TAFAKARI :-
Kuna mwalimu aliyezoea kumchapa viboko mwanafunzi mmoja mchelewaji. Mwanafunzi huyu alikuwa akichelewa kipindi cha kwanza kila siku. Hivyo, siku ambazo mwalimu huyu alikuwa na kipindi cha kwanza, mwanafunzi huyu alikuwa anachapwa kwanza kabla ya kuingia darasani. Hali hii iliendelea kwa muda mrefu. Wiki moja ilipita bila yule mwanafunzi kuonekana shuleni.
Wiki lililofuata yule mwanafunzi alifika shuleni kabla ya mwanafunzi mwingine yeyote. Mwalimu yule alipomwona alifurahi sana. Alipoingia darasani alimwita na kumsifia sana mbele ya darasa.
"Simama. Darasa, Mpigieni makofi kwa sababu leo kawa wa kwanza kufika shuleni. Kumbe fimbo zile zimesaidia, enhe"
Wanafunzi walipiga makofi huku wengine wakimcheka. Akamwomba mwalimu ampe nafasi aseme jambo. Mwalimu akamruhusu
"Mwalimu, siku zote nilizokuwa nikichelewa kufika shule nilikuwa namuuguza mama yangu. Baba yangu alifariki kabla sijazaliwa. Nimelelewa na mama yangu tu. Simjui ndugu yeyote. Mama yangu alipokumbwa na maradhi alipelekwa hospitalini lakini maradhi yake hayakuonekana. Akaruhusiwa kurudi nyumbani akiwa na dawa za kutuliza maumivu tu." Kwa sababu hatukiwa na pesa, hakuweza kupelekwa popote kwa vipimo zaidi."
Akafuta machozi yaliyoanza kutiririka mashavuni. Mwalimu.
"Hivyo, nilitakiwa kufanya usafi wa nyumba, kuchota maji, kumsafisha mama yangu, kumwandalia chakula chake kabla ya kuonda kuja shuleni na kazi zingine zote." Akanyamaza kidogo."
"Lakini leo nimewahi kwa sababu mama yangu alifariki wiki lililopita. Kwa hiyo kilichokuwa kinanichelewesha kimeondoka ndo maana leo nimewahi."
Hakuweza kuongea tena. Taratibu akakaa kitini huku akilia kwa kwikwi
Darasa zima liligeuka mahala pa msiba.
WITO:
Msiharakishe kuadhibu bila kutoa nafasi ya kujieleza sababu baadhi ya wenye makosa hupenda wapate kujieleza ili upatikane ufumbuzi unaofaa wa tatizo.
UKIIPENDA SHARE TAFADHALI ILI WENGINE WAPATE UJUMBE HUU
BONYEZA LINKI HII
https://www.facebook.com/mtikiso ILI KUJIUNGA NA FACEBOOK PAGE YETU UWEZE KUSOMA SIMULIZI MBALI MBALI ZA MAISHA