Hizi ni propaganda tu, lakini Kiswahili kimezungumzwa Uganda tangu enzi za falme za Bunyoro na Buganda. Kusema Iddi Amini ndiyo amepeleka kiswahili Uganda iwe lugha ya kijeshi siyo sahihi. Buganda, Manyema, Mirambo, Kilwa, Mogadishu, Mombasa, Sofala, Yao na Zanzibar ziliunganishwa na The East African Long-Distance Trade, ambapo waswahili walitembea falme hadi falme kufanya biashara na kupelekea kiswahili kukua.
Lugha za Kibantu, ambazo sehemu kubwa zinafanana zilioana na lugha za Kiarabu na kiajemi kutengeneza lugha mpya ya kiswahili.
Mkoloni anafika akakuta kiswahili kinazungumzwa sehemu kubwa ya Afrika Mashariki, basi na kuanza kukitumia kama moja ya lugha muhimu za kiutawala. Ndiyo maana tunaposoma nadharia za kiswahili moja ya nadharia ni kwamba KISWAHILI NI KIBANTU, au KISWAHILI NI KIKONGO, au KISWAHILI NI KIARABU, au KISWAHILI NI PIJINI.
Waganda wengi wanakisikia na kukielewa vizuri kiswahili, sema tu huwa hawataki kukizungumza.