Hii imekaaje ndugu zangu wazazi

Bando la wiki

JF-Expert Member
May 23, 2023
723
2,502
Mimi ni kijana mwenye mtoto wa miaka 5. Nina ukaribu sana na watoto yaani kwa kifupi mimi hupenda sana michezo na kuhakikisha watoto wanapata furaha na kucheka.
Uzuri wangu mtoto akikosea huwa sipendi masihara nae, anakula mboko za kutosha. Najiepusha nisimpige kwa hasira sana kwa mikono au mabuti, mimi ni mwendo wa bakora tu kwa mtoto wangu huyu. Bakora zinakuwa heavy kwenye makalio kwa muda mfupi tu (namshukuru Mungu kwa hilo kwa sababu husipo control hasira wakati unamuadhibu mtoto ni risk sana kwa kizazi hiki)

Kinacho nishangaza kwa mwanangu, ni baada ya kula fimbo za kutosha haipiti dakika 10 baada ya kumaliza kulia hurudi kwangu kwa furaha na kunipigisha story sana. Tunaanza ukarasa mpya wa kucheka na kufurahi.
Hii imekaaje wazazi au ndo kusema mtoto huwa hakumbuki zile fimbo nilizomtandika? Hivi watu wazima tungepewa moyo thabiti kama watoto hii dunia nadhani ingekuwa ya amani sana.
 
Mathayo 18:2-4
[2]Ni nani basi aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni? Akaita mtoto mmoja, akamweka katikati yao,
[3]akasema, Amin, nawaambia, Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.
[4]Basi, ye yote ajinyenyekeshaye mwenyewe kama mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni.
 
Back
Top Bottom