Heslb (Bodi Ya Mikopo) Mnachowafanyia hawa wadogo zetu sijui mnataka wasisome

Mayunga234

JF-Expert Member
Feb 17, 2017
1,725
1,994
Vyuo Vingi vimeanza kufunguliwa kwaajili ya kuwapokea Mwaka wa Kwanza Na kufanya Usajili, ila ukiangalia hadi Leo Bado ya Mikopo imetoa Awamu Moja tu na hadi Mda huu hakuna kinachoendelea na vyuo vishafunguliwa Wanafunzi wanashindwa kufanya usajili kwasababu hawajui hatma yao either watapata au watakosa na wametoka nyumbani wakijua watapata mkopo,

Wanafunzi wengi walioomba mkopo hali za familia zao ni duni na wanategemea kupata mkopo ili Kuendelea na Elimu ya vyuo vikuuu

Uwaga nashindwa kuelewa criteria wanazotumia Bodi ya mikopo ili mtu aweze kupata mkopo cz nakumbuka kipindi nipo UDSM 2016 kuna wanafunzi kibao walikosa mkopo na ukiangalia Asilimia kubwa ya hao wanafunzi Wametoka kwenye familia za chini kabisa kiasi kwamba mzazi kumlipia mwanae Ada na Expenses zingine ni Changamoto ilifikia stage wengine wakashindwa kuendelea kusoma na wengine wakapostpone na wengine wakakomaa kibishi huku tukijichanga kama darasa ili waweze kulipa Ada Wengine hadi hela ya kula ni mtihan wana gongea kwa wana hivo hivo kibishi

Then ukija upande mwingine waliobahatika kupata mkopo wanaponda maisha vibaya mno tena wanapokea mara mbili kwa wazazi na bodi
Heslb sjui ni soka bet

Ila Heslb Wafikirieni sana hawa wadogo zetu waliomba mkopo yaani hadi mtu ajitutumue kuomba mkopo means hali ya maisha familia ni duni na hawana uwezo wa kulipia Ada na Expenses zingine mnawakatisha hawa madogo tamaa ya kuendelea na Elimu ya juu kwa kukosa mkopo

Hali ya kiuchumi ni mbaya kwa familia nyingi kwa sasa mkiwanyima mkopo means kuna watakaoshindwa kuendelea na Elimu ya chuo kikuuu na tutakuwa tunatengeneza sijui watu wa aina gani huko mtaaani majambazi wataongezeka, Wanaojiuza wataongezeka na matapeli pia cz hali ni ngumu

Mtaani kuna Idadi kubwa ya waliokosa ajira wakichanganyika na hawa waliokosa mkopo wa kuendelea na Elimu ya ya chuo iseee sijui itakuwaje.

Leo nimepita around ifm kuna newcomers kibao wanalalmikia bodi ya mikopo hadi sasa hawajui kinachoendelea na wametoka nyumbani wamepewa hela ya nauli na ya kula tu imagine Nawaza tu wakikosa je huo mkopo what next

HESLB ( BODI YA MIKOPO) WAPENI WANAFUNZI WOTE WALIO NA SIFA ZA KUPATA MKOPO ILI WAWEZE KUSOMA TEGEMEO LA WANAFUNZI WENGI NI HESLB
 
Mkuu wasome waende wapi? ajira hakuna, wanachoma pesa za serikali na za wazazi bure tuu. Heri hizo pesa wangewapa wajiajiri.
 
Mbongo ukizoea kumpa pesa siku ukimyima anakuchukia..anaona msaada ni haki yake kumbe sio..huo mkopo ni msaada kama msaada mwingine mana hata kulipa wengi tu hawalipi..sasa serikali ikitoa kidogo kidogo kila mtu apaye hata boom manaaza kulia lia..kwanza hela zenyewe mnenda kuhongea mademu tu na kuvinjali kusoma kwenyewe zero.

Tambua akunyimae dengu kakupunguzia mashuzi.

#MaendeleoHayanaChama
 
Hao jamaa Mungu anawaona. Walisema batch 2 wanatoa jana lkn wamehamisha magoli wanasema mpaka tar 25th.10
 
Back
Top Bottom