Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 40,319
- 72,742
Mbona kama vile nchi hii ina Ufa mkubwa sana wa kujali raia wake?
Yaani mwanajeshi mstaafu kapigana vita Uganda na kaponea chupuchupu mara kadhaa vitani, daktari aliyestaafu miaka ya 1990 na Mungu amempa maisha mpaka leo au Mwalimu aliyekuwa anatumika kwa moyo wote miaka hiyo bahati mbaya kwa serikali HAJAFA hadi leo anapokea kutoka HAZINA shs laki moja kama pension kila mwezi lakini eti wake wa viongozi nao wawe wanalipwa mamilioni 25% ya mishahara waliyokuwa wanalipwa waume zao?
Basi nchi hii ni tajiri sana! Lakini kwa nini haiwakumbuki basi hata hawa wazee waliolitumikia taifa kwa moyo mmoja enzi hizo.
Kumbukeni nazungumzia wastaafu walio staafu zamani 1998 kwenda nyuma kabla ya mifuko ya jamii haijaanza na wanalipwa na Hazina.
Kwanza sidhani kama wastaafu hawa wanazidi 5000 nchi nzima maana wengi wametangulia mbele ya haki waliobaki ni mateso tuu.
Mara ya mwisho kiwango hiki kupanda na kuwa laki moja ni miaka 10 iliyopita wakati wa JK. Waoneeni huruma acheni uchoyo.