Hii hapa mikoa 12 inayoendesha uchumi wa nchi, inamiliki na kushikilia asilimia 70% ya uchumi wa Tanzania

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
54,357
64,392
Kwa Mujibu wa Takwimu za NBS za mwaka 2023 kutoka Kwenye Chapisho la Tanzania in Figures 2023 Limebainisha masuala kadhaa ya takwimu za msingi za Nchi.

Moja kati ya takwimu hizo ni Mchanganuo wa Uchumi wa Kila Mkoa Kwa Tanzania Bara.

Kwa Mujibu wa Takwimu hizo , imebainisha Mikoa 10 ambayo imeshikilia Uchumi mkubwa wa Tanzania yaani yenye Pato la Mkoa (Regional GDP) ya kuanzia kuanzia Shilingi Trilioni 6.7 Hadi Trilioni 32.2.

Mikoa hiyo 10 inashikilia zaidi ya asilimia 70% ya Uchumi wa Nchi huku Mikoa mingine 14 Kwa pamoja ikibakia na asilimia 30% tuu.

Kiufupi mpaka hapo inaonesha umaskini mkubwa huko Mikoani Kwa sababu haiwezekani Mikoa 12 iwe na Uchumi mkubwa kushinda Mikoa 14. Hapa Serikali Ina kazi ya kufanya.

Orodha ya Mikoa hiyo Heavy Weights na Pato la Kila Mkoa (Trilioni) ni ;

A)Kundi La Kwanza(Top 3 Regions)-Mikoa yenye GDP Zaidi ya Trilioni 10.

1.DSM =32.2
2.Mwanza =13.5
3.Mbeya =10.7

B)Kundi La Pili-GDP Kuanzia Trilioni 8.0-9.9

4.Arusha=8.8
5.Tanga=8.8
6.Morogoro=8.8
7.Geita=8.6
8.Kilimanjaro=8.2

C)Kundi La Tatu-GDP kuanzia Trilioni 6.5-8.0

9.Ruvuma=7.1
10.Shinyanga=6.7
11.Mara=6.7
12.Tabora=6.7

My Take
•Mikoa ya Ruvuma, Shinyanga, Mara, Geita na Tabora ni game changer kwenye Uchumi wa Nchi, kutoka kusikojulikana hadi kuwa Mikoa muhimu ni jambo la kupongezwa na kuonesha kwamba kumbe ukifungua Nchi Kwa miundombinu Uchumi unafufuka.

•Dodoma ni Makao Makuu ya Nchi lakini haichangii chochote Cha maana kwenye Uchumi wa Nchi.Pwani inaongoza Kwa viwanda Tanzania lakini ni kama havina Msaada wa Moja kwa kwenye Uchumi wa Mkoa labda mauzo ya Nje ya Nchi nk.

•Mwisho, Serikali Ipeleke rasimali za Kutosha kwenye Mikoa ya Mwanza na Mbeya kulingana na Mchango wao kwenye Uchumi.
Haipendezi kuchukua jasho la watu wa Mikoa mingine na kwenda kujengwa Dar, Dodoma na Arusha. Mgawanyo wa Rasilimali ufanyike Kwa uwiano mzuri.

•Mikoa ya Kaskazini (Tanga,Arusha, Kilimanjaro) Inaonekana Iko Very Stable Kiuchumi,Kila takwimu muhimu huwezi ikosa.



Angalizo:
•Uchambuzi huu sio rasmi Bali ni abstract tuu,hivyo uchukuliwe Kwa lengo la kutoa picha ya Juu Juu kuhusu Hali ya Uchumi wa Mikoa.

•Uchambuzi rasmi na takwimu rasmi za matumizi ni zile zinazotolewa na mamlaka husika kama NBS,ESRF,FinScope,BoT nk.

Pia soma Mikoa 10 Yenye Watu Maskini Zaidi Tanzania :Kagera namba 2, Dodoma namba 5.Nini Kinaiponza Mikoa Hii Maarufu?
 

Attachments

  • sw-1721204106-2023 Tanzania in Figure Kiswahili.pdf
    2.1 MB · Views: 7
Tabora ni kwasababu ya tumbaku kupanda bei katika miaka ya hivi karibuni
 
1. Kama Njombe haipo kwenye top 10, hiyo ripoti inaweza ikawa imechakachuliwa

2. Kama kila mkoa ungeruhusiwa utumie mapato yake kwa maendeleo yake, Arusha pangekuwa pameendelea zaidi ya ilivyo sasa.
 
1. Kama Njombe haipo kwenye top 10, hiyo ripoti inaweza ikawa imechakachuliwa

2. Kama kila mkoa ungeruhusiwa utumie mapato yake kwa maendeleo yake, Arusha pangekuwa pameendelea zaidi ya ilivyo sasa.
Umekurupuka hujaelewa mada.

Pili muendelee kuzidi hapo wakati Hadi hapo mumetumia pesa za wengine 🤣🤣🤣🤣

Inaelekea watu wengi hamuelewi hata maana ya GDP
 
Uchumi wa Mikoa 4 ya Kundi la Pili ndio Dsm peke yake,tunatakiws tutoke huko walau Mikoa 2 inayofuatia Dar ndio walingane Kwa Uchumi,hii gap ni kubwa sana.
Ruvuma kuna uvunaji mkubwa sana wa Makaa ya mawe unaendelea. Huu uvunaji hauna impact ya moja kwa moja kwa mwananchi wa kawaida wa Ruvuma zaidi ya kuongeza mapato ya Mkoa na Taifa. Maisha ya wanaruvuma bado ni duni sana kusema kweli.

Kila mara nasema itungwe sheria kulazimisha sehemu ya mapato yatokanayo na rasilimali ibaki eneo husika ili kusaidia maeneo hayo kuinuka kiuchumi. Kwa sasa wanaruvuma wanashangaa tu malori maelfu kwa maelfu yanasomba mkaa kila uchao bila faida yoyote kwao
 
Nimefurahi kuona mkoa wetu wa Morogoro unafanya vizuri.
 
Mfumo wa Uchumi wa Nchi unasababisha hivyo,mnachoambulia ni service levy Kwa level ya Halmashauri basi ila Kwa maeneo husika labda CSR ambayo nayo Halmashauri ndio inaamua.
 
Ndugu zetu Ishomile siwaoni
Nahisi Kagera "inaonewa". Mkoa mzuri kama huu usingepaswa kutajwa miongoni mwa mikoa masikini. Nipo kwenye gari naelekea Ngara mjini nikitokea Rulenge. Mkoa ni mzuri sana.
1. Hali ya hewa nzuri!
2. Milima ya kuvutia
3. Ardhi yenye rutuba. Uoto wake na mazao ya migomba unathibitsha hilo.

Sioni sababu ya Kagera kutokuwa "tajiri"
 
1. Kama Njombe haipo kwenye top 10, hiyo ripoti inaweza ikawa imechakachuliwa

2. Kama kila mkoa ungeruhusiwa utumie mapato yake kwa maendeleo yake, Arusha pangekuwa pameendelea zaidi ya ilivyo sasa.
Hakuna kitu kama hicho, Arusha wanajionaga wa mbele sana. Hivi unajua wanachoringia Arusha ni matajiri wachache wenye hela nyingi ambapo matajiri hawa wachache hawawezi kuwa sehemu kubwa ya maendeleo ya mkoa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…