Hii ni too much au ni ushamba wangu?

Udochi

JF-Expert Member
Jul 25, 2015
782
1,056
Hapa maeneo napofanyia kazi Kuna mfanyakazi mwenzetu anaoa,Sasa baada ya kikao,
kamati ya ndoa imeadhimia Kuwa,Kila mfanyakazi atoe laki 1.

Sasa miye kwa kuwa nishazoea kadi za ndoa za mtaani za elfu 20 hadi 30,Hii imenishtua kimtindo.

Nikiufikiria mshahara wangu wa ngama, kutoa laki 1 kwa Ajili ya ndoa ndoa nd'o nachoka sana.
____
Hebu nipeni experiences zenu wakuu,
Huwa mnakabiliana Vipi na mambo kama Hizi zinapojiri Kwenye Sehemu za kazi ikiwa kuna majukum kibao, kama vile kusapoti Wazazi na ndugu Wengine,
Yote yanayotegemea hela hiyo??

Na ni madhara yapi kutochangia?

Nawasilisha.
 
Inategemea je upo mkoa gani maana kuna mikoa mingine ina asili hiyo

Sent from my SM-E700H using JamiiForums mobile app
 
ndugu yangu jiangalie maisha yako yakoje usipende kuwapa faida wengine wakati wewe mwenyewe ujafanya mambo yako
nakushauri jpange wewe na jiulize moyoni mwako je utoe au usitoe
 
ndugu yangu jiangalie maisha yako yakoje usipende kuwapa faida wengine wakati wewe mwenyewe ujafanya mambo yako
nakushauri jpange wewe na jiulize moyoni mwako je utoe au usitoe
Kiukweli kwa maisha Yangu yalivyo hiyo hela ni nyingi,
Na
Nikitoa itabidi nipangue taratibu zangu zingine zinazohitaji pesa.
 
Mchango wa arusi unapaswa kuwa hiari ya mtu. Sasa hii ya kulazimisha nadhani wanavuka mipaka.

Fanya unavyoona inafaa, lakini kwa vyovyote mchango uwe ndani ya uwezo wako.
 
Siku hizi nikipata kadi ya mchango inaenda moja kwa moja kwenye dustbin. Nilaumiwe tu jamani but i am soleeee
Ila hapa ni kazini mkuu,
Ingekuwa mtaani INGEKUWA rahisi kuescape mkuu.
 
mama wee, kumbe sisi tulilizwa? sie mchango kwa kila mwanakamati ilikuwa 1m.
 
mkuu saidia ndugu zako.
Haina maana kufurahisha watu kwa starehe
na wakati kuna watu wanakuangalia, kukutegemea na kuhitaji
msaada wako.

Mimi sitoagi hata centi moja kwenye maharusu.
ila kila mwezi natoa fedha world vision.

Naamini kama mmeamua kuoana ni jukumu lenu ku save
fedha zenu za harusi. Acheni kutegemea mifuko ya watu .
 
Ila hapa ni kazini mkuu,
Ingekuwa mtaani INGEKUWA rahisi kuescape mkuu.
Hapo una changamoto. Kwa kweli ingekuwa mimi nafumba macho tu. kama sina nikaibe? Mungu anajua...na si dhambi nisipochanga. Maneno ya watu sasa loh
 
Kama huna usitoe... Ila kwenye sherehe kuwa shapu wa kusaidia kazi za hapa na pale...
 
Siku hizi imekua lazima, na hizi mambo ya tigo pesa unajikuta huna pa kukwepea, maana wanakaba balaa. ila mi dilisha acha kutoa michango ya harusi, baada ya kutuma pesa kwa m pesa alafu mlengwa akasema mbona hujaweka pesa ya kutolea aisee!
 
Toa kwa kadiri ya uwezo wako ila ukiwa kwenye kamati ni kawaida kupewa kiasi cha kutoa kwa kila mwanakamati unaweza waomba wasikuweke kwenye kamati uwe mchangiaji wa kawaida tu ambayo hata hiyo 20 huwa inakubalika....Life's too easy to be so damn complicated.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…