Heshima ina viwango, usitake heshima iliyokuzidi wengi huteseka

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
26,022
62,542
HESHIMA INAVIWANGO. USITAKE HESHIMA ILIYOKUZIDI WENGI HUTESEKA

Anaandika, Robért Heriel
Mtibeli

Heshima ina viwango vyake.
Mwingine ana 100, mwingine ana 90, mwingine 60 mwingine 30 na mwingine ni 10.

Lakini yapo mambo ambayo yatamfanya mtu aheshimiwe.

Mambo haya ni kama ifuatavyo;
1. Utu 10%
2. Tabia njema 20%
3. Kipato. 20%
4. Akili. 20%
5. Familia
6. Mamlaka 20%

Ili angalau uishi maisha ya kuona unaheshimiwa atleast ufikifikishe 70%
Na ili uone kama Watu wanakudharau basi uwe chini ya 40%

1. UTU
Kitendo cha wewe kuzaliwa tayari Watu watakuheshimu kwa asilimia 10 tuu kwa sababu ya utu tuu.

Lakini yanayo fuata lazima ujitutumue.
Wewe kuwa binadamu haimaanishi heshima yako italingana na Watu wengine kisa wote ni binadamu. Ni hiyo 10 tuu.

2. Tabia njema 20%
Watu watakuheshimu kwa tabia yako njema lakini heshima hiyo haitazidi 20%
Hiyo itakufanya uwe na 30% kwa kujumlishwa na 10% ya utu.

3. KIPATO 20%
Kipato matokeo ya kufanya kazi+ akili+ bahati.
Kadiri unavyokuwa na kipato ndivyo heshima yako inavyoimarika. Lakini haitazidi 20%
Kwa hiyo wapo wenye vipato ambao hupata heshima ya 5% kutoka kwenye vipato. Na wale waliofanikiwa kuwa na vipato vikubwa ndio huchukua 20% kama ilivyo

4. AKILI 20%
Kazi kubwa ya akili ni kumsaidia mwanadamu kuishi maisha rahisi.
Hata uwe na akili namna ipi. Heshima yako haitazidi 20%.

5. FAMILIA 10%
Kitendo cha wewe kuanzisha familia kitakupatia 10% ya heshima.
Kuitwa mke au mume ni tafsiri kuwa upo na majukumu kwa jamii katika familia yako.
Familia ni tafsiri halisi ya muungano wa hiyari wa makusudi wenye kulenga kusaidiana majukumu baina ya Mwanamke na mwanaume.
Ushirikiano wa umoja wenye kufuata haki, upendo, kweli na maarifa huifanya familia kuwa chanzo bora kabisa ya kizazi chenye mafanikio.

6. MAMLAKA 20%
Kuwa kiongozi, mtawala katika nyanja fulani huongeza heshima yako.
Ingawaje kilatu ni kiongozi wa maisha yake lakini hapa tunazungumzia kuongoza au kuwa na Mamlaka juu ya wengine. Kuwaamulia wengine.

Kadiri kundi la unalowaongoza linavyokuwa kubwa ndivyo unavyoikaribia 20% ya heshima. Yaani ndivyo heshima yako inavyoongezeka lakini haitazidi 20%.

Mgawanyiko wa heshima ya Mamlaka
I) familia 0.5%
II) Taasisi 1%
iii) jamii 2.5%
iv ) Taifa. 6%
v) Dunia. 10%

Ni ngumu kuheshimiwa kwa 100% na hakuna binadamu anayeheshimiwa kwa asilimia 100%

Kuna mambo makuu mawili yanayomfanya binadamu ahangaike kila siku. Mambo hayo ni.
1. Heshima
2. Upendo

Kwa bahati mbaya mambo hayo yanahusiana kwa ukaribu sana.
Kadiri unavyoheshimiwa ndivyo unavyozidi kupendwa.
Heshima huleta upendo.

Achana na ule upendo wa from nowhere. Upendo wa mapenzi ya mke na mume.
Hapa tunazungumzia upendo wa nje ambao unahusu mahusiano ya mtu na mtu na mtu na mazingira yake.

Elewa, heshima(upendo wa nje) huathiri upendo wa ndani.

Sio ajabu hata kwenye Familia na ndoa mke na mume walianza kwa kupendana kwa upendo wa ndani kabisa lakini kutokana na kutokuwa na heshima (upendo wa nje) baina ya mmoja wao au wote wawili kuamua kutokuheshimiana
Hiyo inasababisha upendo wa ndani kuisha.

Kuwa Mume isimaanishe utake heshima 100% wakati vigezo vingine huna.
Kuwa Mke usilazimishe heshima.

Kuwa Rais au kiongozi isikufanye utake kuheshimiwa Kama Mungu uliyeumba Watu. Wewe ni kiongozi tuu.

Heshima inaendana na Haki.

Acha nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Back
Top Bottom