Hii nchi wanasiasa wanatuchezea, nimemua kuishi kivyangu na lolote litokeee wala sijali

Makonde plateu

JF-Expert Member
Nov 19, 2022
1,360
3,316
MSHAHARA WA WABUNGE HAUENDANI NA WANACHOKIFANYA BUNGENI.

Na Thadei Ole Mushi.

Ukiangalia Mshahara wa Mbunge na anachokifanya Bungeni vinatia Hasira Sometimes…

Twende Sawa

Rais Magufuli ndiye Rais aliyevunja Rekodi ya wabunge kuweka maazimio ya kumpongeza Bungeni. Maazimio ya mwisho mwisho kabla hajafa ni lile lilowekwa na Bunge Kumpongeza kwa kufanikisha kuifurusha Corona nchini 😀😀😀 ikaondoka zake. Azimio Lingine ni lile la Kumpongeza kwa Kununua Korosho za Mtwara kwa kutumia JWTZ mpaka anafariki Mzee JPM alikuwa ana maazimio zaidi ya 10 ndani ya bunge kumpongeza kwa mambo mbalimbali.

Jana Bunge limehamia rasmi Kwa Rais Samia. Wameanza na Azimio la Kukuza Demokrasia nchini na Kukuza Diplomasia ya Uchumi.

Kilichofanyika hapa ni Kuwa Wabunge wameamua tu kubadili frequency za medula zao na kuhamia kwenye frequency walizohamia wapinzani. Sio kwamba wanatoa Pongezi za Kweli lah hasha wameamua tu kwenda kuwachezea Rafu wapinzani kwa kuwa nao wapo kwenye frequency hizo hizo za kumpongeza mama Samia.

Kwa wanaoweza kuona Mbali ni kwamba Wabunge wa CCM wanachokitafuta ni kuwahamisha wapinzani kwenye frequency hizo za masifu na litania…. Ili wabakie peke yao na ndio wenye haki ya kumsifu Rais. Wanafanya hivi katika Hali ya Kumtengeneza Rais Samia awasaidie Kushinda uchaguzi wa 2025…. Chadema nao wanamsifu sana Rais Samia ili asiingilie Mchakato wa Uchaguzi 2025 angalau malengo yao ya kurejesha majimbo yao yafanikiwe. Matokeo yake wote Upinzani na CCM wanashindana kumsifu Rais na majukumu yao ya Msingi wote wameachana nayo sasa wanasaka ubunge….. ubunge ni Mtamu sana.

Mshahara wa wabunge.

Kwa Mujibu wa kanuni za bunge Mbunge huvuna yafuatayo kwa Mwezi…….

1. Mbunge hulipwa mshahara kwenye scale ya LSS (P) 2 ambayo mshahara wake ni Shilingi 4,600,000.

2. Atalipwa posho ambazo kwa Mwezi hufikia Shilingi 8,292,000 katika mchang'anuo ufuatao.

✓ Atalipwa posho Kwa ajili ya mafuta ya gari yake Shilingi 3,750,000.

✓Atalipwa Posho Kwa ajili ya Matengenezo ya Gari yake Shilingi 1,500,000.

✓Atalipwa Posho inayoitwa (Posho ya Mbunge na matumizi mengine jimboni) Shilingi 1,000,000.

✓ Atalipwa Posho ya kujikimu ya siku 10 kama atajisikia kwenda Jimboni Shilingi 450,000.

✓ Atalipwa Posho ya kujikimu kwa Wasaidizi wake watatu Kwa siku kumi atakazokuwa jimboni Shilingi 900,000 hapa kama atajisikia kwenda Jimboni au kwa mchepuko Dar 😂

✓ Atalipwa Posho ya watumishi watatu kama atajisikia kuajiri (Mhudumu wa Ofisi yake, Katibu wake, na Dereva) katika mchang'anuo ufuatao.

Katibu wake Shilingi 352,000 Mhudumu 170,000, Dereva 170,000. Jumla Shilingi 692,000. Hapa ni kama atajisikia kuajiri sio lazima.

Jumla ya Fedha zote zinafika Shilingi 12,892,000.Fedha hizi zote zinaingia kwenye account yake Mbunge.

Fedha zote hizo ni nje ya Sitting allowance ambazo atalipwa Mbunge akiwa kwenye vikao vya bunge. Mfano bunge la sasa la bajeti litatumia Siku zisizizopingua 84 chukua siku 84 zidisha kwa 200,000 utapata 16,800,000 hizi ni za kikao kimoja cha bajeti.

Sifa kubwa ya kuwa Mbunge ni kujua kusoma na kuandika …..🤔🤔🤔🤔

Watumishi wengine nchini….Kabla ya kuanzia Tanzania hebu tuchungulie hapo Kenya kidogo….

Mwalimu wa Sekondari mwenye miaka miwili kazini nchini Kenya hulipa Ksh 73,200 ambazo ni sawa na shilingi za kitanzania 1,545,296.

Kila baada ya miezi 28 sawa na miaka miwili na Miezi minne walimu nchini Kenya increment ni asilimia 4%. Kwa hiyo mwenye miaka miwili kazini baada ya miaka miwili ataongezewa sh za Kitanzania 60,000. Hapa nazungumzia walimu wapya kabisa kazini. Fuata link hii kusoma zaidi kuhusu Kenya :-


Kwa Tanzania Mwalimu mwalimu mwenye degree Moja anaanza na mshahara wa D1 Basic salary ni 716,000 take home 540,000.

Huyu mwalimu kwenye Mshahara wake anakutana na yafuatayo:-

Bodi ya Mikopo 15%, Income Tax 10% ,Mifuko ya Jamii 5% ,Bima ya afya 3% ,CWT 2%. Jumla ya makato yote ni asilimia 35 ya mshahara wote.

Yaani karibia Nusu ya Mshahara unarudia ulipoingilia. Akijichanganya tu huyu mwalimu akakopa kwenye Ile bank yetu pendwa tunayochukulia mishahara lazima aongee Mwenyewe Barabarani.

Hapo hatujamwekea Kodi ya nyumba labda kwa nyumba ya kawaida kabisa 150, 000 huyu Ni bachela ambaye hajaoa ili apate sebule chumba kimoja na Jiko. Ukitoa pale kwenye 540,000 inabakia 390,000. Toa hapo Chakula Cha mchana na jioni kwa maana ya kuanzia chai, Chakula Cha mchana, Chakula Cha jioni tufanye vyote hivyo vimegarimu 5,000 kwa Mwezi atatumia 150,000 ukitoa pale kwenye 390,000 iliyobaki inabaikia 240,000. Tutoe hapo nauli shule nyingi hazina nyumba za walimu tuweke tu kwa siku nauli ya 1000 kwa Mwezi elfu 30,000 hapo Ni umekuwa na nidhamu ya Kutosha ukitoa pale inabakia 210,000 hujalipa maji na Umeme na hujathibutu kununua Shati hata moja.

Huyu ni Mwalimu aliyeanza na Degree moja atakayeanza na certificate huwa haelewi kinachoendelea huwa anashangaa tu mpaka anastaafu….. akistaafu anatwangwa na Kikokotooo anaamua kufuata watenda Miujiza huko mtaani wanamwambia weka hela hapa itazaa anaweka anatapeliwa anabakia kuongea mwenyewe njiani.
 
^The ultimate tragedy is not the oppression and cruelty by the bad people, but the silence over that by the good people.^ Martin Luther King, Jr.

^...the only thing it takes for evil to succeed is for good men to do nothing.^
 
Aisee inasikitisha na kuhuzunisha sana. Kwangu mimi, chanzo cha haya yote ni ccm. Hiki chama hakina faida yoyote ile kwa Watanzania.
 
Mapendekezo.
1. Mawaziri wasitokane na wabunge.
2. Uwakilishi wa majimbo ufutwe badala yake kuwe na uwakilishi kiwilaya. Hii itapunguza idadi ya majimbo.
3. Punguza posho za wabunge kwa 75%
4. Vipindi vya kugombea ubunge visizidi viwili.
5. Futa nafasi za viti maalum.
 
Walimu mnapenda kulia lia sana huo mshahara scale wa D1 ni kwa bachelor degree wote wa 3yrs course wanaoajiliwa serikali kuu wizarani na kwenye almashauri..

Sasa nyoe sijui mnataka nn kwamb muonekane mnanyanyaswa sana.

Nikwamba huwezi kuwa tajiri kwa mshahara wa serikali hao mnaosikia wanadegree na wanalipwa sijui 1.mil, 2 milli hawafiki hata theruthi ya wafanyakazi wote.

Kwa upande mwingine i can feel your pain yapo mashirika ya umma mengi yanalipa wafanyakazi mishahara na posho kubwa ilhali wanaingiza hasara serikali kila siku hapo serikali itazame kama shirika haliingizii serikali faida mishahara ishushwe iendane na ile ya wizara..

Kuwa shirika au taasisi aina maana mishahara iwe mikubwa bali ni kuongeza ufanishi katika kutoa huduma ili serikali inufaike matokeo ya huduma safi na nzuri ndio pato kuongezeka na posho na hayo malupulupu walipane humo..
 
Sifa kuu ya mbunge ni kujua kusoma na kuandika, total income ya mwezi ni 12.8m.

Sifa kuu ya mhandisi(engineer) ni elimu ya chuo kikuu, degree ya miaka minne huku akipambana na michoro, mahesabu makali yenye precision ya hali ya juu ili asijekosea kutengeneza miundombinu iwe ya kieleckroniki, kiujenzi, kidijitali....mshahara wake ni l 1000k kutegemeana na kampuni au taasisi.

Ndio maana jamaa wapo radhi wakuue ili wakakalie viti vya bunge.
 
Walimu mnapenda kulia lia sana huo mshahara scale wa D1 ni kwa bachelor degree wote wa 3yrs course wanaoajiliwa serikali kuu wizarani na kwenye almashauri..

Sasa nyoe sijui mnataka nn kwamb muonekane mnanyanyaswa sana.

Nikwamba huwezi kuwa tajiri kwa mshahara wa serikali hao mnaosikia wanadegree na wanalipwa sijui 1.mil, 2 milli hawafiki hata theruthi ya wafanyakazi wote.

Kwa upande mwingine i can feel your pain yapo mashirika ya umma mengi yanalipa wafanyakazi mishahara na posho kubwa ilhali wanaingiza hasara serikali kila siku hapo serikali itazame kama shirika haliingizii serikali faida mishahara ishushwe iendane na ile ya wizara..

Kuwa shirika au taasisi aina maana mishahara iwe mikubwa bali ni kuongeza ufanishi katika kutoa huduma ili serikali inufaike matokeo ya huduma safi na nzuri ndio pato kuongezeka na posho na hayo malupulupu walipane humo..
Mkuu,
Kwa hiyo unaona sawa mtu mwenye sifa ya kusoma na kuandika alipwe 12.8m huku hana tija yoyote katika kuongeza ufanisi kiuchumi?
 
Ticha mpwayungu na account nyingine kaamua kufungua account ya jina la some pendwa
 
Ndiyo sababu wengi wao ni washirikina na makahaba/malaya wa kike na kiume waliokubuhu
 
Hapa huwezi wakuta kina Mmawia
Erythrocyte
Tindo
Heche,Msigwa,Mbowe!

Wanasiasa wa Tanzania wameunda Cartel ya kuwafilisi watanzania!

Wanasiasa wa kitanzania ni wasaka Tonge!

Nakubaliana na Thadei ole mushi
 
Hapa huwezi wakuta kina Mmawia
Erythrocyte
Tindo
Heche,Msigwa,Mbowe!

Wanasiasa wa Tanzania wameunda Cartel ya kuwafilisi watanzania!

Wanasiasa wa kitanzania ni wasaka Tonge!

Nakubaliana na Thadei ole mushi
Hoja yako umeiharibu kwa kuleta ushabiki wa kijinga. Kwa nini huioni ccm kama chanzo Cha huo upuuzi wote?
 
Mkuu,
Kwa hiyo unaona sawa mtu mwenye sifa ya kusoma na kuandika alipwe 12.8m huku hana tija yoyote katika kuongeza ufanisi kiuchumi?
Kwa muundo wa majukumu yao wanastahiki kupata hiyo pesa na ni ndogo ila kwa kuwa nchi na wanachi wenyewe wameamua kutokuwa serious basi tunajienda tu.
 
Back
Top Bottom