Hili la walimu kuchangishwa michango ya Mbio za Mwenge kwa lazima likomeshwe

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
520
2,929
Mkurugenzi wa Halmshauri ya Ifakara ameandikia Barua Walimu wa shule kutaka walipe mchango wa kufanikisha shughuli za Mwenge. TAMISEMI mmeagiza Halmshauri kufanya hivi? Huo Mwenge hauna bajeti? Mbona hamna huruma na walimu nchi hii? Barua hii ibatilishwe, fedha zirudishwe kwa walimu.

Na hii sio tuu ifakara, Gairo huko DMO anawalazimisha watumishi wa Afya kutoa mchango wa Mwenge, Morogoro DC Mkurugenzi anawalazimisha walimu kutoa michango ya Mwenge na hii inaonekana ni maeneo mengi nchini na sio mwaka huu tu, kila mwaka wakati wa mbio za Mwenge walimu na watumishi wa Umma walio chini ya TAMISEMI wanachangishwa fedha.

Jambo hili la walimu na watumishi wa umma chini ya TAMISEMI kuchangishwa michango ya namna hii linapaswa likomeshwe. TAMISEMI wapo kimya, Waziri yupo kimya, huenda jambo hili wanalijua na wao ndiyo wameagiza.

Halmshauri kuagiza michango ya namna hii huku TAMISEMI ikiwa kimya, sisi tutajua TAMISEMI ndiyo wameagiza.

1. Tunataka kujua msimamo wa Serikali/TAMISEMI katika hili.

2. Kama TAMISEMI hawahusiki, tunataka tuone waraka wa kubatilisha michango ya namna hii kwa Halmshauri zote nchini.

Chama cha Walimu kipo kimya, kimekuwa butu!

Tangu kuondolewa kwa Katibu wa CWT, Deus Seif kutokana na mashtaka na shutuma zilizokuwa zinamkabili kabla ya kushinda Rufaa ya kesi yake, Chama cha Walimu kimekuwa na migogoro mikubwa sana hadi sasa. Kwa sasa ni kama kime-paralyze na hakiwezi kufanya jambo lolote kutetea maslahi ya walimu.

Migogoro ni mikubwa sana ndiyo maana Rais Samia aliona ni busara kutatua migogoro hiyo kwa viongozi wote wa sasa kuwapa U-DC kuanzia Rais wa CWT Leah Ulaya aliyeteuliwa kuwa DC wa Mbogwe, kaimu Katibu wa CWT Japhet Maganga aliyeteuliwa kuwa DC Kyerwa, Makamu wa Rais wa CWT Dinah Mathamani aliyeteuliwa kuwa DC wa Uvinza na Cornel Maghembe.

Waliokubali uteuzi wa Rais tena baada ya kujifiiria sana ni Makamu wa Rais CWT Ndug. Dinah Mathamani na Cornel Maghembe, ila Rais wa CWT Leah Ulaya na Kaimu Katibu wake Ndug. Japhet Maganga waligomea uteuzi wa Rais wakaandika barua kwa Rais kumshukuru kwa uteuzi na wakisema wametosheka na nafasi zao.

Unaweza kuwaza kipi ambacho wanakipata huko CWT wakati hawafanyi kazi zozote ingawa sasa wana kesi ya kimaadili inaendelea.

Na hawa viongozi ndiyo waliomponza RC Omary Mgumba wa Tanga, mlikuwa mnajiuliza kwanini aliondolewa wengi wakisema ni issue ya yeye kukemea madaktari wakati wa ajali ila kuna sababu nyingine, baada ya uteuzi wa Rais kwa viongozi hao wa CWT.

Viongozi hao walienda kufanya kikao Tanga, wakamualika RC Mgumba, RC akatamka wachape kazi hata kama Rais amewateua wao bado ni viongozi wa CWT hii nayo ilikuwa sababu ya utenguzi wa RC Mgumba.

Leo hii Rais Leah Ulaya na Katibu wake wanataka kuwaondoa watendaji wote wa CWT Makao Makuu sababu eti ni watu wa Katibu aliyepita Deus Seif, hivyo wanataka waweke watu wao.

Kesi nyingi za walimu Mahakamani zilizo chini ya CWT haziendelei sababu wanasheria hawalipwi. Walimu wana changamoto lukuki CWT ipo kimya, viongozi wa CWT wananufaika kwa michango ya walimu ikiwa hawafanyi kazi ya kuwasemea na kuwatetea walimu.

Walimu nyie ndiyo mlitufundisha hadi sisi tumefika hapa tulipo. Sasa kwanini mnakubali kuongozwa na watu wa CWT wasio na uwezo? Kwanini mnakubali kudhulumiwa? Kwanini mnakubali kuchangishwa michango ya namna hii, kwanini mnakubali kuonewa namna hii?

952990877.jpg
 
Umenena kweli bwana Nondo. Ila tatizo kubwa liko kwa walimu wenyewe. Nadhani tangazo linajieleza kuwa siyo lazima ni hiari.

Walimu wetu wanapenda kujipendekeza sana ili wateuliwe ukuu au umeki.

Kama wangeungana pamoja kukataa huu uhuni nadhani tungekuwa mbali sana.

CWT si mtetezi wao tena. Ni mnyonyaji wao.

Hebu ona Katibu wa CWT wilaya mojawapo ya jiji la Mwanza bwana Onesmo Makota ni mwenyekiti wa CCM wilaya ya Maswa. Je ataweza kuishurutisha serikali ya CCM?
 
Acha kubweka wewe mpumbavu unajua nguvu aliyokuwa nayo mkuu wa idara, Das na DED WEWE ? unajua weakness iliyopo kwenye idara ya elimu wewe unaongea ypumbavu ukiwa einza.??? Hujui lolote kuhusu halmashauri mpumbavu wewe
Mbona kama umepaniki ghafla! Hao unao wasifia, wana nguvu gani ya ajabu kwa mtumishi wa umma?

Kwani ikitokea mtu amekataa kutoa huo mchango, watamfanya nini? Watamfukuza kazi kutokana na hiyo sababu ya kipuuzi?

Unaufahamu mchakato mzima wa kumfukuza kazi mtumishi wa umma? Unafikiri ni mwepesi kiasi hicho? Mnapenda sana kutishia watu nyau.

Narudia tena; mtumishi wa umma atakaye changia huo mchango kwa lazima, atakuwa hana akili kichwani. Labda achangie kwa hiyari yake mwenyewe.
 
Acha kubweka wewe mpumbavu unajua nguvu aliyokuwa nayo mkuu wa idara, Das na DED WEWE ? unajua weakness iliyopo kwenye idara ya elimu wewe unaongea ypumbavu ukiwa einza.??? Hujui lolote kuhusu halmashauri mpumbavu wewe
Ngoja mnyolewe Sasa,hao unaposema Wana Nguvu hawana chochote Cha maana ,kujufuta kazi hawezi sana sana atakuhamisha au kukishusha cheo.
 
Mbona kama umepaniki ghafla! Hao unao wasifia, wana nguvu gani ya ajabu kwa mtumishi wa umma?

Kwani ikitokea mtu amekataa kutoa huo mchango, watamfanya nini? Watamfukuza kazi kutokana na hiyo sababu ya kipuuzi...
Tate mkuu,

Nilifanya hayo yote nikiwa huko Halmshauri my 10 yrs nikiwa mtumishi nayajua na nimeptia mengi mkuu.

Tusikutane jf watu wajifanye hapa kama ni new mesia nw huyu hajawahi kuyapitia
 
Back
Top Bottom