uttoh2002
JF-Expert Member
- Feb 3, 2012
- 15,934
- 29,971
Kwa kweli ndugu zangu wa Tanzania, haya ni mambo ambayo yanasikitisha na kuonyesha hii nchi haitujali kwa dhati (Unaweza ongeza yako) :
1. Hivi inawezekanaje ni agenda serious Kabisa kwamba watu tufunge Mikanda (Jambo jema sana), Lakini kuna Magari ya abiria yenye leseni, Bima, safe sticker na gari zima halina Mikanda?
2. Hivi inawezekanaje mtu upande Bus ushushwe kwenye mgahawa, unapewa a plate kwa 8000/- wali haujaiva, chips boko boko kama ugali, nyama hazijaiva, huna option? Mamlaka zipo.
3. Hivi inawezekanaje Makonda, kada wa CCM mwenye lawama za kutosha na uonevu mkubwa, anaongozwa na msafara wa magari ya serikali ya mamilioni, lakini vijijini Wakina Mama zetu wanakufa sababu ya kususwa na manesi ambao hawalipwi vizuri wanalazimisha rushwa?
4. Hivi inawezekanajae trafic kusimama mahali ambao barabara ni mbovu, na hatari kusimama, anakusimamisha, hakuna pa kupaki, kuna siku niliwashawahi kugongwa, yani sio salama, sasa malengo ya trafic ni nini?
5. Hivi inawezekanaje mifumo ya serikali, mfano sumatra, inaweza kuwa na Shida hata week nzima, na ukienda unajibiwa hovyo, hapo nje kuna watu ambao wanakuongelesha kwamba wanaweza kukusaidia kwa charges?
6. Hivi inawezekanaje, nimepita TRA, nimepata clearance, nimefanikisha kila kitu kwa mateso Latra, naenda office ya Latra asubuhi ili niwahi kwenye kazi, najikuta mwenyewe, nangoja steaker kwa saa nzima, na kujibiwa hovyo? Ni sawa kweli?
7. Hivi inakuwaje mimi naleta serikalin hela yangu ya kodi, kamili na kwa uaminifu, leseni au mambo mengine, ili muipokee lazima nitoe rushwa? Hivi jamani huu ni utu kweli ndugu zangu.
8. Jamani, jamani! HAKUNA ajira, hii nchi, tumekubali, ni sawa, wacha vijana wetu wa pambane, ila:
1. Wanajiajiri.
2. Umeme unakatika.
3. Ratiba hakuna
Swali : Hivi mnafikiri hawa vijana watajipanga na kazi zao bila ratiba ya umeme? Jamani? Kutoa ratiba kuna shida gani?
Hemu fikirieni:
Mnajua ni vijana wangapi wako kwenye hizi field? Wameoa, wanasomesha, waishije?
Baada ya kuwanyima umeme, TRA wanapita na tangazo, lipa Kodi yako kwa maendeleo ya Taifa, this is day light robbery.
Baada ya machungu yote haya, report ya CAG inakuja na maelezo ya kutosha juu ya wizi wa watumishi wa serikali, Hakuna hatua mnachukua!!!!!!!!!????????
Hivi serikali, sisi wananchi tumewakosea nini? Hemu tuambieni basi leo ili tuombe msamaha, tumalizane, tuishi kwa amani!

- Saloon
- Beauty parlors
- Mafundi wa kuchomea
- Magereji
- Wafyatua matofali