Hii siyo Tanzania tunayoihitaji

tufahamishane

Member
Jun 22, 2024
28
30
Ndugu zangu wa Tanzania tumuombe Mungu aturejeshee Tanzania Yetu tuliyokuwa Mayo
1: Tanzania itakayothamini na kuheshimu utu wa watu wote
2: Tanzania itakayothamini na kuheshimu uhai wa watu
3: Tanzania isiyowazuia watu kuongea na kujadili Hali ya nchi Yao bila hofu ya watu kutekwa
4: Tanzania aliyotuachia mwalimu nyerere

Tunaitaka Tanzania inayoitambua Tanganyika na Zanzibar.

Mungu ibariki Tanzania Yenye Uhuru wa kuongea na kutambua thamani ya uhai
 
CCM ndio adui namba moja wa Mtanzania.
CCM ya sasa imebakia tu na jina la CCM, lakini ukweli hiki ni chama tofauti chenye misingi na imani tofauti na iliyokuwa CCM. CCM ya sasa inaamini kwenye siasa za kuua watu.

Ukimsikikiza Tulia utajua hii ni CCM ya hovyo na hatari namna gani kwa usalama wa nchi na wananchi!! Tulia anawaambia UVCCM, eti mtu akimsema vibaya yeye Tulia, UVCCM "waruke naye". Hii "kuruka naye", ni kila kijana wa UVCCM atakavyoitafsiri, kama ni kuteka ni sawa, kama ni kujeruhi ni sawa, kama ni kuua ni sawa. Yaani Tulia hata afanye upuuzi wa namna gani, anataka watu wasimseme vibaya!! Halafu kuna wajinga bado wanamwona Tulia ni leadership material!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom