kindikwili
JF-Expert Member
- Oct 5, 2016
- 1,862
- 2,875
Habari wadau!
Ni matumaini yangu kwamba sote tu wazima wa afya, binafsi nawapa pole wote walioguswa na vifo vya wadogo zetu Consolata na Maria. Nawapa moyo ndg wa mama aliyejifungua watoto wenye ulemavu sawa na akina conso na maria huko kagera. Mungu ni mwema na kazi yake haina makosa.
Nirudi kwenye mada ndg zangu, juzi kati nilitoka eneo langu la kazi kwenda kwenye majukumu mengine katika kutafuta grisi kulainisha vyuma. Nilichukua gari eneo la ITV pale mwenge nikichukua gari ya T/Nyuki kwenda kivukoni. Nikiwa kwenye gari nikajikuta niko karibu na binti moja mdogo kama miaka 15-17 hivi, huyu binti pamoja na mambo mengine alikuwa ni mzuri sana kwa sura na shepu. Ukimuona ni kama anatokea ushuani vile alivyo na ngozi nyororo na mwonekano bomba. Basi nikamuuliza jina akaniambia jina lake, nikamuuliza bado uko shule akajibu kwamba kamaliza form six Maria Goreti PCB. Stori zikaendelea na nikataka kujua kama amepangiwa kwenda JKT ambapo alinijibu kapangiwa na kwamba hataenda kwasbabu anaumwa kifua. Wakati huo tulikuwa tumefika ferry basi ile nashuka dogo kaniambia nimnunulie ICE CREAM nikatoa 2000 nikampa , basi akaniomba nimpe namba ya simu walau tuwe tunawasiliana. Akaniambia baba yake ni enginer wa wizara na mama yake ni nesi tukaagana.
Sasa ilipofika saa moja hivi usiku akanitext "njoo mbezi beach baba na mama wameenda kwenye sherehe watarudi usiku sana" . Sikumuelewa vizuri nikamuuliza unajua umemtext nani? akajibu ndiyo nikamkatalia kwa madai kwamba naishi mbali. Lakini nilibaki najiuliza huyu dogo mbona kama simuelewi elewi. Basi akaniambia njoo basi weekend mbezi tuonane, sikuwa na jibu but nikasema nitacheki. Ilipofika siku ya juma mosi akanitext "hallow" nikamjibu . Akaniambia njoo river side tuonane, kwa vile nilikuwa mwenge nikasema si mbaya. Nilipofika mlimani city nikamwambia haya njoo stendi nishfika cha ajabu hadi nafika alikuwa bado hajafika bado akaniambia nikae pub fulani hapo river side . Kufika ile pub kukawa kuna live band na muziki mkubwa sana nikaona hapanifai nikaondoka kumbe nao wakawa wanakuja yeye na binti aliyekuwa anamuita shangazi yake. Ile nafika Maua opposite na kituo cha Mabibo Hostel wakawa wamefika na pikipiki. Wakaniomba nilipe mwenye boda nikagoma maana mimi sikusema waje na boda lakini walianza kunioesha tabia za kihuni walipoanza kuiponda ile bar nadhani inaitwa MAUA wakasema pale ni pachafu , mara hapana hadhi na mengine mengi. Basi ile tunakaa nikaona ishara fulani kama za kuonesha leo tunataka kumchuna mbwa huyu mpaka akome. Kwa kutumia uwezo wangu wa haraka nikagundua wale si watu wazuri, hapo hapo nikshangaa naitwa baby bila kujua ubaby unatoka wapi. Basi alipokuja waiter wakaagiza Savanna wote wawili mimi nikaagiza Sprite maana mwenyewe si mnywaji. Nikashangaa naombwa 8600, nikauliza hivi hizi savana sh ngapi wakasema 4000. Wale mabinti wakaanza kunishangaa na kucheka wakisema mimi ni mshamba, mara nimepoe sana. Nikawajibu siwezi kujua gharama make situmii pombe. Hatujakaa ghafla wakaona watu wa jikoni wanakuja wakaanza kusema sijui hapa kuna burger mara wataje vyakula tofauti tofauti. Yule mhudumu wa chakula alipofika nikamuwahi kwamba sisi tumetosheka na kwamba vile vinywaji vinatosha. Aisee nikaanza kushambuliwa eti mimi ni bahili , nikajitetea kwamba muda huu ni muda wa kwenda kula nyumbani maana ni jioni saan moja.
Kutoka na ile hali ikabidi niage kwamba nina appointment na mtu na kwamba ananisubiri, basi wakaanza kulalamika kwamba nimewaharibia muda na appetite na kwamba nimewaharibia ratiba. Nikamuuliza yule binti mdogo ambaye ndiye nilikuwa namfahamu kwamba anaweza kunywa bia ngapi akasema kama ni bia aina ya serengeti na safari anaweza kunywa kuanzia chupa 10 kuendelea, majibu yale yalinistaajabisha sana. Niliposema naondoka nikaombwa nauli ya kurudi na kumlipa yule boda wa kwnza jumla elfu 15. Nikagoma sina hela ila nikawapa 2000. Aisee nilitukanwa matusi ya nguoni ya hatari , mara bwege , masikini, dume suruali, mwanaume gani anatembea na sh 10,000 tu na matusi mengine kibao. Yule binti mdogo anasema nisimtafute tena, wakawa wanasema waondoke waende sea cliff. Basi nikaondoka huku nikimwagiwa madogo nyuma yangu na vicheko juu. Pamoja na hayo niliweza kusave pesa zangu nlizokuwa nazo maana ndiyo nilikuwa nimetoa bank kuchukua laki 4. Nikasema heri fedheha kuliko hasara.
Jamani hali ni mbaya, inawezekana kwamba yule binti anaaga kwao kwenda kwa shangazi halafu huko anafanya ufuska au ni kwamba watoto wadogo wameingia kwenye ukahaba na kujiuza. Bado najiuliza maswali mengi juu ya huyu mtoto.
NB: Kutokana na mwandiko wake na mpangilio kwa maandishi yake yule binti hajasoma hata form four labda form four ya ukahaba.
KUWA MACHO EPUKA WASICHANA MATAPELI.
Kindi