The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 1,547
- 3,186
✓Ni ajabu lakini ni kweli kuwa ndugu huyu ambaye amewahi kuwa RC maarufu sana enzi zile wa mkoa wenye watu wengi zaidi Tanzania yaani DSM analalamika kuwa anawindwa na kundi la watu ili wamuue..
✓Ndugu Makonda ukiwa RC - DSM, unatuhumiwa kuongoza kundi la UGAIDI WA KIDOLA (State Sponsored terrorism) la kuteka, kujeruhi, kuua na kupoteza wakosoaji wa sera za aliyekuwa Rais awamu ya 5 na chama chake - CCM hayati John P. Magufuli..
✓ Ukisoma posts zako huko Instagram utatambua kuwa ndg Makonda wewe bado ni mtu mwenye kiburi lakini wakati huohuo nafsi yako kwa ndani ukiwa na hofu na mashaka makubwa ya kukosa usalama yaani KIFO. Huoni kubwa na ulinzi tena uliokuwa unautegemea na unaowategemea wamekupa kisogo. Unaona giza nene mbele yako. Hulioni tumaini..!
✓Sisemi au kuandika haya ili kukuhukumu ndugu Makonda kwa kukuona ni mtu mwenye dhambi sana, mkosaji sana na huku mimi nikijihesabia haki ..... la hasha... Sina maana hiyo..!
✓Nataka kuonesha kuwa sisi ni binadamu. Wote tuna tabia moja ya kurithi tokana na ubinadamu wetu, yaani ya tabia ya kuzaliwa ya asili ya dhambi tuliyorithi kwa babu na bibi yetu Adamu na Hawa/Eva...
✓Hakuna mwenye haki hata mmoja unless tumekubali kupokea neema ya kufanywa wenye haki mbele ya Mungu kwa njia ya sadaka (tambiko/dhabihu) ya mwanae wa pekee yaani Yesu Kristo aliyemtoa afe, amwage damu msalabani miaka 2022 iliyopita ili iwe ondoleo la dhambi ya ulimwengu wote. Kumbuka dhambi ndiyo chanzo cha hofu na mashaka yetu. Dhambi ni lango la shetani la kuingilia ndani mwetu na kuleta uharibifu ikiwemo mauti yaani Kifo..
✓Kwa sababu hii, Makonda, wewe ni binadamu na unabeba tabia zote za kibinadamu za udhaifu wa kibinadamu kama ilivyo mimi na wewe. Unafanya makosa kama ambavyo kila mtu hufanya makosa. Na neema iliyo Ktk Yesu Kristo iko kwa ajili ya kila mtu apendaye na anyenyekeaye na aipokeaye..
✓Tofauti pekee tuliyonayo binadamu mmoja mmoja ni uwezo wa kuiona na kuikubali njia au neema ya wokovu iliyokwisha funuliwa kwa watu wote, yaani YESU KRISTO..
✓ Neema hii inamkalia mtu iwapo tu ataamua kuipokea kwa UNYENYEKEVU na UTII na MOYO WA SHUKRANI na kumwezesha kutii amri na maelekezo (guidelines) za Mungu zinazompa namna bora ya kuishi hapa duniani kupitia kwa Yesu Kristo Bwana na mwokozi wa watu wote, ukiwemo wewe na mimi..
✓ Nikukumbushe kubwa kuna time katika maisha, watu huwa tunakwama na kukosa msaada kabisa haijalishi tuna marafiki na utajiri wa vitu na fedha kiasi gani. Kwa wakati huo, haya yote huwa yanakuwa hayana msaada ili kuthibitisha kuwa furaha na amani na wokovu wa mtu haupo katika mali na utajiri..
✓Na Mungu huamua atuweke katika hali hiyo ngumu kimwili na kiroho (nafsi), ili yamkini tupate muda wa kumgeukia yeye na kumuona kuwa yeye ndiye pekee mwenye msaada wa kutuokoa kutoka katika mtanziko tuliomo wakati huo..
✓Ndugu yengu Makonda na wengine wenye tabia kama yako, mko Ktk hali hii. Mnahitaji msaada. Na kama mauti imefungwa kwa sasa, maana yake mna bonus ya muda wa kutengeneza mambo yenu. Maana yake mnayo neema ya Mungu, lakini tatizo lenu ni upofu wa fikra za ndani. hamuioni neema hiyo..
✓Watu wa namna hii wamejaa KIBURI cha uzima. Bado Wanawaangalia na kuwatazama wanadamu kama misaada wao. Kwamba wao ndiyo watawaokoa. Wamekosea. They are wrong. Hakuna mwanadamu hata mmoja awezaye kuondoa nguvu na hukumu ya dhambi isipokuwa mwana pekee wa Adamu - Yesu Kristo..!
✓Katika scenario hizi, naongea na Paul Christian Makonda. Namhurumia sana. Dunia na watu wote wanamhukumu. Naye anajaribu kupambana nayo kwa akili na nguvu zake mwenyewe. HAKIKA hawezi kushinda. Asipoigeuikia neema ya Mungu iliyofunuliwa kwake ktk Yesu Kristo, hakika yanayomtia hofu na mashaka, YATAMPATA SAWIA..!
✓Paul Makonda rafiki yangu, bado unakabiliwa tatizo la KIBURI. Yaani huoni kuwa wewe ni binadamu wa kawaida kabisa kama tulivyo sisi wengine na kwamba binadamu wote tunakosea na mara zote tunahitaji msaada..
✓Ndugu yangu Makonda kiuhalisia kwa sasa ulipaswa uwe umekufa. Lakini wewe Mungu anakupenda sana. Mungu bado anakupa NEEMA YA UHAI ili urekebishwe mambo yako..
✓Bahati mbaya ni kuwa umejaa KIBURI. Huonekani kutaka kujishusha na kunyenyekea kwa kukiri na kutubu makosa yako kwa Mungu muumba wako na kwa wote aliowakosea..
✓Paul Makonda uliishi maisha ya kumtegemea binadamu aliyezaliwa na mwanamke, anayekufa, kuzikwa na kisha kuoza ardhini badala ya Mungu aliye muumba na kumpa uhai. Ulianza kukosea hapo. Leo mwanadamu uliyemtegemea hayupo, kafa. Utafanyeje sasa?
✓Inasikitisha kuwa, kwa sababu ya kiburi chako, huoni kabisa kuwa upo msaada mbele yako. Bado unajaribu kujitetea kwa kujihesabia haki. Unajaribu kukwepa kuwajibika kwa makosa yako mwenyewe. Unajaribu kutwisha mzigo wa makosa yako watu wengine. Hiyo haiwezi kukusaidia. Tabia inakusindikiza kwenye mauti yako ya kimwili na kiroho. Fungua macho ya ndani ya ufahamu wako. Jiepushwe na hukumu ya Mungu iliyo mbele yako..
✓Msaada wako kwa sasa uko kwa Mungu Yehova pekee kupitia kwa Yesu Kristo, mwokozi wa ulimwengu huu na watu wote..
✓Kimbilia huko ndugu yangu Makonda. Nenda kakiri na kutubu makosa yako. Mungu atakusamehe kabisa na kukuondolea adhabu au hukumu ya dhambi zako iliyoko mbele yako..
✓ Ukifanya hivyo, nenda hatua moja mbele. Chukua ujasiri wa kuonana na wote uliowaumiza wakati ukiwa na madaraka ya kiserikali. Waambie NISAMEHENI niliwakosea. Ni ngumu lakini ndiyo njia ya kupona kwako. Huna njia nyingine..
✓Ukimaliza hatua hiyo, rudisha kila mali au vitu vya watu uliyochukua kwa nguvu Pasipo ridhaa yao wakati ule ulipokuwa na mamlaka na madaraka ya serikali..
✓ Kumbuka machozi ya uliowaumiza na kuwanyanyasa na kuwanyang'anya [kuwaibia kwa nguvu] vitu walivyovipata kwa kufanya kazi zao halali kwa sababu tu walikupinga au mlitofautiana nao yamemfikia Mungu na hayo ndiyo yanayozalisha ghadhabu ya Mungu na hasira za Mungu kuku - torment wewe..
✓Ukikubali ushauri wangu, hakika neema ya amani ya Bwana Yesu Kristo itakuwa juu yako. Utasamehewa makosa yako kabisa kama mimi nilivyosamehewa maana nilikuwa mbaya na mchafu kuliko wewe. Hakika kwa kuchukua uamuzi huu, utabaki na moja tu, kuuguza makovu ya matokeo ya dhambi za kihistoria. Ukikataa na kuendelea kubeba kiburi chako hakika Mungu anasema UTAKUFA kabisa..
Asante, NEEMA YA BWANA YESU KRISTO iwe pamoja nawe..