Zack Abdul
JF-Expert Member
- Mar 9, 2026
- 566
- 534
Ufafanuzi juu ya suala la uagizaji wa mafuta nchini kipindi cha Aprili - Juni, 2026.
Tarehe 27 Juni 2026, kupitia akaunti ya Instagram ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche, alichapisha taarifa akidai kuwa Kampuni ya Vitol imeiuzia Tanzania mafuta kwa gharama kubwa zaidi kuliko Uganda, akitumia jedwali linaloonyesha Tanzania ikiwa na premium ya USD 200–260 kwa tani huku Uganda ikiwa na USD 83 kwa tani.
Hata hivyo, ufuatiliaji uliofanyika juu ya taarifa ya Heche umebaini kuwa taarifahiyo haijawasilisha muktadha kamili wa biashara ya mafuta katika nchi hizo, hali hii inaweza ikatengeneza taswira ya kuwapotosha wananchi.
Ufuatiliaji zaidi umeonesha kuwa nchi ya Uganda iliingia mkataba wa muda mrefu na Vitol mwishoni mwa mwaka 2024. Masharti ya mkataba huo yalifikiwa kabla ya mabadiliko makubwa ya soko la mafuta yaliyosababishwa na migogoro ya kimataifa. Hivyo, kulinganisha moja kwa moja gharama za Uganda na Tanzania bila kuzingatia tofauti za mikataba siyo jambo lililozingatia uweledi katika uhitimishaji hoja yake.
Aidha, kwa upande wa Zambia, takwimu zilizotolewa na Heche hazikujumuisha gharama za usafirishaji kupitia bomba la mafuta na malori pamoja na vipengele vingine vya bei za mafuta. Kadhalika, Mfumo wa Zambia wa uagizaji wa mafuta pia unatofautiana na ule wa Tanzania jambo ambalo linaonesha upotoshaji wa makusudi uliofanywa na Heche.
Taarifa za kiuchunguzi kutoka katika vyanzo vyetu zimeeleza kuwa mwanasiasa huyo amepotosha na kutoa taarifa ambazo siyo sahihi ili kutimiza malengo yake ya kisiasa, ambapo moja ya Kampuni ya mafuta imehusishwa na jambo hilo.
Vilevile, chanzo hicho kimeeleza kuwa Heche amekubali kuingia katika mtego huo na kupanga kufanya mkutano na Vyombo vya Habari Julai 6, 2026 kuhusu suala la mafuta ili kuzima sakata la ubadhirifu na ufisadi wa fedha za michango ya chama anaodaiwa kufanya. Katika ubadhirifu huo Lema ametajwa kuanzisha sakata hilo katika Kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika Mkoani Kigoma ambapo alimtuhumu Heche kula kiasi cha shilingi milioni 60 za michango kama ambavyo Boniface Jacob (Boni Yai) alitoa shutuma ya Heche kula kiasi cha Milioni 40 na Leonard Magere akimtuhumu kula kiasi cha shilingi milioni 20.
Heche inaelezwa alikiri tuhuma hizo na kudai kuwa alijua ni michango binafsi aliopewa na wafadhili hao.
Mwisho imeelezwa Heche kulaumiwa na wajumbe wa kikao hicho kuwa ni mbinafsi asiyetaka Tundu Lissu atoke gerezani kwa kuwa Heche kipindi alichokamatwa kwa kosa la Uhaini aliwaomba ndugu zake waliokuwa Serikalini kumuombea msamaha na hatimaye akarudi mtaani jambo ambalo hajalifanya kwa Lissu.