Hili la kuwaambia watu wazima wanatembea kama kobe mbona hamlisemi?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,710
149,954
Kuna mtu jana nilimsikia akiwaambia watumishi waliokuwa wanatakiwa kumkabidhi mh. fulani barua yake mele mjengoni wafanye haraka na waacha kutembea kama kobe!

Sasa mtu alietoa kauli kama hii na yeye akipewa za uso kuna dhambi gani?

Mnaohoji yeye kutukanwa mbona hili hamlisemi/hamlihoji?

Tuache unafiki maana haya ndio maisha tuliyoyachagua katika ule mjengo na hatuna budi kuyaishi unless wote wajirekebishe kuanzia viongozi wao na wanaowaongoza.

Tuache kujipendekeza huku tukijitia upofu na tutambue kila mtu anastahili heshima bila kujali cheo au nafasi yake katika jamii.

Jiheshimu utaheshimiwa na kamwe si vinginevyo.
 
Hakuna mtu mwenye vimaneno vya shombo na kuudhi kama mh.ndugai...utasikia haya kikalishe, mara mpuuzi..kwa matendo aliyoyafanya ataachaje kuwa fala
 
Hili nalo kwako ni ajabu.Huko nyumbani kwako mbona haya maneno ya kawaida sana.Kutembea kama Kobe maana yake si polepole?.Jambo la kawaida mbona unataka kuligeuza kuwa la ajabu!.Maneno mwembamba kama sindano,anaongea kama chiriku,hujawahi kuyasikia?.
 
Kuna alisema bungeni wanajua kulala na kuchekesha tu.

Huyu spika alimuita yule mtu. Jana ndio kadhihirisha bungeni kuwa kuna shida kubwa sana.

Wakiguswa na watu wa nje wabunge wote wanaungana kujitetea
 
Hakuna mtu mwenye vimaneno vya shombo na kuudhi kama mh.ndugai...utasikia haya kikalishe, mara mpuuzi..kwa matendo aliyoyafanya ataachaje kuwa fala

Kwanza kuitwa fala kuna heshima fulani ndani yake. Ningekuwa mimi nimechokozwa, walahi ningemwita mkuu-******.
 
Hili nalo kwako ni ajabu.Huko nyumbani kwako mbona haya maneno ya kawaida sana.Kutembea kama Kobe maana yake si polepole?.Jambo la kawaida mbona unataka kuligeuza kuwa la ajabu!.Maneno mwembamba kama sindano,anaongea kama chiriku,hujawahi kuyasikia?.
Hata neno "fala" kwa mujibu wa kamusi maana yake ni 1.mjinga 2.mzembe
 
Hii kauli imenichekesha sana, imagine mwendo Wa Kobe
 
Ningeliandika lakini nimekumbuka ile bakora kura za maoni ccm.hivi jamaa alipona ?
 
Wewe fafa kwa kukua kwako kote leo ndio umesikia kwa mara ya kwanza matumizi ya tamathali za semi kama "alitembea kama kinyonga au unatembea kama kobe". Toka lini maneno hayo yakawa tusi? Angesema wewe kobe mbona hufiki hapo ningekuelewa.
 
Hili nalo kwako ni ajabu.Huko nyumbani kwako mbona haya maneno ya kawaida sana.Kutembea kama Kobe maana yake si polepole?.Jambo la kawaida mbona unataka kuligeuza kuwa la ajabu!.Maneno mwembamba kama sindano,anaongea kama chiriku,hujawahi kuyasikia?.
Nakwambia aliyemfundisha huyu kiumbe lugha ya kiswahili anajilaumu. Kwa umri huo na usomi anaounadi kuwa nao kiasi cha kumsakama Makonda anashindwa kujua haya matumizi ya tamathali za semi tashibiha kama hii, maana yake nini pindi inapotumika,inatia shaka usomi wake. Kwa hiyo mpumbavu huyo akiwa katika kaunta ya polisi hapo anafungua kesi ya kutumia lugha ya matusi. Hii jitu ni la kudharau na kutia shaka uwezowake wa kufikiri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…