Hezbollah wathibitisha kuuawa kwa kamanda wao, Ali Karaki ambaye ameuliwa na Israel

MK254

JF-Expert Member
May 11, 2013
32,237
50,402
Hezbollah imethibitisha Jumapili kwamba kiongozi wake wa juu Ali Karaki aliuawa katika shambulio la anga la Israeli kwenye kitongoji cha kusini mwa Beirut, shambulio ambalo pia liliua kiongozi wa kundi hilo, Hassan Nasrallah.

Israel ilisema ilimuua Nasrallah katika shambulio la anga kwenye makao makuu ya Hezbollah katika vitongoji vya kusini mwa Beirut Ijumaa hukuHezbollah ilithibitisha kuwa kiongozi huyo aliuawa Jumamosi.

Kundi hilo linaloungwa mkono na Iran limesema katika taarifa yake ya Jumapili kwamba Karaki alikuwa kamanda wa eneo la kusini tangu mwaka 1982.

Na kuongeza kuwa Karaki alishiriki katika mapambano makuu dhidi ya Israel mwaka 2000, Julai 2006, na hivi karibuni alikuwa na jukumu la moja kwa moja kuongoza eneo la kusini kwa ajili ya kuunga mkono Gaza wakati wa vita vinavyoendelea kati ya Israel na Gaza.

===========================================

Hezbollah confirmed on Sunday that senior leader Ali Karaki was killed in the Israeli strike on Beirut’s southern suburb that also killed the group’s leader Hassan Nasrallah.

Israel said it killed Nasrallah in an airstrike on Hezbollah’s headquarters in Beirut’s southern suburbs on Friday. Hezbollah confirmed he had been killed on Saturday.

The Iran-backed group said in its statement on Sunday that Karaki was the commander of the southern front since 1982.

It said that Karaki participated in the main confrontations against Israel in 2000, July 2006 and most recently he was directly responsible for leading the southern front in support of Gaza amid the ongoing Israel-Gaza war.

Source: The Jerusalem Post
 
Hezbollah kupunguzwa nguvu ni faida kwa Serikali ya Lebanon pia. Manake wale ni jeshi ndani ya nchi yenye jeshi. Hezbollah hata wasipochaguliwa kwa kura bado wanaweza ipindua serikali ya Lebanon. Hezbollah inaifanya Lebanon itawaliwe na Iran bila matakwa yake. Ni yale ya DRC na Kagame wa Rwanda ndio yanafanyika huko Lebanon 🤔
 
Back
Top Bottom