official scandal
JF-Expert Member
- Jan 7, 2016
- 389
- 815
Historia: Tukio lilipelekea vifo vya watoto watano - Vituka Folkland mwaka 1997
Mwaka 1997 utabaki kuwa mwaka wa kihistoria kwa wakazi wa eneo la Vituka-Fokoland kutokana na tukio la kusikitisha lilitokea katika eneo hilo.
Ilikuwaje?
Miaka ya katikati ya 1990 ndio miaka ambayo watu wengi walianza kujenga maeneo ya Yombo -huu upande wa Lumo na Vituka Sekondari.
Kulikuwa na shughuli nyingi za ujenzi katika maeneo haya. Moja kati ya mambo yaliyokuwa yakifanyika ni uuzaji wa mchanga kwa hawa waliokuwa wanajenga nyumba zao.
Hii shughuli ya kuuza mchanga ilikuwa imeshamiri sana kiasi ambacho hata watoto wa umri wa kuanzia miaka 12 - 15 nao walikuwa wakikusanya mchanga kutoka eneo la uwanja wa ndege na hatimaye kuuza ili kupata hela.
Nakumbuka wakati huo debe la mchanga ilikuwa shilingi 300-500. Hapa wanafunzi wengi walijiingiza kwenye biashara hii.
Wakati huo nikiwa na miaka 14 nilitamani sana kufanya hii biashara lakini baba na mama walikuwa wakali sana, hawakutaka kabisa sisi kushiriki kwenye kusomba mchanga.
Siku ya tukio...
Nakumbuka ilikuwa kipindi cha likizo fupi ya mwezi wa tisa, tuliamka kama kawaida na watoto wa umri wangu wakawa wapo bize na shughuli ya kukusanya mchanga ili wauze. Kulikuwa na mashimo kadhaa makubwa ambayo watu walikuwa wakichimba mchanga kwa ajili ya biashara.
Siku hiyo vijana hawa wadogo wakiwa katika shughuli ya kukusanya mchanga walikuwa wamechimba shimo ambalo lilikuwa limeingia ndani upande mmoja. Wakiwa wanaendelea na shughuli hii ndipo shimo lilipokatika na kuwafukia vijana 7, wawili wakaweza kuchomoka kwenye mchanga na kuponya nafsi zao.
Hawa vijana waliopona wakatoka na kupiga yowe ili kuomba msaada, raia waliokuwa karibu haswa wakazi wa kando ya reli wakakimbilia eneo la tukio na kuanza kazi ya kufukua kifusi ili kuokoa maisha wa wale watoto watano.
Kifusi kilitolewa lakini kwa vijana wale wadogo watano wakawa tayari wamepoteza maisha.
Vijana wadogo watano, wawili wakiwa wa familia moja wakapoteza uhai baada ya kufukiwa na mchanga.
Ilikuwa simanzi na huzuni kubwa.
Nimekumbuka hii habari kwa kuwa nilikukatana na mama aliyepoteza watoto wawili miezi kadhaa mahali fulani, baada ya kuniona alisema kauli hii ‘’watoto wangu wangekuwa kama wewe sasa hivi kama sio kufa kwa kufukiwa na mchanga’’. Sikuwa na neno la faraja kwa mama huyu; vifo vya watoto wake bado vibichi kabisa moyoni kwake. Ni miaka 27 imepita sasa lakini bado kumbukumbu ya vifo hivi vimebaki kuwa sehemu ya maisha ya mama huyu.
Natumai labda ipo siku atapata faraja na kuendelea kuishi kwa amani.