Angeagiza Polisi.
Alafu ku-arrest ni sawa na kumtaka mtu afike Polisi?
Amepewa mamlaka ya kusababisha mtu awe arrested lakini sioni mamlaka ya kumtaka mtu afikie Polisi.
Kwa mujibu wa kifungu cha (2),lazima ajiridhishe kuwa anaetakiwa kukamatwa anaweza kusababisha uvunjifu wa sheria(kuvuruga amani) na kwamba akamatwe iwapo njia pekee ya kumzui mtu huyo kuvunja amani au kufanya kosa lingine ni kwa mtu huyo kuwekwa Mahabasu.
Sasa hata kama Makonda akiitwa Mahakamani na kutakiwa kuthibitisha mbele ya Mahakama kuwa Mbowe asingekamtwa angesababisha uvunjifu wa sheria, Makonda angethibitisha vipi hapo?