Hii Mikopo ya Bajaji sasa imekua kama kausha damu, tuwe makini

monotheist

JF-Expert Member
Apr 30, 2017
792
1,294
Pitapita zangu maeneo ya town nikaona bango kubwa linalohusu mkopo wa bajaji na pikipiki nikaamua isiwe shida ngoja nijisogeze yaliyojiri ni kama yafuatayo;
Aina ya bajaji ni RE
Kianzio cha mkopo ni 700,000 na marejesho kwa siku ni 28,000 kwa miaka miwili inamaana hapa ndani ya miaka miwili unarejesha zaidi ya 20 milion aisee huu ni unyonyaji wa hali ya juu

Halafu nimekutana na jamaa pale ndo anatoa hiyo pesa anafurahi na kusema marejesho ya elfu 28,000 kwa siku kwake haisumbui huyu jamaa atakuja juta baadae
IMG_20241004_132706.jpg
 
Hiyo kampuni marejesho sio 28,000 ni 27,714 ambapo kwa wiki ni 194,000 faida yake ikiharibika wanatengeneza wenyewe kwa kipindi chote cha mkataba 2yrs. Kuna kampuni rejesho ni 31,200 na kila kitu ni kwa dereva.
Hii inafanyika hata kwa maboss wa mtaani na ni kawaida kabisa walio katika kiwanda hiki wanajua ndio maana kelele hamna.
Kwa kiasi flani haya makampuni yamekuwa mkombozi kwa watu kwasababu maboss wa mtaani manyanyaso yalikuwa makubwa sana kwa madereva wengine wanasubiria mkataba unataka kuisha anakutafutia makosa anakunyanganya chombo
 
Wewe ni. Wakala wa Hilo kampuni
 
Back
Top Bottom