matunduizi
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 7,616
- 18,475
Ukiacha Ufalme wa Mungu jambo la pili lililotawala hotuba, story mifano ya Yesu lilikuwa ni Pesa/Mali na uchumi. Hili alilizungumzia sana kuliko Maombi na Imani.
Zipo sababu nyingi, ila hii ni moja ya muhimu sana.
Umasikini ni utumwa. Mwenye mali atatumikiwa na wasionacho. Hii ni kanuni. Yesu alitaka wafuasi wake wawe na uhuru wa kifedha (financial freedom) ili katika hali zote wasiwe watumwa wa matajiri wa dunia hii kama tunavyoona watumishi wa siku za mwisho masikini wanavyopelekeshwa na waumini matajiri.
Ndio maana anasema yeye alifanyika kuwa masikini ili sisi tulio masikini tupate kuwa matajiri.
2 Wakorintho 8:9
Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.
Mwisho Yesu anajua mwenye uhuru wa kifedha ndio mwenye influence au ushawishi. Ndio maana hata yeye baada ya kufa sasa hivi anatawala kama mfalme wa wafalme mmiliki wa kila kitu. Kwa sasa anainfluence kubwa kuliko alipokuwa duniani ndio maana anasema kwa sasa wanaomfuata watafanya makubwa kuliko enzi zake.
Mwenye uhuru wa kifedha hata akiongea pumba watu hupiga makofi. Je sio zaidi ukiwa huru kifedha huku umejazwa madini ya roho mtakatifu?
Tafakari, chukua hatua.
Ni hayo tu.
Mtumishi Matunduizi