Hiki hapa unachohitaji kufahamu kuanzia Tecno phantom A+ mpaka phantom 6

TECNO Tanzania

Senior Member
Jul 6, 2016
192
216
Kutoka kwa lemutuz blog HIKI HAPA UNACHOHITAJI KUFAHAMU KUANZIA TECNO PHANTOM A+ MPAKA PHANTOM 6 ~ Blogu ya Wananchi

Tangu uzinduzi wa toleo la kwanza kabisa la TECNO Phantom, toleo hilo limepata mafanikio na umaarufu mkubwa, sababu kuu ikiwa ni sifa zake zinazoifanya iwe na ubora wa kipekee na kuwapa watumiaji wake uzoefu.

Tecno Soon to be released.jpg


Toleo la sita la Phantom hivi sasa liko katika maandalizi, na tunasubiri kwa hamu tukijaribu kuangalia tofauti ya matoleo mengine ya zamani huku tukifananisha matoleo hayo na matoleo mapya ya hivi karibuni. Ni Dhahiri kuwa TECNO imeanza mbali na sasa tunasubiri kuona nini wanatuletea safari hii. Bila kusubiri, tuangalie kuanzia toleo lake la kwanza kabisa hadi sasa ikiwa ni moja ya smartphone ya Android inayosifika.



TECNO Phantom A+ (F7)

Phantom A+.jpg



TECNO ya kwanza kabisa ilitangazwa mwaka 2013 na ilitambulika wazi kuwa TECNO ndio inayoongoza kwa mauzo.

Kwa sifa zake, Phantom A Plus imewezeshwa na Android 4.2 (Jelly Bean), CPU ya GB 1.0 yenye RAM aina ya Quad-core iliyo na 1.2GHz. Vile vile simu hii imekuja na skrini kubwa na nyembamba inayoipa mwonekano wa kipekee.

Phantom A plus haikuwa simu iliyo kamilika kwa vyovyote vile, mara nyingi ilikuwa na mushkeri fulani na kugomagoma kwingi. Licha ya hivyo, imekuwa ni moja ya simu mashuhuri zaidi katika historia TECNO na bila shaka ni miongoni mwa simu bora za mwaka 2013.

Tecno Phantom A2 (F8)

Phantom A2.jpg



Katika toleo la pili la mlolongo wa matoleo mengine ya TECNO, Phantom A2 (F8) ilipata wakati mgumu kuendeleza umaarufu wa Phantom A+. Phantom A2 ilikuwa moja ya simu zilizo na kasi ulimwenguni kwa wakati huo.

Ilikuja na uwezo mkubwa na uliboreshwa kwa upande mzima wa skrini ukilinganisha na matoleo mengine yaliyopita.


TECNO PHANTOM A3

Phantom A3.jpg.png


Kama Phantom A2 ilikuwa na wakati mgumu katika soko, ni sawa tukisema kwamba TECNO Phantom A3 ilikuwa na wakati mgumu. Matarajio ya wengi kwa toleo hilo la tatu yalikuwa juu, wakitegemea kuwa itakuwa na uwezo mkubwa kuifanya simu hiyo miongoni mwa nyingine za Android kuwa bora. Kilichofanya simu hii kuwa kinara ni uwezo wake ikiwa na prosesa aina ya Quad-core iliyo na 1.5GHz, kamera ya mbele yenye MP 8.0 AF na nyuma yenye MP 13.0 ikiwa na sense ya BSI, HD IPS tachi skrini, pamoja na memori ya GB 16GB/GB1.


TECNO Phantom Z

Bongo5-Phantom Z.jpg.png


Hebu pata picha, ya TECNO Phantom A3 kwa dakika kadhaa; ingekuwa nyembamba ,yenye uwezo zaidi na bora kwa kila namna. Bila shaka hiyo ingekuwa ni TECNO Phantom Z. TECNO Phantom Z imekuwa gumzo kwa muonekano na uwezo wake mkubwa. Skrini yake ya ukubwa wa 1920×1080 imetengenezwa na teknolojia ya AMOLED. Phantom Z imeonyesha kuwa kamili ikiwa na betri yenye nguvu. Kwa mara nyingine, simu hii imeweza kuwaletea watuaji wake uzoefu wa kipekee.

TECNO Phantom 5

LeMutuz-Phantom 5.jpg


Kwa upande wa Phantom 5, TECNO ilikuja na dezaini ya hali ya juu. Simu hii ndio ya kwanza kwa TECNO kutengenezwa na chuma ikiwa na betri ya ndani kwa ndani yenye nguvu ya 3000mAh.

TECNO Phantom 5 imekuwa ni muendelezo wa milolongo mingine tangu ilipoachiwa. Sifa zake zimeifanya simu hiyo kupendwa na wengi. Na ufanyaji kazi wake umedhihirisha kuwa TECNO ikidhamiria kufanya kitu, kinatimia.

Sifa zake nyingine ni pamoja na teknolojia ya fingerprint, mfumo wa sauti na spika aina ya Dolby yenye nguvu ya aina yake.



TECNO Phantom 6 & 6+

Bongo5-Phantom 6 &6+.jpg




Picha za Phantom mpya iliyoachiwa.

Toleo jipya la Phantom bado liko jikoni likitarajiwa kuzinduliwa mnamo Septemba 2016. Lakini, na uvumi uliosambaa ni kwamba Phantom 6 itazinduliwa pamoja na toleo lake lingine la 6+, lenye tofauti kidogo.Kwa mujibu wa waandishi, simu hizo zitakuwa ndio bora zaidi kuzinduliwa mwaka huu. Kuna fununu kuwa zinakuja na sifa za kipekee na uwezo makubwa kama ilivyodhihirishwa na baadhi ya wataalamu wakiziiita “simu ya kimapinduzi”.

Ukweli ni kwamba nakubaliana nao kwa sababu ni simu chache sana miongoni mwa nyingine ambazo zinaweza zikatamba juu ya betri iliyo na nguvu zaidi ya 4000mAh pamojua na prosesa ya upana wa milimeta 6 -7. Simu hii inatabiriwa kuwa na kasi kushinda zote.

Tunaisubiri kwa hamu kuiona rasmi.
 
Back
Top Bottom