Hii tabia ya Wanaume kuwatelekeza watoto wao inanichefua sana na kunihuzunisha

Mmanu

JF-Expert Member
Feb 11, 2015
1,745
987
wanaJf mkoa salama?

Kuna tabia ambayo huwa inafanywa na baadhi ya wanaume ambao hawana huruma kabisa.

Unakuta dume zima na ndevu zake na ni pande la baba linazalia watoto sehemu halafu mwishowe linakuja kuwakana na kuwakimbia kabisa watoto.

Hii tabia sio poa sana kwani kulikuwa na ulazima gani umzalishe watoto huyo mdada halafu ukamtelekeza na kujisahaulisha kwamba damu yako ndiyo unaidharirisha.

Inauma sana na nachukizwa na hii tabia
 
Kuna mambo mengi sana kwenye dunia hii ikiwemo baadhi ya wanawake kujibebesha mimba ili aolewe, hili huwapoteza wanawake wengi sana. Unakuta mtu hajajipanga unapigwa mimba juu kwa kutegeshwa, hebu koma kutegesha mimba
 
Mwanaume hua hakimbii changamoto hua anapambana nayo ila kwa kesi hizi wadada wenye hua ndio husababisha kwa asilimia fulani haswa kutokua stable kwenye nyanja ya mahusiano
Ila tuna uwezo wa kupambana na hizo changamoto zote basi sioni sababu ya dume kuacha watoto wakiteseka ni vyema kupambana nayo tu
 
Sifa ya kwanza ya uanaume ni kukubaliana na majukumu na kila changamoto ya maisha.

Sifa ya pili ya uanaume ni kujua unachotaka, ikimaanisha kama umeamua kulala na mwanamke basi ujue pia unachokitaka katika kulalana huko.

Sasa ikiwa mtu anakimbia uzao wake huyo tayari keshapoteza sifa za kuwa mwanaume. Huyo ni mvulana tu. Uanaume sio umri bali ni matendo na tabia.
 
Swadaktaa mwanaume uliyetimiliwa huwezi kimbia damu yako bhana
 
wanaJf mkoa salama?

Kuna tabia ambayo huwa inafanywa na baadhi ya wanaume ambao hawana huruma kabisa.

Unakuta dume zima na ndevu zake na ni pande la baba linazalia watoto sehemu halafu mwishowe linakuja kuwakana na kuwakimbia kabisa watoto.

Hii tabia sio poa sana kwani kulikuwa na ulazima gani umzalie watoto huyo mdada halafu ukamtelekeza na kujisahaulisha kwamba damu yako ndiyo unaidharirisha.

Inauma sana na nachukizwa na hii tabia
Pole sana Dada naona Machungu ya Kuzalishwa Mfululizo na Kukimbiwa kutokana na Gubu lako lililotukuka umeamua kuja Kumalizia hapa JamiiForums.
 
wanaJf mkoa salama?

Kuna tabia ambayo huwa inafanywa na baadhi ya wanaume ambao hawana huruma kabisa.

Unakuta dume zima na ndevu zake na ni pande la baba linazalia watoto sehemu halafu mwishowe linakuja kuwakana na kuwakimbia kabisa watoto.

Hii tabia sio poa sana kwani kulikuwa na ulazima gani umzalie watoto huyo mdada halafu ukamtelekeza na kujisahaulisha kwamba damu yako ndiyo unaidharirisha.

Inauma sana na nachukizwa na hii tabia
Faika ya mwanamke ni ule utamu aliupata haku lazimishwa kuzaa au kubena mimba, ukibeba ni mzigo wako pambana nao
 
Back
Top Bottom