Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 1,190
- 2,893
Jeshi la Polisi Tanzania limemuita Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika kufika katika Ofisi ya Upelelezi wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni kwa ajili ya mahojiano kuhusiana na mauaji ya Ally Mohamed Kibao.
Kulingana na barua rasmi iliyotolewa tarehe 16 Septemba 2024, na Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Kinondoni wito huo umetolewa kwa lengo la kusaidia uchunguzi wa mauaji hayo.
Barua hiyo yenye kichwa cha habari "Wito wa Kufika Polisi," iliyosainiwa na Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Kinondoni, SSP Davis J. Msangi, inamtaka Mnyika kufika katika ofisi hiyo tarehe 18 Septemba 2024 saa nne asubuhi bila kukosa.
"Ofisi hii inafanya upelelezi kuhusiana na jalada tajwa hapo juu. Ili kukamilisha uchunguzi, nimelazimika kukuita kwa ajili ya mahojiano kwani kuna masuala ambayo wewe unayafahamu yanayoweza kusaidia katika upelelezi wa shauri hili," inaeleza barua hiyo.
Soma pia: Mnyika: Mzee Kibao alitekwa na Kuuawa akiwa ametoka kuendesha Mafunzo ya Maandalizi ya Uchaguzi Serikali za Mitaa. Tutaendeleza Majukumu aliyoyaacha!
Wito huo unatokana na hatua ya uchunguzi unaofanywa kuhusu kifo cha Kibao, ambaye alikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, ambaye alitekwa kisha kuuawa Septemba 2024. Tukio hilo limekuwa gumzo nchini, likiwakera wanasiasa, wanaharakati, na wananchi kwa ujumla.
Mnyika ameitwa chini ya kifungu cha 10(2) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, sura ya 20 na kifungu cha 32 cha Sheria ya Jeshi la Polisi na Polisi Wasaidizi, sura ya 322.
Soma zaidi:
==> Rais Samia: Nia yako njema ya uchunguzi mauaji ya kibao lakini ninashauri iundwe tume huru kuchunguza na sio Polisi
==> Familia yaomba uchunguzi wa haraka Kifo cha Ali Kibao, Waziri Masauni akabidhi Tsh. 5m ya Rambirambi
==> Freeman Mbowe: Iundwe Tume ya kijaji kuchunguza kifo cha Ali Kibao, Polisi hawawezi kujichunguza