Historia fupi ya ATC

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
ATC iliendelea vizuri katika awamu Kwanza ya Mwalimu Nyerere hadi mwaka 1985 ailipong’atuka na kumwachia mzee Ali Hassan Mwinyi. Shirika lilianza kupoteza mwelekeo miaka ya tisini.

Kabla ya Rais mzalendo wa Afrika Kusini, Nelson Mandela kutoka gerezani Februari 11, mwaka 1990, Makaburu wa nchini humo walikuwa wamefikia uamuzi wa kudhoofisha maishirika ya ndege ya nchi jirani kwa nia ya wao kubaki wenyewe na Shiria la Ndege la Afrika Kusini na hivyo kutawala anga ya biashara ya ndege kusini nwa Jangwa la Sahara.

Mkakati ulilenga kudhoofisha mashirika ya Zambia Airways, Air Tanzania, Air Botswana, Royal Swazi, Air Zimbabwe na Uganda Airlines. Walilenga baada ya kuua mashirika hayo wafanye biashara kupitia kampuni ya Alliance Air, ambayo walianzisha kama kiini macho kuwachanganya viongozi wetu kuwa ni Shirika la Ndege la Umoja kati ya nchi hizo za kusini na kati ya Afrika na kutoa ndege aina ya B747SP (Special performance).

Ndege hizo ilikuwa wanazitumia wakati wa utawala wa ubaguzi wakiruka kutoka Johannesburg, South Africa kueleka Ulaya na Marekeni bila ya kutua katika nchi yoyote ya Kiafrika kutokana na vikwazo walivyokua wamewekewa na nchi wanachama wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU).

Ndege hizo aina ya B747SP zilikuwa zinatumia mafuta mengi kuliko mizigo inayosafirishwa kuleta faida katika biashara ya ndege hivyo, nchi zilizokubaliana nao zililainishwa ku share hasara hiyo kubwa iliyozingiiza serikali za Tanzania na Uganda mkenge katika biashara hiyo ya kihuni chini ya Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Ami Mpungwe.

Mpungwe alipewa cheo cha Mwenyekiti wa Bodi ya mashirika ya ndege ya nchi za Kanda ya Kusini mwa Afrika, Zimbabwe na Kenya (Air Zimbabwe na Kenya Airways) walikataa uhuni huo.

Baada ya kununua hisa nyingi za ATC, Makaburu waliiamuru menejimenti ya ATC kupunguza marubani 15 na wahandisi 30 na wafanyakazi wengine, ingawa lengo lao zaidi ilikuwa ni kuondoa wataalamu wazalendo kuifuta ATC katika biashara ya Airline za Afrika.

Makaburu Waliilazimisha memenjiment kuuza ndege za B737 –200 (5H – ATC/5H –MRK) Serengeti na Kilimanjaro kwa makampuni ya Afrika ya Kusini kwa bei ya kutupa. Kila ndege moja haikuzidi dola milioni tano. Hapo ndipo walipomaliza mipango yao kuiua ATC na kuanza kufanya kama wanavyotaka. Wakaamua kuleta ndege zao ndogo za ndani, wakaiondoa alama ya Twiga kama alama ya Air Tanzania na kuweka bendera ya Afrika Kusini.

Njia zote za Air Tanzania wakawa wanazitumia kwa faida yao na baadhi ya maafisa wa serikali yetu wakishirikiana nao kulihujumu shirika letu katika eneo la anga. Walipoona wametimiza malengo yao ya kuiuwa ATC wakaamua kuachana nayo na kurudi kwao Afrika Kusini. Lakini shirika lao la ndege South African airways waliendelea kufanya shughuli zao za kibiashara kama kawaida wakiendelea kuruka kutoka Dar/Johannesburg.

Precision Air, shirika la wazalendo, baada ya kuona kuwa haina mshindani katika biashara ya ndege ikaongeza idadi ya ndege na kuongeza wafanyakazi ambao wengi wao walitokea ATC. Hawa ni wataalamu wa ndege wazoefu (Experienced pilots and Engineers) kwa hiyo hawakuwa na gharama ya mafunzo kwa kuwa Serikali ya Tanzania tayari ilishawagharamia kwa lengo la kulitumikia shirika la Taifa ATC.

Baada ya msukosuko huo mkubwa kwa ATC wajanja wakaanza kunyofoa vitega uchumi vya ATC kama Cargo handling, catering, passengers handling, galileo, hangar la Kia – Kilimanjaro Air craft maintenance facilities (KIMAFA) likafanywa kuwa jumba la kuhifadhia maua badala ya kutengenezea ndege.

Viongozi wengi walioteuliwa kuliongoza shirika la ndege ATC na wao pia walichangia kulidhoofisha shirika hilo kwa kutokuwa na vision ya uongozi wa airline na kuchelewa kutoa uamuzi wa kuibinafsisha katika mashirika ya maana kama KLM, Lufthansa, British Airways, Delta Airlines, Trans World Airlines na si South African Airways ya makaburu.

Mwandishi wa Makala hii wanajeshi mstaafu wa jeshi la wananchi wa Tanzania 0785 042078.


Source: ATC ni zaidi ya biashara (1) | Gazeti la Jamhuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…