Vyombo vya habari nchini Marekani, vinaripoti kuwa mgombea wa urais wa chama cha Democratic, Hillary Clinton ameshinda uteuzi wa chama hicho katika eneo la Puerto Rico.
Ushindi huo unaimarisha matumaini yake ya kunyakua uteuzi wa chama hicho, katika uchaguzi mkuu unaopangiwa kufanyika mwezi wa Novemba mwaka huu.
Matokeo ya awali yanaashiria kuwa Bi Clinton atashinda kwa asilimia 60% ya kura ikilinganisha na asilimia 35% za mpinzani wake Bernie Sanders.
Bi Clinton sasa anahitaji chini ya wajumbe 30 tu ili kushinda uteuzi wa chama hicho.
Ushindi huo ni afueni kubwa kwa Bi Clinton huku wakipiga kura katika majimbo ya New Jersey na California wakiajianda kupiga kura siku ya Jumanne.