Linguistic
JF-Expert Member
- Mar 16, 2021
- 3,669
- 8,265
Kuna hii dhana ambayo inalazimishwa kuingizwa kwenye vichwa vya watu hasa mashabiki wa klabu ya Simba kutoka kwa viongozi wa Simba, ni dhana mfu.
Kusema Yanga SC huwa wanaikamia Klabu ya Simba kwenye Derby, kwamba ndiyo mafanikio yao makubwa kuifunga Simba. Huu ni uoga unaotumika kama mbinu ya kujitetea kuwalinda viongozi ili hata ikitokea wamepoteza mashabiki waamini kuwa si jambo la ajabu kwa sababu Yanga wanaikamia Simba.
Moja ya furaha ya klabu yoyote Duniani ni kushinda Derby, na hakuna klabu yoyote Duniani isiyopenda kushinda derby, hivi vingine ni mbinu ya kujitetea tu.
Msimu unapoanza lengo mama la klabu yoyote kubwa kwenye eneo husika ni kushinda makombe. Ili ushinde Kombe la Ligi Kuu, muhimu ni kuchukua alama kutoka kwa 'Title Contenders' wenzio ili kurahisisha mbio za kulisaka kombe.
Ni uongo kuwaambia watu kuwa Simba huwa haichezi kwa nguvu dhidi Yanga, kwamba malengo ya Simba ni kimataifa na sio ligi ya ndani, hata shetani ataona aibu. Ukifungwa kubali umefungwa na siyo kutafuta sababu mara uchawi, mara timu hii inakamia sana.
Hao jamaa wa njano na kijani wangekuwa wanakamia mechi moja pekee wasingekuwa na makombe 28 ya ligi, na wasingekuwa na 'Unbeaten' 42 za Ligi Kuu mpaka sasa.
Wakosoaji watahoji, mbona kimataifa Yanga hawafanyi vizuri kama hawakamii? Jibu rahisi tu, kufanikiwa kwenye michuano ya kimataifa kuna mchanganyiko wa vitu vingi, Bahati+Uzoefu+Ubora+Muda na jinsi mnavyoyaendea mashindano.
Na ndiyo maana Manchester city ni miongoni mwa vilabu bora Duniani kwa sasa, wametawala soka la England 🏴 miaka ya hivi karibuni lakini wanahangaika kwenye michuano ya UEFA. Wana kila kitu ila linapokuja suala la UEFA wanafeli. Hawa nao unaweza sema wanakamia timu za England pekee?
Mafanikio ya klabu ni makombe vingine ni maoni tu ya watu na siyo ukweli. Kama Makombe yanapatikana kwa kushinda mechi ikiwemo Derby, kwanini isiwe?