Helios Towers, kwa Ushirikiano na Camara, Yakabidhi Maabara ya Tehama Shule ya Sekondari ya Jamii ya Wafugaji ya Endevesi, Oljoro, Arusha.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
52,329
118,597
Kampuni ya Helios Towers, Yakabidhi Darasa la Maabara ya Tehama na Compyuta 26 kwa Shule ya Sekondari ya Endevesi, ambayo ni ya watoto wa wafugaji, Eneo la Oljoro Arusha.

Kampuni ya Helios Towers, inayoongoza kwa miundombinu ya mawasiliano kwa njia ya minara, kwa ushirikiano na taasisi ya Camara Education, zimepongezwa kwa kufadhili maabara ya tehama yenye computers 26 kwa shule ya Sekondari ya Endeves ambayo ni ya watoto wa wafugaji wa Kimasai, iliyopo Oljoro, nje kidogo ya jiji la Arusha.

Akizindua maabara hiyo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Arusha, Ojung’u Piniel Salekwa, amezishukuru na kuzipongeza kampuni ya Helios kwa ushirikiano na taasisi ya Camara, kwa msaada huo na kusema serikali haiwezi kufanya kila kitu, hivyo misaada kama hii kutoka kwa wadau, inasaidia sana na kusisitiza dunia ya sasa ni ya sayansi na teknolojia, hivyo msaada huo una maana kubwa sana kuingiza shule hiyo kwenye dunia ya sasa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Helios Towers Tanzania na Mkurugenzi wa Kanda ya Mashariki ya Afrika, Gwakisa Stadi amesema kila kwenye mnara wa Helios, jamii husika hufaidika kwa kupatiwa misaada ya kijamii, hivyo msaada huo wa kufadhili maabara ya Tehama chumba cha kompyuta shule ya sekondari ya Endevesi na compyuta 28 ni moja ya utekekezaji sera ya Helios ya huduma kwa jamii, CSR.

Gwakisa Stadi alisema: " Kampuni ya Helios Towers inajivunia kuchangia katika uunganishaji wa kidigitali nchini Tanzania, barani Afrika na dunia kwa ujumla. Tunaamini kuwa miundombinu ya mawasiliano yenye nguvu, endelevu, na inayoweza kupanuka ni ufunguo wa kufungua uwezo wa kidijitali wa maeneo mengi ya vijijini zikiwemo shule kama hii.

Naye Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Godson Sukuruet ameshukuru kwa msaada huo wa maabara ya tehama ambao sio tuu utawasaidia wanafunzi wa shule yake kupata vitabu kwenye mtandao, bali pia utawasaidia waalimu wa shule hiyo kwenda kidigitali.

Kwa upande wao, wao, wanafunzi Mwanahamisi Rajabu na Daudi Loshilu, waliwashukuru wafadhili hao, Helios Towers na Taasisi ya Camara kwa msaada huo, ambapo kabla ya msaada huo, walilazimika kusafiri kilomita 30 kujifunza compyuta.

Helios Towers ni kampuni inayoongoza katika miundombinu ya mawasiliano yenye idadi kubwa zaidi ya minara barani Afrika na Mashariki ya Kati. Kampuni hii inaratibu ufanisi wa kushirikiana miundombinu na makumpuni ya mitandao ya simu (MNO) ili kufanikisha upatikanaji wa mitandao ya simu kwa haraka, kwa gharama nafuu na kuzingatia utunzaji wa mazingira kwa kupunguza matumizi ya alama za kaboni (carbon footprint). Hii kwa upande wake inasaidia upanuzi na ubora wa mawasiliano kwa njia ya simu, ikichochea maendeleo endelevu katika masoko yake.


Paskali
 

Attachments

  • Helios  Endevesi Oljoro Photo 10.JPG
    Helios Endevesi Oljoro Photo 10.JPG
    1.4 MB · Views: 3
  • Helios  Endevesi Oljoro Photo 14 .JPG
    Helios Endevesi Oljoro Photo 14 .JPG
    635.4 KB · Views: 3
  • Helios Endevesi Oljoro Photo 1. jpg.png
    Helios Endevesi Oljoro Photo 1. jpg.png
    1.1 MB · Views: 2
  • Helios Endevesi Oljoro Photo 2. jpg.png
    Helios Endevesi Oljoro Photo 2. jpg.png
    1.5 MB · Views: 2
  • Helios Endevesi Oljoro Photo 4. jpg.png
    Helios Endevesi Oljoro Photo 4. jpg.png
    1.7 MB · Views: 2
  • Helios Endevesi Oljoro Photo 5 - Mkurugenzi akizungumza. JPG.JPG
    Helios Endevesi Oljoro Photo 5 - Mkurugenzi akizungumza. JPG.JPG
    494.9 KB · Views: 1
  • Helios Endevesi Oljoro Photo 6 . Mkurugenzi Akishuhudia wanafunzi PG.JPG
    Helios Endevesi Oljoro Photo 6 . Mkurugenzi Akishuhudia wanafunzi PG.JPG
    298.2 KB · Views: 1
  • Hellios Endevesi Oljoro Photo 8 .JPG
    Hellios Endevesi Oljoro Photo 8 .JPG
    535.1 KB · Views: 2
  • Helios Endevesi Oljoro Photo 10 .JPG
    Helios Endevesi Oljoro Photo 10 .JPG
    957.9 KB · Views: 2
  • Helios Endevesi Oljoro Photo 7 .JPG
    Helios Endevesi Oljoro Photo 7 .JPG
    697 KB · Views: 2
  • Helios  Endevesi Oljoro Photo 11 .JPG
    Helios Endevesi Oljoro Photo 11 .JPG
    335.9 KB · Views: 2
  • Helios Endevesi Oljoro Photo 13 .JPG
    Helios Endevesi Oljoro Photo 13 .JPG
    308.2 KB · Views: 3
Back
Top Bottom