Hili jibu la TABOA hakika nimelipenda sana kwani hata na 'Mwenyewe Mwenyewe 2025 Tena' nae anachukua kweli kweli Rushwa bila ya Huruma

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
59,949
119,214
Katibu Mkuu wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (Taboa), Priscus John amedai rushwa barabarani kwa wakaguzi wote wa magari ni ya kiwango cha kutisha.

Amesema wanaopokea wanaonekana kuwa ni Jeshi la Polisi pekee kwa sababu wanavaa nguo nyeupe lakini ipo kwa wakaguzi wote.
John amesema hayo leo Jumatano Agosti 7, 2024 alipochangia mada kwenye mjadala wa Mwananchi X Space (zamani twitter) ulioandaliwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) ukiwa na mada inayohoji, ‘Vitendo vya rushwa kati ya madereva na askari wa usalama barabarani, nini chanzo na nini kifanyike kuvidhibiti?’
Uwepo wa rushwa kati ya madereva na askari barabarani, amesema unachochewa na tabia, mazingira na wamiliki wa mabasi na madereva kutofuata sheria, mazingira ya kazi kuwa magumu na watu kutoridhika na mishahara yao.
“Jambo la kufanyika ni rushwa kupigwa marufuku kuanzia shule za msingi, hata watu wazima sasa nao wapewe elimu ya rushwa namna inavyorudisha nyuma maendeleo kwa sababu unampa mtu haki isiyo yake, unamnyima mwenye haki. Rushwa Tanzania ni changamoto, hakuna sehemu ambayo haichukuliwi,” amesema.
John amesema barabarani yapo mageti mengi na magari yanakaguliwa na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (Latra), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).

Ameshauri matumizi ya teknolojia katika ukaguzi wa magari akisema yatasaidia kubaini upungufu uliopo.
John amewataka wamiliki wa mabasi kutoingiza magari mabovu barabarani kuepuka mazingira ya rushwa.

“Tunatakiwa wamiliki na madereva kujitambua, hizi hela ndogondogo na biashara ilivyo ngumu tunaacha hela nyingi barabarani,” amesema John.

Pia, ameshauri mazingira ya kazi ya Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani yaboreshwe ili kupunguza vitendo vya rushwa.

Chanzo: mwananchi_official

Anayechukua mno Rushwa tena za Kukufuru kabisa na hata hana Huruma nanyi hamumsemi ila TABOA mnawasema.
 
Back
Top Bottom