Sangamwalogesha
JF-Expert Member
- Mar 10, 2025
- 557
- 468
Shule ya sekondari Maji ya Chai iko Halmashauri ya wilaya ya Meru, wilaya ya Arumeru mkoa wa Arusha.
Tusilaumu hizi shule, mazingira wala wanafunzi, mchawi mkubwa ni walimu na viongozi wao.
Shule hizi zimetelekezwa, walimu wanafanya shughuli zao binafsi, wengine wana vipindi shule binafsi. Hii shule tajwa hapo juu iko karibu kabisa na barabara kuu ya Arusha-Moshi, ni kilometa moja tu kutoka barabara kuu.
Headmaster wa hii shule haonekani shuleni, tunaambiwa ana shule yake binafsi, ni kwa nadra sana kufika kazini, ni mtoro wa kudumu.
Hii imefanya mpaka leo walimu hawajaanza kufundisha. Kwa mfano, mwalimu wa Physics wa kidato cha kwanza ameingia darasani mara moja tu na kafundisha "What is Physics" tu mpaka leo tunaenda mwezi wa nne.
Halafu tunakuja kutukana watoto wetu hawana akili? Physics kidato cha kwanza ina mada (topics) karibu kumi mpaka leo hawajafundishwa, kwanini watoto wasifeli?
Kwanini wasichukie masomo ya Sayansi? Headmaster wa hii shule na huyo mwalimu wake wa Physics ni wachawi wa watoto wetu.
Tunajua ndani ya Halmashauri kuna Afisa Elimu Sekondari, kuna wadhibiti ubora, kuna mkurugenzi. Wako wapi wasijue uhuni wote huu unafanyika?
Inawezekana tatizo limeanzia juu kwa waziri. Rais, mpeleke Dr. Dorothy Onesphory Gwajima Wizara ya Elimu, yule mama ni mwajibikaji. Prof. Mkenda anachojua ni kubadili mitaala na kutunga sera mpya, hayo ni makaratasi tu hayatasaidia kitu kama hakuna uwajibikaji.
Mtazamo na ushauri wangu, yule headmaster ashushwe, anyang'anywe ukuu, na mwalimu wa Physics wa kidato cha kwanza apewe onyo. Kama hataki kazi apishe, tuko wengi tunaojua Physics zaidi yake. Atupishe tusaidie watoto wetu kufikia ndoto zao.
Afisa Elimu wa pale Meru ni jamaa moja yuko na makogo tu, anafikiri cheo ni egoism, siyo kazi. Yule jamaa hajitambui, apelekwe DEO mwingine anayejua wajibu wake. Wale wadhibiti ubora waondolewe pale, kazi yao ni umbea na kusubiri muda wa chai na lunch.
Hawa viongozi wote niliowataja watoto wao wako private huku wanakula kodi zetu. Wawafuate watoto wao waliko, wafanye kazi huko.