Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,850
- 34,294
Play video, "Watch: Small explosion in Lebanon supermarket", Muda 0,22
00:22
Maelezo ya video,Tazama: Mlipuko mdogo katika duka la jumla la Lebanon
20 Septemba 2024
Wakati umati wa watu ulipokuwa umekusanyika kuomboleza baadhi ya waliouawa katika wimbi la mashambulizi ya bomu Jumanne, mlipuko mwingine ulisababisha kutokea kwa hali ya sintofahamu huko Dahiyeh, ngome ya Hezbollah kusini mwa Beirut.
Katika eneo jirani hali ya kuchanganyikiwa ilitokea wakati sauti ya mlipuko iliposikika mitaani.
Kuombeleza kukasitishwa ghafla. Wale waliokusanyika walitazamana, wengine bila kuamini kilichotokea.
Ripoti zilipokuwa zikienea kwamba hii ilikuwa sehemu ya wimbi la pili la milipuko ambayo sasa inalenga redio za mawasiliano, hakuna vifaa vya kielektroniki vinavyochukuliwa kuwa salama.
Huko Dahiyeh, wafuasi wa Hezbollah walisimamisha timu yetu mara kadhaa, wakitaka tusitumie simu au kamera zetu.
Mmoja wa watayarishaji wetu alipokea ujumbe kutoka kwa rafiki, ambaye alisema alikuwa amebadilisha kadi ya simu yake ya Lebanon hadi nambari ya kimataifa, akihofia kuwa simu yake inaweza kulipuka pia.
Watu wengi hapa, na kote nchini, bila shaka wanajiuliza ni nini kitakachofuata. Wengine hata wanasema hawajui ikiwa ni salama kutembea karibu na watu wengine, na wanabadilisha mipango yao.
"Kila mtu ana hofu tu... Hatujui kama tunaweza kukaa karibu na vipakatalishi au simu zetu za mkononi. Kila kitu kinaonekana kama hatari kwa wakati huu, na hakuna anayejua la kufanya," mwanamke mmoja, Ghida, alisema.
Mkanganyiko huo ulizidishwa na uvumi ulioenea kwenye mitandao ya kijamii. Mmoja wao alipendekeza kuwa hata paneli za jua zinalipuka. "Hali ya hofu ilitanda kila mahali," mwanamke mwingine alisema. "Ukweli kabisa hali hii inatisha sana."
Shambulio la Jumatano, ambalo liliua watu 25, limetokea wakati nchi bado imeshangazwa na kukasirishwa na kile kilichotokea siku iliyopita, ambapo maelfu ya vifaa vya mawasiliano vililipuka katika shambulio lililopangwa, baada ya watumiaji kupokea ujumbe ambao waliamini ulitoka kwa Hezbollah.
Vifaa hivyo vililipuka wakati watu walikuwa madukani, au na familia zao nyumbani, na kuua 12, akiwemo msichana wa miaka minane ambaye alienda kuchukua kifaa cha mawasiliano ili kumpa baba yake, na mvulana wa miaka 11.
Takriban wengine 2,800 walijeruhiwa, huku mamia wakihitaji kufanyiwa upasuaji.
Akiwahudumia baadhi ya waliojeruhiwa, Dk Elias Warrak alisema takriban asilimia 60 ya watu aliowaona baada ya milipuko hiyo ya Jumanne walipoteza angalau jicho moja, huku wengi wao pia wakipoteza kidole au mkono mzima. Aliielezea kama "siku mbaya zaidi ya maisha [yake] kama daktari".
"Ninaamini idadi ya majeruhi na aina ya uharibifu ambao umefanyika ni mkubwa," alisema. "Kwa bahati mbaya, hatukuweza kuokoa macho ya watu wengi, na kwa bahati mbaya uharibifu hauko kwenye macho tu - baadhi yao wameathirika ubongo pamoja na uharibifu mwingine wa uso."
Mashambulizi hayo ni ya kufedhehesha Hezbollah inayoungwa mkono na Iran, na dalili zinaonesha mtandao wake wote wa mawasiliano unaweza kuwa umeingiliwa na Israel, ukiukaji mbaya zaidi wa usalama katika historia ya kundi hilo.
Ripoti zinaonyesha shehena ya vifaa vya mawasiliano huenda viliingizwa vilipuzi, kabla ya kulipuliwa kutoka mbali.
Hezbollah ilikuwa imesambaza vifaa hivyo huku kukiwa na wasiwasi kwamba simu za mkononi zilikuwa zikitumiwa na jeshi la Israel na mashirika ya kijasusi kuwasaka na kuwaua wanachama wake.
Bado haijabainika ni vipi mashambulizi ya Jumatano huenda yalitekelezwa.
"Maumivu ni makubwa, ya kimwili na ya moyoni. Lakini hili ni jambo ambalo tumelizoea, na tutaendelea na mapambano yetu,” alisema kijana mmoja katika eneo la Dahiyeh.
Mwanamke mmoja alisema: “Hili litatufanya tuwe na nguvu zaidi, aliyepoteza jicho atapigana kwa kutumia jicho jingine na sisi sote tunasimama pamoja.”
Hezbollah imeapa kujibu, ikiilaumu Israel kwa mashambulizi hayo. Kama kawaida, Israel haijatoa maoni yoyote. Hofu inayoongezeka tena ni kwamba, machafuko ya sasa kati ya maadui hao wawili, ambayo yamesababisha makumi ya maelfu ya wakaazi wa pande zote mbili za mpaka kuyahama makazi yao, yanaweza kuongezeka na kuwa vita vya pande zote.
Chanzo cha picha,Getty Images
Hezbollah inasema mashambulizi yake dhidi ya Israel, ambayo yalianza takriban mwaka mmoja uliopita, yana mshikamano na Wapalestina huko Gaza, na kwamba yatakoma tu kwa kusimamisha mapigano, jambo ambalo ni gumu kwa sasa.
Saa chache baada ya milipuko ya hivi karibuni, waziri wa ulinzi wa Israel, Yoav Gallant, alisema nchi yake ilikuwa "mwanzoni mwa awamu mpya ya vita", huku kitengo cha 98 cha jeshi la Israel kikihama kutoka Gaza kuelekea kaskazini mwa Israel.
Hadi sasa, Hezbollah imedokeza kwamba haina haja na vita vingine vikubwa na Israel, huku Lebanon ikihangaika kujikwamua kutokana na mzozo wa kiuchumi uliodumu kwa miaka mingi.
Wengi hapa wanasema mzozo hauko kwa maslahi ya nchi. Hezbollah iliyoharibiwa pia haiko kwa maslahi ya Iran, kwani kundi hilo linajiendesha kama lenye kujizuia dhidi ya Israel.
Lakini wengine hakika watadai jibu kali. Dalili ya kile Hezbollah inaweza kuwa inapanga kufanya inaweza kujitokeza siku ya Alhamisi, na itakuwa mara ya kwanza kujitikeza kwa umma kwa kiongozi wake mwenye nguvu, Hassan Nasrallah. chanzo.BBC