Hip Hop ya Bongo

Feb 6, 2024
40
60
HIP HOP YA BONGO.

Wasanii wa hiphop wanaunda sehemu kubwa na ya muhimu katika muziki wa Tanzania. Japo kuna watu wanaoamini kuwa ushindani kati ya rappers wa Tanzania umepungua ukilinganisha na wasanii wa kuimba Tofauti na zamani.

Kuna Harakati mbalimbali Mfano okoa Hip hop movement kibao zilianzishwa kuipa support Hip Hop.

OKOA HIP HOP.

Okoa Hip hop ni mradi maalum ulikuwa umebuniwa na msanii Adili a.k.a Hisabati ambaye ambaye alipigana vilivyo kuhakikisha muziki huo unasimama na kufanya vizuri kama ilivyo aina nyingine za miziki hapa nchini najua Hip Hop haina special package kama ilivyo aina nyingine ya miziki kwani wadau wenyewe wametoa macho kwenye bongo fleva ambayo hivi sasa imekuwa ikithaminiwa wakati ni muziki unaoongoza kwa kuipotosha jamii alisema Adili ambaye ndiye alikuwa kiongozi na mbunifu ambaye alianzia mradi huo Enzi hizo..

Wasanii waliounda movement hiyo..

Jay Moe, Adili, Joh Makini, Mansu-Li, Mapacha, Blac, marehemu Salu-Te, Saigon, Magazijuto, Nako 2 Nako, marehemu Geez Mabovu .

Hizi ni baadhi tu ya Harakati mbalimbali zilizoanzishwa Enzi hizo kuokoa Hip hop.

#funguka.

Nini kinafanyika kuokoa Hip Hop Bongo KWA sasa...

Maana true Hip hop rappers Bongo wamepungua KWA 75%

IMG-20240222-WA0195.jpg
 
Kubali ama kataa, hip hop, reaggea, na mnanda, hii miziki imepitwa na wakati, reaggea na mnanda imeshajifia ck nyingi, hiyo hip hop nayo imebaki story tu. Unakumbuka kile kibao kinachoitwa Hip hop haiuzi? Baada ya miaka 20 ijayo hakutakuwa na muziki unaitwa hip hop, hip hop na reaggea ni miziki iliyokuja kwa kazi maalum.
Ukitaka kujua, nitakuhadithia, chunguza kwa umakini, tena umakini uliyoenda shule, kizazi cha miaka 18-35 si wengi wenye kuipenda hip hop
 
View attachment 2913022
Harakati pekee ambayo binafsi yangu naipa uzito kwenye Bongo hiphop na ilikuwa na impact ni Anti-Virus, kwa hakika vinega wakiongozwa na Sugu walifanya harakati hii ndiyo ilikuwa harakati maana ilikuwa na lengo na sababu nyuma yake

Japo walikuja kupatana ila ilisaidia kuexpose vitu ambavyo vilikuwa vinaishia kwa wasanii wenyewe na kutujuza mashabiki vikwazo walivyokuwa wanapita wasanii kwenye baadhi ya media
 
Kubali ama kataa, hip hop, reaggea, na mnanda, hii miziki imepitwa na wakati, reaggea na mnanda imeshajifia ck nyingi, hiyo hip hop nayo imebaki story tu. Unakumbuka kile kibao kinachoitwa Hip hop haiuzi? Baada ya miaka 20 ijayo hakutakuwa na muziki unaitwa hip hop, hip hop na reaggea ni miziki iliyokuja kwa kazi maalum.
Ukitaka kujua, nitakuhadithia, chunguza kwa umakini, tena umakini uliyoenda shule, kizazi cha miaka 18-35 si wengi wenye kuipenda hip hop

Ngoja tubishane.
Unamaanisha nini kusema ni miziki iliyopitwa na wakati, ni wakati gani unao uongelea? Hip hop kitambo ilishindanishwa na dansi, zouk, taarab, kwaito, bhangra, takeu, mduara. Hizo miziki zooote zimepotea ila hip hop Bado ipo. Na huwezi kusema imepitwa wakati wewe binafsi leo hii bado unaishindanisha na afro pop ama amapiano ambazo nadhan ndo unamaanisha ni miziki ya kisasa.

Amini time inakuja amapiano nayo itaondoka kama ilivyopotea kwaito ila michano itabaki sabab ndio root ya miziki yote bongo. Hiyo miziki Yako yenyewe haipendezi bila verse ya hip hop. We utatuambia nini
 
Miziki yenye akili,ujumbe haitakiwi siku hizi
Sahv we imba upuZ,sifia ushoga na ujingjinga mwingine mziki wako
Utaenda

Ova
 
Ngoja tubishane.
Unamaanisha nini kusema ni miziki iliyopitwa na wakati, ni wakati gani unao uongelea? Hip hop kitambo ilishindanishwa na dansi, zouk, taarab, kwaito, bhangra, takeu, mduara. Hizo miziki zooote zimepotea ila hip hop Bado ipo. Na huwezi kusema imepitwa wakati wewe binafsi leo hii bado unaishindanisha na afro pop ama amapiano ambazo nadhan ndo unamaanisha ni miziki ya kisasa.
Amini time inakuja amapiano nayo itaondoka kama ilivyopotea kwaito ila michano itabaki sabab ndio root ya miziki yote bongo. Hiyo miziki Yako yenyewe haipendezi bila verse ya hip hop. We utatuambia nini
Hiphop itakuwepo tu
Acha hao wanaoimba usngusng
Waendelee tu ila hiphop itakuwrpo
Tu

Ova
 
DAZi...! Chakufanyika ni media zikumbuke kuajiti wadau wa Hip Hop pia.
 
hip hop ipo real haiongopi ndomana wanaarakati wengi waukweli walikuwaa wasanii wa hiphop mfano 2pac angalia bongo wasanii waliopata ubunge walikuwa wanaimba mziki gani,ni vile saizi dunia haitaki vijana waendeleze harakati ya ukombozi wanaipa airtime miziki yakipumbavu na matusi izidi kuwavuluga vijana wasifatilie mambo ya msingi
ila kwa vijana wanaojielewe wanapenda hip hop yenyewe ile kama ya kina Sugu na Profesa jay
 
tatizo ni kwamba rap/hip hop haijakaa kibiashara, ipo kiharakati zaidi, mimi kama mdau na muwekezaji wa muziki, binafsi siwezi kuwekeza kwenye huo muziki kabisa. wewe angalia kati ya anaeIMBA na anaeRAP yupi mwenye uchumi na maisha mazuri?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom