Hii ni kwa WASAFIRI NA DIASPORA TU: Lets Go, Wale mliofanikiwa kwenda nchi za Ulaya au America tuambieni ni njia zipi mlizitumia??? AGENTS??

Drax Draxlerr

Member
Sep 3, 2022
15
21
Habari
Kama Heading inavo sema, hii ni kwa watu wa safari tuu ikiwa wew huamin katika safar na upambanaji katika nchi za watu basi pita kushoto hii haikuhusu

Kwa wale wenzangu wenye ndoto za kusafir kwenda Poland, Australia, Ujeruman, Denmark, Scandinavia, UK, Canada, US na nchi nyingn zenye fursa kwa wapambanaji huu uzi apa kushare mawili matatu on how we can make our dreams true on 2025

Yafuatayo ni mambo ambayo napenda kujua kutoka kwa yoyote aliyefanikiwa kufika huko au yoyote ambae bado hajafanikiwa lakn anafuatilia hiz mambo na ana Ideas
1; Agents, je ni kweli hapa kwetu Tanzania kuna Agents wanaosaidia watu kusafir na kwenda kufanya kazi huko mbele?????? na je hao agents ni real Agents au weng wao ni matapel??? km wapo trusted agents wanao safirisha watu basi wataje hapa na tuambie ofis zao zipo wapi
2; Je ni scholarships zipi au za nchi zipi ni rahis zaid kwa watz kuzipata na kuzitumia kuingia katk nchi hizo kwa njia ya kusoma?
3; Ukiachana na Agents ni njia ipi nyingine ambayo kijana anaejitafuta anaweza kuitumia kufanikisha kusafir kwend nchi zilizo endelea na kupambana kwa ajili ya manufaa yake, ya familia na ya taifa kwa ujumla.

Sina Information nying lkn mara zote nmekuw nikiwaza nje ya Box na kufikiria ni jinsi gan ntaweza kuingia katk nchi za ulimwengu wa kwanza kwa lengo la kupambana na kujitafuta for myself, my family and my vountry in general so nawaomba wale ambao tayar mlifanikiwa mtupe Hints muhimu mlifanikishaje au mtu yoyt mweny Ideas bas tupe mchango wako pengn kupitia mchango wako kuna watu watafanikiwa in 2025 na watasaidia familia zao just thtrough your Informations

NOTE:; km safar za kutafuta maisha nje sio ndoto zako usicomment chochote plizz hii ni kwa ajili ya hustlers pekee

All in All wishing you all MERRY CHRISTMAS and HAPPY NEW YEAR
 
Ila haya maisha. Hata hivyo kujipendekeza kwangu kwa wazungu ilinisaidia kiaina lakini inakera na madharau. Nakumbuka kulikuwa na mavolunteers flani machalii tu kutoka Skendinevia. Yani yalikuwa majinga sana yalikuja yakaanzisha mashindano ya kuendeshaji baiskeli.Yani kwa kujipendekeza nilinyonga hasa maamaee nikashinda. Nikadhani labda tutazawadiwa hela ndefu tukaambulia kupewa vikadi flani hivi vinapicha ya teddy bears kama zawadi nilimaindi kichizi.

Chaliifrancisco

Nyau de adriz
 
Kwa teknolojia ilipofika wala huitaji Agent yeyote wa kukusaidia kufika Ughaibuni.

Agent wa kukusaidia kufika Ughaibuni ni YOU TUBE, GOOGLE, WEBSITE ZA EMBASSY Mbalimbali pamoja na Research.

Ila ukiwa mvivu hutaki kufanya research, unataka usaidiwe hadi ku Google vitu. Basi utakutana na Ma Agents watakao kupiga hela nyingi sana kwa kitu kidogo tu ambacho wewe mwenyewe unaweza kukifanya.
 
Tongoza ma volunteers ama watalii. Funga ndoa halafu unavushwa.

Chaliifrancisco

Nyau de adriz
Oya acha Bangi Mzee huu Uzi siriazi nipo hapa kusikiliza madini juzijuzi nimeenda uhamiaji tayari passport ipo kwenye begi nasubiri nimalize shule In Shaa Allaah niangalie wapi niibuke.

Nitaenda kulima msimu ukianza In Shaa Allaah nikatafute pesa ya nauli kwanza na mambo mengine.
 
Kwa teknolojia ilipofika wala huitaji Agent yeyote wa kukusaidia kufika Ughaibuni.

Agent wa kukusaidia kufika Ughaibuni ni YOU TUBE, GOOGLE, WEBSITE ZA EMBASSY Mbalimbali pamoja na Research.

Ila ukiwa mvivu hutaki kufanya research, unataka usaidiwe hadi ku Google vitu. Basi utakuta na Ma Agents watakao kupiga hela nyingi sana kwa kitu kidogo tu ambacho wewe mwenyewe unaweza kukifanya.
Kikubwa kingine zaidi ni pesa , mfano mimi nimeambiwa niwe na kama M4 na nusu hivi ndio nitaweza kufanya process zote mwanzo mwisho , nauli na vinginevyo mpaka kupewa mkataba wa kazi wenyewe.
 
1734961285857.png

 
Ila haya maisha. Hata hivyo kujipendekeza kwangu kwa wazungu ilinisaidia kiaina lakini inakera na madharau. Nakumbuka kulikuwa na mavolunteers flani machalii tu kutoka Skendinevia. Yani yalikuwa majinga sana yalikuja yakaanzisha mashindano ya kuendeshaji baiskeli.Yani kwa kujipendekeza nilinyonga hasa maamaee nikashinda. Nikadhani labda tutazawadiwa hela ndefu tukaambulia kupewa vikadi flani hivi vinapicha ya teddy bears kama zawadi nilimaindi kichizi.

Chaliifrancisco

Nyau de adriz
Unawakilisha mawazo ya vijana wengi wa kitanzania i.e. kudhani watu weupe wana fedha nyingi na huzitoa bure bure tu kwa watu weusi. Kwa wale ambao hawajafika nchi za Ulaya zenye watu weusi wachache ngoja niwape somo moja. Ombaomba wa kizungu wanalenga watu weusi kuliko weupe wenzao. Mnajua sababu? Kwa sababu wazungu hawana utamaduni wa kumpa mtu fedha bila sababu maalum au channels rasmi wakati watu weusi ni rahisi kutoa.
 
Back
Top Bottom