongozi bora kama Magufuli.

Nasema tena mtikisiko wa CHADEMA kuelekea uchaguzi mkuu 2020 utaleta madhara makubwa sana kwa CHADEMA na kuleta ushindi mwepesi sana kwa CCM kwa ngazi zote za ugombea. CCM tulipata tabu kuyazuia mafuriko ya Lowassa alipokatwa, je CHADEMA mtaweza kuzuia mafuriko ya Lowasa mkimkata?

Kuna vita kali sana ndani ya CHADEMA ya urais kuelekea uchaguzi mkuu na wanachama wapo radhi kugawana mbao/ fito sasa hivi ili hicho kibanda kianguke. Yeyote atakayechaguliwa CHADEMA kama mgombea hakutamzuia mgombea wa CCM kushindwa kwa sababu mgawanyiko wa CHADEMA utaipa ushindi wa kishindo CCM na kuiimarisha ACT-wazalendo.

CCM tusilaze damu ushindi wa kishindo unakuja na ni wa kishindo kikubwa kwa sababu WanaCHADEMA hawajui ni Lowasa, Lissu au Nyarandu kuelekea 2020.

na Karlo Mwilapwa
 
Usisahau nafasi ya AK 47 na pingu za maafande wetu kwenye kuimarika kwa chama chenu na kufifia kwa chama chao
uzuri mnajua kuwa hata mbowe akiwa ndio mwenyekiti wa NEC atajisika aibu sana kuitangaza Chadema imeshinda ilhali haina uwezo wa kushinda hata CCM tukiweka jiwe
 
Back
Top Bottom