Mcqueenen
JF-Expert Member
- Nov 2, 2019
- 6,843
- 11,701
True story: Tea time,
Nilizaliwa katika ukristo na kukulia kwenye ukristo.
Mwaka Jana nilihamia Tanga kikazi, mtaa niliokuwa Ninaishi ulikuwa una Waislam tupu. Nyumba nliyokuwa Ninaishi ilikuwa jirani na msikiti, Kila siku pale msikitini walikuwa wanaimba aya za Quran Usiku kucha. Sijui kwanini lakini Ile sauti ilikuwa ni nzuri sana masikioni na ilinifanya nikawa najisikia amani sana nilalapo.
Mwaka huu mwezi fulan nikiwa nimelala, nikaota ndoto ya ajabu iliyonifaonya nisilimu wiki hiyo. Ndoto yenyewe ilikuwa hivi:
Niliota Mimi na kaka yangu wa Arusha tukitembea maeneo ya mtaani kwetu hapo Tanga. Tukakutana na kundi kubwa la watu wa Kila aina matajiri kwa masikini wakiingia katika ule msikiti jirani.
Pamoja na tofauti zao za kiuchumi lakini wote waliingia ndani katika ule msikiti na kuwa kama kitu kimoja. Hakukuwa na madaraja mule ndani, hakukuwa na mabenchi ila wote waliingia kama watoto wadogo wakijisalimisha kwa Muumba wao. Ni kama vile pesa,vyeo,umaarufu waliviacha nje ya msikiti.
Nikapita jirani nikasikia ndani Quran inasomwa na wote wakistaajabu maajabu ya hiki kitabu kilichoandikwa Karne nyingi zilizopita.
Nikapita kwa pembeni nikielekea zangu nyumbani, ila kwa nje nkakutana na mtu akawa ananialika tuingie kuswali, nikakataa kwa visingizio vingi kama vile Nawahi sehemu,sijui kuswali,siku nyingine nk. Nk.
Lakini yule mtu akanisisitiza na kuniambia kuwa nikiingia Mungu atanitoa gizani na kuniweka kwenye njia ya haki.
Mi nkaondoka lakini nkamuacha kaka angu akiongea na yule mtu. Ndoto ikaishia hapo.
Kaka angu niliokuwa sijawasiliana naye takriban wiki 3 na sikumwambia kuhusu hiyo ndoto,lakini wiki hiyo hiyo nilisikia kuwa kaka angu wa Arusha amesilimu.
Kiukweli nilistaajabu sana na kujiuliza ni nini hiki na maana yake nini?
Baada ya Tafakuri ya mda mrefu niliamua kwenda kwenye huo msikiti labda nitakutana na yule mtu wa ndotoni na hiyo ndiyo ikawa njia iliyonipelekea kurudi kwenye uislam(Kila mtu huzaliwa muislam).
Katika kumtafuta yule mtu Kuna shehe nilimsimulia, akaamua kuchukua jukumu la kunifunza na kunielezea maajabu ya Quran na kiukweli Ile ndoto + maajabu ya Quran ilinifanya nikasilimu. Bado naendelea kujifunza mengi mapya katika hii Imani ya kweli na haki.
Allahu akbar.
PS: Yule mtu Bado sijampata
PS #2: Braza wa Arusha anajua namimi nimesilimu lakini sijamuhadithia kuhusu Ile ndoto.