HESLB yatangaza orodha ya pili wanufaika 2024/2025

Katurido Jr

Member
Jan 23, 2023
19
36
Wanafunzi wa shahada mwaka wa kwanza 30,311

Wanufaika 2,157 mikopo ya ‘Diploma’

Wanafunzi 588 kunufaika na ‘Samia Scholarship’

TZS 99.7 bilioni kutumika kuwagharimia mikopo, ruzuku TZS 2.9 bilioni

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) leo Jumatano (Oktoba 09, 2024) imetangaza awamu ya pili ya orodha ya wanafunzi wenye sifa waliopangiwa mikopo na ruzuku kwa ajili ya mwaka wa masomo 2024/2025.

Makundi ya walionufaika katika Awamu ya Pili

Orodha iliyotangazwa leo inajumuisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliodahiliwa katika vyuo mbalimbali vya elimu ya juu na vyuo vya kati waliopangiwa mikopo kwa ajili ya Shahada ya awali (30,311) yenye thamani ya TZS 93.7 bilioni. Orodha ya awamu ya pili inafanya idadi ya jumla ya wanafunzi 51,645 waliopangiwa mikopo katika awamu ya kwanza na awamu ya pili kwa ajili ya kugharimia masomo yao ya shahada ya awali ikiwa na thamani ya TZS 163.8 bilioni. Kati ya wanafunzi hao, wanafunzi wa kike ni 22,216 (sawa na 43%) na wa kiume 29,429 (sawa na 57%)

Awamu hii ya pii inajumuisha pia mikopo ya Stashahada (Diploma) kwa wanafunzi wapatao 2,157 yenye thamani ya TZS 5.6 bilioni. Wanafunzi wengine 45 ni wa shahada ya uzamili waliopangiwa mikopo yenye thamani ya TZS 205.6 milioni na wanufaika 16 wa Shahada ya Uzamivu waliopangiwa mikopo yenye thamani ya TZS 215.6 milioni.

Kuhusu kutangazwa kwa orodha ya Awamu ya Tatu

HESLB inaendelea kupokea taarifa za udahili kuwezesha kupanga mikopo na kutangaza Awamu ya tatu ya orodha ya wanafunzi waliopangiwa mikopo kwa mwaka 2024/2025 itakayotangazwa siku chache zijazo ili kuwawezesha wanafunzi waliopangiwa mikopo kuendelea na taratibu za kujisajii katika vyuo walikodahiliwa.

Samia Scholarship

Taarifa hii pia ina idadi ya wanafunzi 588 wa shahada ya awali watakaonufaika na fursa za ‘Samia Scholarships’ kwa mwaka huu 2024/2025, ambao wamepangiwa ruzuku yenye thamani ya TZS 2.9 bilioni. Wanafunzi hawa ni wenye ufaulu wa juu katika tahasusi za sayansi na waliodahiliwa katika vyuo mbalimbali kwenye fani za Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na hisabati na sayansi za Tiba.

Wito

HESLB inawakumbusha waombaji wa mikopo na ruzuku wenye sifa kwa mwaka 2024/2025 ambao bado hawajapangiwa mikopo au ruzuku, kuendelea kufuatilia taarifa za maombi yao kupitia ‘SIPA’ wakati taratibu za uchambuzi na upangaji wa mikopo na ruzuku zikiendelea.
Imetolewa na:

BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

Jumatano, Oktoba 09, 2024
 
Mm account yangu haijaandikwa chochote, ndo nisubiri mpaka batch ya3 au inakuaje hapo mtoa mada
 
Huyo amepata mkopo asubiri kupangiwa tu.

Akaunti ikishabadilika na kusoma SIPA tayari ana sifa ya kupata mkopo atapangiwa wakati wowote awe anaingia mara kwa mara kwenye akaunti yake.
VIP kwa AMBAO wapepangiwa kiasi kidogo kwa Ada Ada ya Chuo kwa MWAKA Ni millioni 7+ ila kapangiwa Ada ya mkopo 400000 itakuwaje ama ataongeewa lakin appeal inagoma kufunguka
 
Back
Top Bottom