Sema " Rais Mstaafu. "
Walisema hawataingia kwenye uchaguzi mkuu kwa Katiba hii na wakaenda mbali zaidi kudai kuwa Rais Kikwete ni mnafiki.
Ni nani hapa mnafiki?
Ambaye hakuyasimamia maneno yake au aliyewafanya wasisimamie maneno yao?
Ndio siasa!Hapa Mbowe anamuita Rais Kikwete Kigeugeu na Mnafiki nae Kikwete kwa Uvumilivu wake wala hakumnya'anya Jengo la Bilicanas wala hakumlazimisha aanze kulipa Malimbikizo ya kodi ya Pango NHC.
Hapa Mbowe anaahidi hawataingia kwenye UchaguZi wa 2015 bila ya Katiba Mpya wala Tume huru ya Uchaguzi.
Sijui sasa nae Mbowe anaweza kujiita Kigeugeu na Mnafiki kwa kutotekeleza ahadi aliyotoa wa Mwenyewe bila ya kulaZimishwa Kama alivyomtukana Mh. Jakaya Kikwete?