JituMirabaMinne
JF-Expert Member
- May 4, 2020
- 3,381
- 9,740
Gari ina sensor nyingi sana kama MAF sensor, MAP sensor, A/F sensor, IAT sensor, ECT sensor, TPS sensor, CPS, VSS n.k.
Lakini katika hizo sensor zote kuna sensor moja tu ambayo ndio sensor kuu (master sensor). Ukuu wake unatokana na sababu kwamba sensor hiyo hutumika katika operations nyingi sana kwenye engine na baadhi kwenye automatic gearbox.
Sensor hiyo ni Engine Coolant temperature sensor (ECT sensor). Kazi ya sensor hii ni kupeleka signal ya joto la coolant kwenye control Module(PCM). Kwanza kabisa hii ndio sensor ambayo inaamua engine ioperate vipi(Yaani operating strategy ya engine). Hebu tuone baadhi ya operations ambazo zinaamuliwa na signal kutoka kwenye hii sensor.
Huenda hizo points nmezipanga vibaya lakini ni muhimu ukazisoma zote.
1. Cold start fuel enrichment
Unapowasha gari asubuhi sensor hii hupeleka signal kwenye Control module kwamba coolant ni ya baridi hivyo control module huamuru kwamba mafuta yaingie mengi kwenye engine kwa kuongeza muda wa injector nozzle kuwa wazi (Pulse width). Kama sensor hii itaharibika na ikawa inatoa signal ya cold tu basi itapelekea engine kutumia mafuta mengi sana pia kama itaharibika na ikawa inapeleka signal ya hot tu basi itapelekea misi, kuzimazima au rough idle wakati wa kuwasha gari asubuhi au wakati engine imepoa.
2. Spark advance and retard
Hii spark advance maana yake spark inakuwa released degrees chache kabla piston haijafika juu ya cylinder( yaani Top dead centre). Inasaidia sana katika performance ya engine na mambo ya emission. Kama joto ambalo engine inatakiwa kuoperate halijafikiwa basi spark advance itakuwa limited kufanya kazi.
3. Exhaust gas recirculation (EGR)
Control module ya gari haitaruhusu EGR valve kuwa wazi mpaka engine ipate joto la kutosha. Na kama ikiwa wazi wakati engine ni ya baridi inaweza kupelekea gari kumisi, rough idle au hata kuzima. Na kama ikifungwa wakati imeshapata joto inaweza kuathiri performance ya engine.
4. Open/closed loop feedbackh control of A/F ratio
Control module ya gari(PCM) inaweza kuignore signal kutoka kwenye Oxygen sensor kwamba Air/fuel ratio ni rich/lean mpaka pale engine itakapofikia joto fulani. Unapowasha gari asubuhi au muda wowote ambapo engine ni ya baridi PCM itabakia kwenye open loop na itaamuru mafuta mengi yaende kwenye engine kwa ajili ya kuboresha idle speed quality na cold driverbility. Kama PCM itashindwa kuingia kwenye closed loop pale engine itakapokuwa ya moto basi itapelekea gari kutumia mafuta mengi na kuchafua mazingira.
5. Idle speed(Silencer wakati wa baridi)
Control module ya gari itaongeza RPM wakati umewasha gari engine ikiwa ya baridi ili kuifanya engine isizime na kuboresha idle speed quality.
6. Lock up mechanism ya torque converter kwenye Automatic gearbox
Hii lock up hutokea ikiwa speed ya engine na speed ya gearbox zinafanana au zimekaribiana, yaani maana ya lock up ni kunakuwa na direct drive kati ya engine na gearbox, hii kupelekea kutokuwepo kwa joto jingi linalozalishwa kwenye torque converter na hivyo kuifanya gearbox yako iishi maisha marefu. Sasa hii lock up haitatokea ikiwa joto la engine linalohitajika halijafikiwa. Kama sensor yako ni mbovu, au umeng'oa thermostat au umeunga direct fan basi operating temperature ya engine haitafikiwa na unapunguza maisha ya gearbox yako.
7. Radiator fan(Feni ya rejeta)
Hii ndio sensor inaamua kwamba sasa feni ya rejeta iwake au izime(ukiondoa gari za zamani sana ambazo hutumia temperature switch). Hivyo kama sensor hii ikiwa mbovu feni yako inaweza isiwake kabisa au ikawaka muda wote kutegemea na signal inayopeleka kwenye control module. Kama isipowaka kabisa engine itaoverheat na kama ikiwaka muda wote engine itaoperate chini ya joto lake.
Hizo ni baadhi tu ya operations za muhimu ambazo zinafanywa na sensor hii. Hivyo unaweza kuona ni jinsi gani sensor hii ilivokuwa ina umuhimu mkubwa katika gari yako.
Kwa leo tuishie hapo.