MPYA Hii video ni ya kweli? kwamba Idd Amin Nduli Dada alikipenda kiswahili hivi?

Taarifa hii ni mpya na bado inafanyiwa tathmini
Source #1
View Source #1
Wakuu wa JamiiCheck msaada tafadhali tupate uhalisia wa hii video kama imetengenezwa au ni ya kweli
Screenshot 2024-11-15 075441.png

Binafsi naamini! Nilipata kusoma mahali ni kwanini Uganda Kiswahili hakikuwahi kupokewa vizuri na kwa majibu wa maelezo yale Waganda walikuwa wanakichukulia kama Lugha ya Jeshini! Sasa hapo utaona wazi ni Wanajeshi wa Enzi za Amini ndo walikuwa wanatumia hicho Kiswahili
 
Hizi ni propaganda tu, lakini Kiswahili kimezungumzwa Uganda tangu enzi za falme za Bunyoro na Buganda. Kusema Iddi Amini ndiyo amepeleka kiswahili Uganda iwe lugha ya kijeshi siyo sahihi. Buganda, Manyema, Mirambo, Kilwa, Mogadishu, Mombasa, Sofala, Yao na Zanzibar ziliunganishwa na The East African Long-Distance Trade, ambapo waswahili walitembea falme hadi falme kufanya biashara na kupelekea kiswahili kukua.

Lugha za Kibantu, ambazo sehemu kubwa zinafanana zilioana na lugha za Kiarabu na kiajemi kutengeneza lugha mpya ya kiswahili.

Mkoloni anafika akakuta kiswahili kinazungumzwa sehemu kubwa ya Afrika Mashariki, basi na kuanza kukitumia kama moja ya lugha muhimu za kiutawala. Ndiyo maana tunaposoma nadharia za kiswahili moja ya nadharia ni kwamba KISWAHILI NI KIBANTU, au KISWAHILI NI KIKONGO, au KISWAHILI NI KIARABU, au KISWAHILI NI PIJINI.

Waganda wengi wanakisikia na kukielewa vizuri kiswahili, sema tu huwa hawataki kukizungumza.​
 
Samahani Mkuu, sijasema Amini ndie alipeleka. Nimesema Kiswahili kilikuwa kinachukuliwa kama lugha ya Wanajeshi. Na ingawaje ni kweli Kiswahili inawezekana kiliwepo tangu hizo enzi lakini ukweli hadi kesho matumizi ya Kiswahili Uganda ni madogo sana! Na kama kweli ni propaganda basi ni propaganda zilizoingia kwa mamilioni ya watu wakiwamo waganda wenyewe.Mathalani Gazeti la Monitor la uganda wanadai "Swahili language was once the neutral language of the army and other military services"! The Obersever la huko huko Uganda wameandika ni kweli individuals and some media wamekuwa wakiki-associate Kiswahili na Jeshi, na wakatoa mfano wa "Panda Gari” (board the vehicle), “Kitambuliso yako iko wapi?” (where is your identity card?), “Funguwa Mulango” (Open the door), and “towa pesa” (bring money) remain deeply ingrained in the memories of those who experienced those difficult times." The Observer walipomuhoji Prof wa Kabale University kuhusu hayo madai, gazeti hilo likaandika "Professor Ruth Gimbo Mukama of Kabale University’s department of African Languages Professor Ruth Gimbo Mukama of Kabale University’s department of African Languages acknowledges the validity in claims that the stigmatization of Kiswahili in Uganda is partly due to abuse by thugs and hooligans during the turbulent periods of the 1970s and 1980s." Lakini Prof akaongeza hoja nyingine ambayo kwa upande mmoja inafanana kwa 100% na hoja yako lakini anadai pia struggle for religious dorminance huku wakijua lugha ni nguzo muhimu, Christian missionaries wakawa wanakipa mgongo Kiswahili kwa sababu Kiswahili kiilingia Uganda kutokana na mwingiliano wa hayo madola ya kichifu uliyotaja na Waarabu pamoja na Wafuasi wa Mwamedi kutoka Pwani ya Afrika Mashariki!

Sasa chukua hiyo hoja ya Prof kuhusu Kiswahili na watu wa Alah, chukua Iddi Amini na kule kujinasibisha kwake na Uislamu, je unatarajia Dikteta na Fashisti Amin angependelea lugha ipi?
 
Sijasema Amini ndie alipeleka. Nimesema Kiswahili kilikuwa kinachukuliwa kama lugha ya Wanajeshi. Na ingawaje ni kweli Kiswahili inawezekana kiliwepo tangu hizo enzi lakini ukweli hadi kesho matumizi ya Kiswahili Uganda ni madogo sana! Na kama kweli ni propaganda basi ni propaganda zilizoingia kwa mamilioni ya watu wakiwamo waganda wenyewe.Mathalani Gazeti la Monitor la uganda wanadai "Swahili language was once the neutral language of the army and other military services"! The Obersever la huko huko Uganda wameandika ni kweli individuals and some media wamekuwa wakiki-associate Kiswahili na Jeshi, na wakatoa mfano wa "Panda Gari” (board the vehicle), “Kitambuliso yako iko wapi?” (where is your identity card?), “Funguwa Mulango” (Open the door), and “towa pesa” (bring money) remain deeply ingrained in the memories of those who experienced those difficult times." The Observer walipomuhoji Prof wa Kabale University kuhusu hayo madai, gazeti hilo likaandika "Professor Ruth Gimbo Mukama of Kabale University’s department of African Languages Professor Ruth Gimbo Mukama of Kabale University’s department of African Languages acknowledges the validity in claims that the stigmatization of Kiswahili in Uganda is partly due to abuse by thugs and hooligans during the turbulent periods of the 1970s and 1980s." Lakini Prof akaongeza hoja nyingine ambayo kwa upande mmoja inafanana kwa 100% na hoja yako lakini kwa upande mwingine struggle for religious dorminance huku ikiaminika lugha ni nguzo muhimu, Christian missionaries wakaanza kukipa mgongo Kiswahili kwa sababu kilikuwa kinahusishwa na Wafuasi wa Mwamedi!

Sasa chukua hiyo hoja ya Prof kuhusu Kiswahili na watu wa Alah, chukua Iddi Amini na kule kujinasibisha kwake na Uislamu, je unatarajia Dikteta na Fashisti Amin angependelea lugha ipi?
Madai ya waganda kusema Kiswahili ni lugha ya kijeshi ni hoja muifilisi na haina mashiko, sawa na zile hoja na madai mufilisi ya kulazimisha Uarabu/Kiarabu uwe Uislamu. Haya yote ni mazao ya ujingwa na mtu mweusi, kuchukia na kuvikana vitu vyake.

Uhalisia ni kwamba Kiswahili ni lugha pana yenye lahaja (Dialects) nyingi tu ambazo huenda zisifanane kabisa japo ni kiswahili. Tanzania tunatumia lahaja iitwayo KIUNGUJA (Standard Swahili) lakini wengine wanatumia KIMRINA, wengine KIAMU, wengine KIMTANG'ATWA na wengine KINGWANA. Nchi zote za Afrika Mashariki na Kati zina lahaja zao za kiswahili ambazo hata wao wanaweza kudhani ni lugha ya kabila fulani ila ukweli ni lahaja ya kiswahili.

Tatizo kubwa ni STIGMA, MALICE AND IGNORANCE, hasahasa zile ambazo kanisa KATOLIKI ilizisababisha sehemu nyingi za barani Afrika. Kwamba UISLAMU havitengwi na UARABU na USWAHILI. Hivyo kila kitu ambacho kinahusiana na USWAHILI au UARABU ni lazima tuvichukie na kuvikataa kwasababu ni UPAGANI na UISLAMU.​
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom